Dili za Mtandaoni/Online deals(special threads)

Duh! Kama ndivyo mbona Upwork wanalima sana, manake $40 inaishia njiani, kabla benki nao hawajachukua chao!
Hiyo ni commision yao hata freelancer wanalima 10% ya mapato yako, na hapo sikuwa naongelea fees, hizo siyo pesa wanazolima freelancer naongelea bank transfer fees wanakula bank zinazokuwa involved siyo wao.
 
Ila up work naona ni pagumu sana kupata kazi
Milolongo ni mingi sana
Upwork imeelemewa na Freelancers, matokeo yake kuna baadhi ya kazi, ujira badala ya kupanda ndo kwanza inapungua! Yaani unakuta Client aliyekuwa analipa $7/hour mwaka 2015, kwa kazi ile ile mwaka 2020 unakuta analipa $3/hour, na bado wapo Freelancer walio willing kufanya hata kwa $2/hour.

Sasa ili kupunguza wimbi la Freelancers, ndo unakuta hivi sasa hata account kuwa approved, ni mbinde kweli kweli let alone mambo ya kuuziana Connects/Tokens ambazo zamani unapewa Free 60 Connects per month; zikikuishia ndipo ungeweza kununua au kusubiri mzunguko unaofuata! But now, hupewi hata connect 1; sasa kwa New Comers sijui wanafanyaje!
 
Hiyo ni commision yao hata freelancer wanalima 10% ya mapato yako, na hapo sikuwa naongelea fees, hizo siyo pesa wanazolima freelancer naongelea bank transfer fees wanakula bank zinazokuwa involved siyo wao.
Na hiyo $40 niliyoitaja sio Upwork Fee bali ni Wire Transfer Fee! Upwork Fee na yenyewe ni full maumivu, manake wanatungua 20% hadi unapofikisha $500 ndipo fee inashuka kutoka 20% to 10%.
 
Ni pagumu sana Mkuu nikipata hata kazi moja upwork itakuwa ni bahati kubwa sana
 
Bado nimekamilisha leo kujiunga,nasubiri baada ya masaa 24
Kwa sasa mtihani ndo uko hapo kwenye approve, tofauiti na zamani. Ikishakuwa approved, unaweza kupitia hii post labda unaweza kuokota kitu:
 
Kwa sasa mtihani ndo uko hapo kwenye approve, tofauiti na zamani. Ikishakuwa approved, unaweza kupitia hii post labda unaweza kuokota kitu:
Nashukuru sana mkuu ngoja niipitie kwa makini
 
Na hiyo $40 niliyoitaja sio Upwork Fee bali ni Wire Transfer Fee! Upwork Fee na yenyewe ni full maumivu, manake wanatungua 20% hadi unapofikisha $500 ndipo fee inashuka kutoka 20% to 10%.
Upwork yah wanakata that much, ila mimi transfer natumia payoneer so wanakata $1 na payoneer wanaka 2$ coz nimeset instant transfer
 
Kwa sasa mtihani ndo uko hapo kwenye approve, tofauiti na zamani. Ikishakuwa approved, unaweza kupitia hii post labda unaweza kuokota kitu:
Nimeanza kuelewa maana ya connect
Niliona kuna kazi zingine zinahitaji connect nne zingine zinahitaji connect sita n.k

Ina mana hakuna hata kazi moja ambayo haimuhitaji mtu kuwa na connects ili aweze kuapply mkuu. Bora nirudi freelancer.com huu mchezo wa kuuziwa connect na uhakika wenyewe wa kupata kazi sio asilimia mia unanifikirisha sana
 
Upwork yah wanakata that much, ila mimi transfer natumia payoneer so wanakata $1 na payoneer wanaka 2$ coz nimeset instant transfer
Natumia zote mbili kutegemeana na amount.Payoneer ni mzuri sana kwa amount chini ya $1000 lakini ikianzia $1000 na kuendelea, kimahesabu payoneer inakuwa expensive kwa sababu ni transactions 6 hizo.
 
