Dili la Ulaya sababu za Kibu Denis Kutoonekana kambini

Dili la Ulaya sababu za Kibu Denis Kutoonekana kambini

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Mchezaji superstar na tegemezi wa timu ya simba Kibu denis, yupo nje ya nchi kukamilisha mazungumzo na klabu yake mpya ya ubeligiji inayocheza ligi daraja la pili, mchezaji huyo alisaini dili jipya na klabu ya simba huku akipewa gari, na pesa zote alizostaili kulipwa, na msimu ulivyoisha alikwenda mapumzikoni huko nchini Marekani ambapo ndo familia yake ipo.

Kutokana na ukubwa wa dili alilopata Kibu Denis Ulaya, imemuwia vigumu kukataa dili hiyo hivyo amekuwa hapatikani hata kwenye mtandao wa simu yake, kwani namba anayotumia sasa hivi ni mpya na anawasiliana na watu wachache sana hapa Tanzania, Kibu Denis atarudi nchini ili kumalizana na Simba kwa maana ya kukamilisha mauzo yake kutoka simba kwenda huko Ulaya, hivyo Simba watapata pesa nyingi sana kupitia mauzo ya Kibu Denis.
 
Mimi nawashangaa viongozi wangu wa Simba kuhangaika na huyu Kibu Denis, kwa kweli sijaona mchango wake kwa Simba msimu uliopita, amewasumbua kumuongezea mkataba na hadi sasa wanasumbuka naye, hana ukubwa huo anaofikiri anao.
Usimchukulie poa, kumbuka katika magoli yote ya Simba msimu uliopita, goli moja alifunga yeye.
 
Munataka mutengeneze mazingira ya kuonekana Mumemuuza Kibu, ilhali jamaa kazamia marekani.
Kibu ni baaria mwenzetu, wale tulioishi Port Elizabeth mutakua mushanisoma.
 
Munataka mutengeneze mazingira ya kuonekana Mumemuuza Kibu, ilhali jamaa kazamia marekani.
Kibu ni baaria mwenzetu, wale tulioishi Port Elizabeth mutakua mushanisoma.
Jamaa inaonyesha alipiga mahesabu yake, apate pesa ya kutosha ya usajili atokomee mazima. Labda kama ana nia ya kuacha mpira ila nadhani hata huko Marekani hataweza kucheza mpaka arudishe pesa za Simba, na pia Simba wakitaka kumfanyia undava wanaweza kumdai hata faini kubwa ambayo hataweza kulipa.

Nafikiri huyu tumtumie kama mfano ili hali hii isije kujirudia siku za mbele. Mauzauza yalizidi sana Simba asee.
 
Mchezaji superstar na tegemezi wa timu ya simba Kibu denis, yupo nje ya nchi kukamilisha mazungumzo na klabu yake mpya ya ubeligiji inayocheza ligi daraja la pili, mchezaji huyo alisaini dili jipya na klabu ya simba huku akipewa gari, na pesa zote alizostaili kulipwa, na msimu ulivyoisha alikwenda mapumzikoni huko nchini marekani ambapo ndo familia yake ipo.

Kutokana na ukubwa wa dili alilopata kibu denis ulaya , imemuwia vigumu kukataa dili hiyo hivyo amekuwa hapatikani hata kwenye mtandao wa simu yake, kwani namba anayotumia sasa hivi ni mpya na anawasiliana na watu wachache sana hapa Tanzania, kibu denis atarudi nchini ili kumalizana na simba kwa maana ya kukamilisha mauzo yake kutoka simba kwenda huko ulaya, hivyo simba watapata pesa nyingi sana kupitia mauzo ya kibu denis
Watu wajinga ndio mnamkweza huyo Kibu Denis.
 
Jamaa inaonyesha alipiga mahesabu yake, apate pesa ya kutosha ya usajili atokomee mazima. Labda kama ana nia ya kuacha mpira ila nadhani hata huko Marekani hataweza kucheza mpaka arudishe pesa za Simba, na pia Simba wakitaka kumfanyia undava wanaweza kumdai hata faini kubwa ambayo hataweza kulipa.

Nafikiri huyu tumtumie kama mfano ili hali hii isije kujirudia siku za mbele. Mauzauza yalizidi sana Simba asee.
Zile nguvu za kumtetea Feisali zihamie kwa Kibu
 
Back
Top Bottom