Didier Deschamps kwanini umemuacha Anthony Martial?

Didier Deschamps kwanini umemuacha Anthony Martial?

Lacazette ameanza kuitwa 2013 ila mpaka sasa ana goli 3 tu.
Lacazette apewe muda wa kutosha. Halafu pia wachezaji walioachwa kama Rabiot,Toliso,Martial,Kurzawa,Coman, NK.ni wa kuangaliwa sana ni kizazi cha thamani hichi.
Nategemea ZIDANE kuirithi mikoba ya Deschamps baadaye.
 
Sawa Giroud ana rekodi nzuri kuliko wenzie. Kama asipopewa mipira ya vichwa hatutalala njaa?
Foward au Striker anayefunga kwa miguu pamoja na kichwa ndiyo chaguo sahihi.
Tunahitaji plan B,
Hao ambao wanafunga kwa miguu yote mbona hawajamzidi magoli??? Njoo na takwimu acha maneno makavu, wenzetu wanacheki takwimu za mchezaji na sio mboyoyo
 
Lacazette apewe muda wa kutosha. Halafu pia wachezaji walioachwa kama Rabiot,Toliso,Martial,Kurzawa,Coman, NK.ni wa kuangaliwa sana ni kizazi cha thamani hichi.
Nategemea ZIDANE kuirithi mikoba ya Deschamps baadaye.
Tolisso yupi unayesema hajaitwa????
Uliowataja wapo reserve na sio kweli kwamba wameachwa. Wachezaji wana damu na nyama lolote linaweza kujitokeza. Kwa nchi kama Ufaransa yenye vipaji vingi kupata hata nafasi ya kuitwa reserve team ni heshima.
Tunaenda kwenye mashindano na sio mechi za majaribio. Waliokosa nafasi sasa watapata kipindi kijacho maana wooote wana umri mdogo tu.
 
kwenye klabu yake anawekwa benchi na lingaard..

je, tumuamini yeye tuache anaogombania nao namba kina mmbape,dembele na vijana wengine wamoto
 
Sasa mkuu kama hicho ndo kigezo, vipi kwa mabeki maana ukiangalia Mendy alikua nje muda mrefu sana karudi juzi juzi tu lakini kaitwa, what's so special about him?
Na mimi naomba unijibu mbona neymar kaitwa licha ya kuwa nje kwa miezi kibao???


Halafu nakuuliza tena kwanini Manuel Neur Kipa wa Bayern Munich ameitwa team ya taifa licha ya kuwa nje kwa takribani mwaka mzima , hapo unasemaje ???.... Jibu ni fupi takwimu zao za awali zinawabeba. Nitajie mchezaji ambae unadhani angeitwa badala ya mendy
 
Desclipne kaipa kipaombele..

Yasije kutokea yale ya fainal za south
 
M
Nimeangalia kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kilichoitwa kwa ajili ya world cup, binafsi sijaridhishwa na maamuzi kadhaa yaliyofanywa na Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps.

Kwanza, hajamuita Winga hatari na mwenye kasi Anthony Martial. Wote ni mashahidi hakuna ambaye hajui uwezo wa Martial katika wing ya kushoto ambaye ana mabao 21 na assist 13 katika michunao yote msimu huu. Kocha amemuita Thomas Lemar ambaye hakuwa na msimu mzuri kikosini Monaco.

Pili, amemuacha Kurzawa ambaye ni full back wa kushoto wa PSG akaja kumuita Ben Mendy ambaye ndio kwanza ametoka majeruhi ya muda mrefu. Hapa amefanya gambling.

Tatu, sijajua ni kwanini amemuacha fundi wa mpira Adrien Rabiot na kujaza watumia nguvu kama akina Matuidi na Kante.
Lacazette nae hajajumuishwa sijui ni kwanini, badala yake ameitwa Super Olivier Giroud.

Nimalizie tu, japo Anthony Martial hakupata muda wa kutosha klabuni chini Jose Mourinho, ila namba hazidanganyi kwa dakika chache alizocheza amefunga magoli mengi na kutengeneza assist za kutosha, Martial alistahili kuitwa timu ya Taifa, kwakuwa hao walioitwa sioni wa kumuweka benchi.

View attachment 780561
Mourinho kasababisha yote hayo kwa kumnyima fundi martial muda Wa kutosha .. France wameacha mafundi kibao
Martial
Zouma
Yedder
Payet
Rabiot
Costril
 
M

Mourinho kasababisha yote hayo kwa kumnyima fundi martial muda Wa kutosha .. France wameacha mafundi kibao
Martial
Zouma
Yedder
Payet
Rabiot
Costril
kila kitu analaumiwa mourinho, martial badala ya ku concentrate kwenye mpira akili yake yote kaihamishia kwa mke wake, anastahili anayoyapitia.
 
Back
Top Bottom