Hakuna kazi unayoweza ku-apply bila connect. Sijaingia Freelancer.com muda mrefu kidogo lakini kama utaratibu wao ndio ule ule wa zamani, binafsi sioni tofauti kubwakati ya Upwork wanaouza Connect na Freelancer ambao hawauzi. Kumbuka Freelancer.com application zinajipanga kutokana na 1. Reputation ya Applicants 2. Paid Application. Maana yake ni kwamba, kama kazi imetangazwa sasa na wewe New Comer ukaanza ku-apply, Application yako itakuwa juu kabisa! Akija new applicant, hata kama hana Star hata moja lakini ana muda mrefu Freelancer.com kuliko wewe, hapo atakaa juu yako na wewe utakuwa chini yake! Kama applicant wa 3 ana Star 1, atawashusha wote wawili na yeye atakuwa juu, wewe new comer application yako itakuwa ya 3. The process goes on!

Sasa assume kuna 50 applicants, na wote hao wamekuzidi reputation in terms of Stars na Ukongwe! Hapo application yako itakuwa down to 50th position. Now ask yourself. Ni Client gani atakayeacha applications ya kwanza hadi ya 49 aje kuichukua yako ya 50?! Sisemi haiwezekani lakini chance ya Client kuziacha application za juu kuifuata ya kwako iliyo chini ni ndogo sana! Na hapo usisahau application zinazokuwa juu zinakuwa ni zile zenye Top Ratings.

Sasa ukiona mbona application yako ipo chini sana wakati ungetemani iwe juu juu ili hatimae Client aweze kuiona kwa wepesi; utakachofanya hapo utatakiwa ulipie ili ipandishwe juu! Na hapa usisahau, wakati wewe New Comer unalipia ili application yako iwe juu, mwenzako mwenye Star 1 nae analipia ili nae application yake iwe juu! Mwenye Star 2 nae analipia ili application yake ipandishwe juu! Sasa kama nyote mmelipa amount sawa; hapa tena applcation ya mwenye Star 2 itakuwa juu ya yule mwenye Star 1 ndipo itafuta ya kwako! Na hapo sio kwamba labda mtapanda hadi nafasi 3 za juu kabisa, HAPANA kwa sababu there's no way mnaweza kuzishusha zile zenye Reputation kubwa zaidi ambazo hata kama walichelewa ku-apply, application zao zitapanda juu na kuonekana kirahisi zaidi na Client! Unachoweza kupata hapo labda application yako kupanda hadi position #10 Depending na Top Ranking Freelancers wangapi wame-apply!

Upwork ujinga huo haupo. Ukiwahi wa kwanza kutuma application basi application yako itaendelea kuwa #1 hata kama kuna Top Rated Freelancers 100, each with 100% Rating, hawa wote watakuwa chini yako! Na asikudanganye mtu, ina-matter sana application yako kuwa juu! Binafsi ingawaje Rating ni 100%, siwezi ku-apply kazi ambayo naona tayari kuna, say 20 Applicants kwa sababu pamoja na kuwa Top Rated, bado application yangu itakuwa #21. Na kama Client anatafuta mtu mmoja tu, basi chance yako hapo ni ndogo sana!!

Na pia usisahau! Pale Freelancer kulikuwa na ujinga wa kulipia test ili kuongeza chance! Kuna Clients wengine unakuta wanaweka wazi kwamba applicants awe amefanya, say, American English so and so! Ili kufanya hiyo test, ni lazima ulipie! Hapa tena, UPwork hawana huo ujinga.

So, kama Freelancer.com bado hawajaacha huo mchezo wa kulipia nafasi ya juu, na wale wenye Reputation Kubwa Zaidi automatically applicationzao kuwa juu hata kama wamechelewa ku-apply; basi ni afadhali ya Upwork ambako unalipia Connect unless kama una skills ambazo majority hawana! Kwa mfano, kama wewe ni Nuclear Scientist, I guess hapo Freelancer hapawezi kuwa na Nuclear Scientists wengi! Kwahiyo ikitokea opportunity kama hiyo, si ajabu total number of applicants mkawa watatu tu!!!!
 
Aisee haya mambo haya
Sasa connect moja huko upwork inaweza ikacost kiasi gani
Fever nao vipi hawana huo unyanyasaji kama freelancer?
 
