I can dare say Yes! Mwezi wa July 1999 kulikuwa na kongamano la Mwalimu Nyerere na nilihudhuria. Lilifanyika kijijini kwake Butiama. Mwalimu nilikaa nae kti kimoja na tulipata kuongea mawili matatu. Alionekana dhaifu sana kimwili, ingawa kiakili na spiritually alikuwa bado very strong. Alikuwa amepoteza rangi kabisa naweza kusema alifanana kabisa na zeruzeru na kichwa chake chote cheupe, alikuwa akitembea kidhaifu na wakati wote alikuwa na miwani myeusi! Wengi tuliokuwa pale tulikwisha anza kuteta na kuulizana kinachomzibu Mwlm Nyerere. Afisa mmoja wa Usalama aliyekuwa karibu alitufahamisha kuwa alikuwa akiumwa muda tu kwa sasa na kuna siku moja aliwahi kumuuliza Raisi wa wakati huo B. W. Mkapa "je, umewaeleza watanzania ninachoumwa?" alimalizia afisa huyo. Alipofariki mwaka huohuo October 14 1999 niliweza kuamini kabisa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari kikiwemo cha BBC ambacho kilisema ninankuuu "The 77-year-old statesman was diagnosed with leukaemia in August 1998 and was being treated in a London hospital" tazama hapa:
BBC News | Africa | Tanzania's Nyerere dies
Sishawishiki kabisa na propaganda yeyote itakayosema kwa umri wake na hali ambayo niliishuhudia mwenyewe kwa macho kuwa atakua ameuwawa. Tayari alikuwa dhaifu sana na kama tutakumbuka aliondoka hapa kwenda kwenye matibabu na si vinginevyo! Hivyo basi, naamini kabisa, Mwl. Nyerere alifariki kwa kifo kinachotokana na ugonjwa aliyokuwa nao na si vinginevyo.