Dilemma ya January, na watu wa Tanga

Dilemma ya January, na watu wa Tanga

Chuki ya January dhidi ya wakristo itamtafuna sana
 
Je watu wanapenda sera gani za kiuchumi zifanyike kule Tanga?
 
Je watu wanapenda sera gani za kiuchumi zifanyike kule Tanga?
Unahangaika kama kuku anayetaka kutaga vile, mara January, mara ukabila,mara udini,mara tusidiscus watu, tatizo nini? A certified idiot, that's what you are.
 
Mimi simfahamu January. Ila naona bado hajakomaa kuwa kiongozi mzuri. Na bado hatumjui the real January.

Halafu anaonekana kidoogo kama ni mtu artificial na anaependa uelite.

January ana reflect dilemma ya watu wa Tanga na udhaifu wao kwenye siasa za CCM Tanzania.

Makabila ya pwani yenye nguvu ndani ya CCM ni watu wa mkoa wa Dar, mkoa wa Pwani, Unguja, na hawa wanashirikiana na watu wa kanda ya ziwa ambao some times ni ndugu zao kutokana na migrations za biashara ya utumwa.

Watu wa Tanga kama wasambaa wana undugu wa mbaaali na wachagga na wapare. Ingawa wasambaa hawapendi hii connection, kwasababu haiwasaidii kisiasa ndani ya CCM. Wapemba wa asili ambao sio washirazi au waarabu wana undugu wa mbaali na watu wa Tanga. Watu watanga pia wana undugu wa mbaaali na watu wa Mombasa.

Watu wa pwani wa mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara na Pemba wana ushawishi mdogo ndani ya CCM. Wanaweza kupata vyeo, lakini wana ushawishi mdogo.

Halafu makabila mengine ya pwani yana dhani kwamba watu wa Tanga wana majivuno. Kwa sababu labda watu wa Tanga in general wana sura nzuri kuliko watu wengine wa pwani.

So mtu wa Tanga kuwa rais wa CCM bado ni ngumu.

Solution ni watu wa Tanga kujikubali, na kutokujionea aibu. Na kuwa a politically independent block ndani ya CCM with equal power na hayo makabila mengine ya pwani.

Njia moja wapo ni kujitegemea kiuchumi. Hayo mashamba makubwa ya mkonge yazalishe pia mazao ya chakula kama sunflower, mahindi na maharagwe. Hii ni muhimu sana sana.

Halafu sehemu ndogo ya hayo mashamba makubwa irudishwe kwa wenyeji wa Tanga kwa usawa (na sio baadhi ya wazawa wapate mashamba makubwa huku wengine wakipata mashamba madogo).

Watu wa Tanga waboreshe elimu ya msingi na sekondari mpaka form 6 pamoja na VETA. Wawe pia na utamaduni wa kufanya biashara (halali na nzuri). Wawekeze pia kwenye utalii na viwanda. Wawe na tabia nzuri za kimaadili na wawe na ujirani mwema.

Mipaka ya miji ya Korogwe na Tanga mjini iongezwe.



ANGALIZO

Lengo la huu uzi ni kumuonea huruma January pamoja na watu wa Tanga. Na pia kumshauri January akomae zaidi na aimprove zaidi, na arekebishe mapungufu yake. Na pia ajue hali halisi ya kisiri siri ya siasa za Tanzania.

Uzi huu hauna lengo la kupromote migawanyiko ya aina yeyote kwenye jamii.
Sawa Bashite eeh
 
Mama yake January Mkristo
Ni kweli. Nimesoma mahali kwamba mama yake ana undugu na Cardinal wa zamani aliyekuwa anaitwa Laurean Rugambwa.

Mojawapo ya vyuo vikuu viwili alivosoma January (kule Marekani) kina milikiwa na shirika la kanisa katoliki.

Inavyo onekana saa100 atakuwa rais mpaka 2030. Baada ya hapo atapokelewa na mkristo.
 
Back
Top Bottom