Dida Shaibu wa Wasafi FM kama Mwijaku. Upeo wao ni mdogo sana

Dida Shaibu wa Wasafi FM kama Mwijaku. Upeo wao ni mdogo sana

Ni aibu sana kuwasikiliza. Siku hizi wasikilizaji wanauelewa mkubwa kuliko watangazaji.
 
Hii Jinsi gani inaonesha watangazaji wetu wanna upeo mdogo.

Katika kipindi cha Mashamsham ya Pwani cha Wasafi FM, Didas akiwa Arusha alipigiwa simu na mtangazaji mwenzake na kumuuliza mlima Kilimanjaro unapatikana mkoa gani, akajibu Moshi.

Hapa Kuna tatizo kubwa kwa watangazaji wetu katika upeo wa kujua mambo muhimu.

Ajabu hata mtangazaji aliyeuliza swali hakuona kosa hilo.
Na ndio wako connected na wenye nchi. Nchi hii kusoma sana na kujua mengi hakuna faida.
Ukiwa na mdomo na guts za kujitoa ufahamu unakula maisha kuliko watu na avidgrii vyao
 
Nilimsikia mtangazaji wa Radio Bongo anaongea wakati yuko hewani," Wenzetu wazungu wakienda chooni wakishamaliza, lazima wageuke kwanza kuangalia kama kuna tatizo lolote kiafya".
Mi nikajiuliza mara mbili hivi kuna watu huko wamekaa kumsikiliza Boyaboya kama huyu na kipindi chake kila siku?
 
Kuna siku babra wa clouds alikuwa anajadiliana na wenzie kuhusu ukienda kuoga huwa unakojoa pia.
 
Wewe ukishaweza kupiga makelele tu nchi hii baaasi umeshamaliza kila kituu...kwenye utangazaji, uigizaji, siasa, uchambuzi, uchawa we unapeta tuu.
 
Hizi redio inabidi wizara husika iingilie kati kuweka regulations maana huku tunakoenda tunatengeneza kizazi chenye uelewa mdogo

Maana unakuta watangazaji wanajadili mambo ya kitaalam kabisa bila kuwa na utaalam huo.

Yafaa kama mjadala unahusu jambo la kitaalam aitwe mtaalam kulitolea ufafanuzi na sio mtu kuongea na kupotosha jamii.
 
Bongo wenye pesa wengi ni mabasha, ndio sababu ukichunguza Bongo watu smart kichwani ndio wanaotaabika na maisha na hawatoki, lakini hii mibwabwa inabadiri magari tu.
Hahaha

Ova
 
Hizi redio inabidi wizara husika iingilie kati kuweka regulations maana huku tunakoenda tunatengeneza kizazi chenye uelewa mdogo

Maana unakuta watangazaji wanajadili mambo ya kitaalam kabisa bila kuwa na utaalam huo.

Yafaa kama mjadala unahusu jambo la kitaalam aitwe mtaalam kulitolea ufafanuzi na sio mtu kuongea na kupotosha jamii.
We huoni kuna mpaka watangazaji wanaitwa bungeni
Ina maana wanaonekana wanakubalika

Ova
 
We huoni kuna mpaka watangazaji wanaitwa bungeni
Ina maana wanaonekana wanakubalika

Ova
Kuonekana unakubalika haimaanishi kuwa unachokifanya ni sahihi.

Wapo watu wengi tu wanaofanya ujinga na bado wameitwa bungeni.

Reffer to yule mlevi aliyepewa mpaka tiketi ya ndege kwenda kuishangilia Taifa Stars.

Ndio utajua jamii yetu imejaa watu wa aina gani.
 
Wewe ukishaweza kupiga makelele tu nchi hii baaasi umeshamaliza kila kituu...kwenye utangazaji, uigizaji, siasa, uchambuzi, uchawa we unapeta tuu.
Mkuu hii comment yako![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Watanzania tuna matatizo sana! Yaani wote mlokoment mmeshindwa kujua kama moshi kuna mlima kilimanjaro?

Kama haupo moshi uko wapi sasa?
 
Back
Top Bottom