Didier Deschamps kwanini umemuacha Anthony Martial?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Nimeangalia kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kilichoitwa kwa ajili ya world cup, binafsi sijaridhishwa na maamuzi kadhaa yaliyofanywa na Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps.

Kwanza, hajamuita Winga hatari na mwenye kasi Anthony Martial. Wote ni mashahidi hakuna ambaye hajui uwezo wa Martial katika wing ya kushoto ambaye ana mabao 21 na assist 13 katika michunao yote msimu huu. Kocha amemuita Thomas Lemar ambaye hakuwa na msimu mzuri kikosini Monaco.

Pili, amemuacha Kurzawa ambaye ni full back wa kushoto wa PSG akaja kumuita Ben Mendy ambaye ndio kwanza ametoka majeruhi ya muda mrefu. Hapa amefanya gambling.

Tatu, sijajua ni kwanini amemuacha fundi wa mpira Adrien Rabiot na kujaza watumia nguvu kama akina Matuidi na Kante.
Lacazette nae hajajumuishwa sijui ni kwanini, badala yake ameitwa Super Olivier Giroud.

Nimalizie tu, japo Anthony Martial hakupata muda wa kutosha klabuni chini Jose Mourinho, ila namba hazidanganyi kwa dakika chache alizocheza amefunga magoli mengi na kutengeneza assist za kutosha, Martial alistahili kuitwa timu ya Taifa, kwakuwa hao walioitwa sioni wa kumuweka benchi.

 
hawa wachezaji wa kiafrika waliokataa uraia wa nchi zao ,goja wakatwe tu mfano. colman, na martial na wengine mafalafala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…