Dida Shaibu aonesha jeuri ya pesa

Dida Shaibu aonesha jeuri ya pesa

Uzuri vifo na Jela ndio huwaumbua na kuanza kupitisha michango Mpesa au kusaidiwa wapi Kajala, Ray c na wengine, wakipatwa na shida kutwa kucha kwenye media kutangaza njaa au wenzao wakiumwa wanalalamika hawana pesa, wasanii bana kweli wanafanya usanii kwenye maisha ya kweli.
 
Kila kitu hapo ni uongo labda Noah hiyo sawa, Range alipiga nayo pic alivyoenda US na hiyo si nyumba yake. Kwanini sijui magazeti mengine wana tabia ya kudanganya watu mchana kweupe. Ni sifa za kijinga nia kuwaumiza hao so called wabaya wake full uswahili.
Kuhusu sembe watu wanamvutia waya tu, Jack Patrick ilikuwa hivyohivyo. Kuna watu wamejitolea kuchoma waharibu vijana kwa madawa.
 
Izo ni ofisi za timesfm watanzania mnanini nyinyi aaaaahaaaaa ana gari moja tu verosa kweli shigongo anajua kuchota akili za watu ..i knw here anapanga mwananyamala hana zaidi

bora umesema ndugu yangu. Watu wanakurupuka tuuu....muwe makini na magazeti ya Shigongo..kah...!
 
Inawezekana ni vyake Dida namjua ni mjasiriamali uwa anaenda china kufata mzigo na nyie muende china trip moja tu inabadilisha maisha yako

Anafungaga mzigo China?
Mzigo gani?
Trip moja China unabadilika kimaisha??
Trip ya kubeba kupeleka au kuchukua nini??
 
kwenye the mboni show alisema

ana maduka ya nguo

ni mtangazaji

anafanya biasha ya madini

ana biashara zake zingine
 
Leo Ofisi za times FM na magari ya wafanyakazi vimekuwa mali ya dida...Binadamu kwanini tunapenda kudanganyana? Kesho nae Bdozen atapiga picha Clouds na mjengo yao na gari la bosi na kusema ni vya kwake na watu wataamini. Aise ni shida sana Wadanganyika:A S confused:
 
hakuna cha mzigo China wala nini, wengi wetu tunasiri nzito sana juu ya mafanikio katika maisha na kamwe hatuko tayari ijulikane kirahisi.

kistaarabu wacha niseme ni mjasiriamali na sitaki kugusia zaidi. Hongera zake :wink2:
 
pambee tu huyu bibi kinachompa jeuri kwanza ana saloon zipatazo 8 bado ana maduka,ya jumla zaidi ya 17 mjini hapa ndo maana yupo juu
 
Huyu asitudanganye. Hebu aweke hati ya hiyo nyumba tuione!
 
huyu ni mjasiriamali mwenye akiri sana ana duka la nguo lkn mjnja sana UAMINIFU na KUJITUMA ndo kumemfikisha hapo alipo
katajilikaa kupiiia hivi
kuna wale weny maduka madogo wenye msingi mdogo eiza hawawezi kwenda china au awajui machimbo ya china yapo vipi au mishe zinaendaje hasa wa mikoani
anachofanya pengne unampa ml 5 umnunulie mzigo amba km ukisema uende kununua kkoo cost yake ni zaidi ya ml 8 sasa yeye ule mzigo anaweza pata kwa ml 3 mpk 4 mpk kukufikia araf alivyo mjanja kuwateka wateja yeye anakusafilishia mpk mlangoni popote tanzania na mari ya uhakika sasa utakuta wewe mzigo wa ml 5 unaingiza mpk ml10 wakati ukisema ununue kkoo lbda utapata faida ml 2 au uuze bei juu

sasa jenga picha akichukua oda za watu 10 tufanye kila mmoja anapata faida kwa lk 8 unafikili ana sh ngap ?
usione wale wadada anaowalusha ktk kipindi chake wale ndo wateja zake wakubwa na ana watu wengi
siyo mbeba NGADA km mnavyokalilishwa
ni mpiganaji na anajua kutumia fulsa
 
Mhhhh!! Napata Shaka Kuamini Hizo Zoote Ni Mali Zake Dida!!! Kama Ni Kweli, Basi Inatia Shaka!! Kama Yule Jamaa Anayemiliki Magari Na Majengo Ya Kifahari, Yaliokutwa Magomeni!! Alikuwa Anatiliwa Shaka, Iweje Yeye Iwe Poa!!!!!??
 
Back
Top Bottom