Natumia zote mbili kutegemeana na amount.Payoneer ni mzuri sana kwa amount chini ya $1000 lakini ikianzia $1000 na kuendelea, kimahesabu payoneer inakuwa expensive kwa sababu ni transactions 6 hizo.
Ofcourse payooneer ni expensive nikiwithdraw milion moja nakatwa zaidi ya laki na ishirini halafu pale kwenye atm naambiwa kila withdraw nitakatwa 11000 payoneer charges $3, na milion moja lazima udraw mara 3 maana maximum ni lak 4 kwa withdraw moja lakini ajabu wanakata ela ndefu sana sema ndiyo hivyo ni quickest way kama nataka kufanya transfer.
 
Aisee haya mambo haya
Sasa connect moja huko upwork inaweza ikacost kiasi gani
Fever nao vipi hawana huo unyanyasaji kama freelancer?
Sijawahi kufanya kazi Fivver. I think I was lucky with Upwork enzi hizo inaitwa oDesk! Baada ya kujiunga tu, ilinichukua chini ya wiki moja kupata kazi yangu ya kwanza; na ndani ya mwezi mmoja nikawa nazikataa kazi! Matokoe yake, sikuwa tena na sababu ya kurandaranda huku na huko, ingawaje hivi sasa it's a matter of time kabla sijaanza kurandaranda manake mambo magumu ile mbaya!

Kuhusu bei ya Connects, wanaanza kuuza 10 Connects kwa $1.5; na unaweza kununua nyingi zaidi kwa staili hiyo hiyo; 20 kwa $3, 30 kwa $4.5 and so on up to 60 Connects for $12. Kumbuka, hizo 10 Connects unaweza kuzitumia to a maximum of 5 Jobs and minimum 2 Jobs. Ukichukua maelezo yangu ya awali kuhusu Freelancer.com kuuza nafasi za juu, hiyo $1.5 inakuwezesha kununua nafasi ya juu kwa Application moja tu, na hakuna guarantee kwamba itakuwa kwenye #1. Kinyume chake, hiyo $1.5 uliyonunua 10 Connects; na kama uta-apply small jobs ambazo nimesema maximum ni 5 Jobs; kama ulikuwa fasta ku-apply, then una guarantee ya zote 5 kuwa #1 in the list or at least kuwa kwenye Top 5 ambayo na yenyewe ni mzuri sana!
 
Dah aiseee
Yani kazi inawindwa kama sungura[emoji1] [emoji1] ukichelewa kidogo tu tayari wameshakutoa kwenye reli

Hivi hapa bongo hamna site kama hizo mkuu mana dah wenzetu huko wamechachamaa kweli kweli kwenye hizi fursa
 
Of course ni expensiv but all in all, kwa 1M bado ni cheap kutumia Payoneer kulinganisha na Wire Transfer kwa sababu haiwezi kufika hiyo 120K. Mfano mzuri, saa chache tu zilizopita nimefanya transaction tatu NMB ambazo ni 1.2M; ambayo ni almost USD 560. Sasa hiyo USD 560 ukitumia wire transfer, say to CRDB, itakayofika kwenye akaunti yako ni 560-45 = $515. Sasa kama itakayofika ni $515, kupata 1.2M ambayo unaweza kuipata kwa Payooner ukitumia mashine za NMB, ina maana rate iwe 1,200,000/515 = TSh. 2330. Huwezi kupata rate kama hiyo kwa non-cash (in fact hata kama ni cash), tena kwa kuuza. Kwa maana nyingine, ukituma USD560 kwa wire transfer, itakayoingia kwenye akaunti ni less than 1.2M. Kwa rate za NMB za leo, hiyo 1M ni kama USD466.5; ukitumia Wire Transfer, itafika USD421.5. Sasa kwa USD 421.5 utaweza kupata 1M only if Selling Rate ni TZS 2372.5 jambo ambalo halipo!!!
 
Dah aiseee
Yani kazi inawindwa kama sungura[emoji1] [emoji1] ukichelewa kidogo tu tayari wameshakutoa kwenye reli

Hivi hapa bongo hamna site kama hizo mkuu mana dah wenzetu huko wamechachamaa kweli kweli kwenye hizi fursa
Kibongo bongo sijawahi kusikia but keep trying, itafika siku utapata tu!! Muhimu ni kuzingatia huku duniani watu wanatafuta kazi kwa mwaka mzima na hawapati lakini wanaendelea kutuma maombi badala ya kukata tamaa. Problem la online jobs, watu huwa wanakata tamaa mapema huku wakisahau online jobs na kwenye traditional jobs kote kunahitaji uvumilivu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…