Sina hakika kama nimekuelewa lakini acha nijibu tu hivyo hivyo!! Mosi, kazi huwa zinakuja randomly; zinazoendana na skills zako na hata zisizoendana na skills zako! ITo stop it, unatakiwa ku-filter. Kwenye SEARCH section ya home page yako, utaona wameandika FIND WORK....... search for jobs:-
View attachment 1357641
Sasa hapo walipoandika Search for jobs, utaandika KEY WORD ya moja ya kazi unazotarajia kuzifanya, kwa mfano
Web Development. Ukishaandika, uta-click hiyo search icon. Ukisha-click search, zitatokea kazi mbalimbali related to Web Development. Ziangalie kwa haraka haraka kujiridhisha kama zinafanana fanana na unachotafuta, ukiona zinafana fanana, achana nazo na badala yake click SAVE SEARCH.
View attachment 1357649
Baada ya ku-click SAVE SEARCH, repeat above process kwa kuandika Keyword ya kazi zingine unazoona unaweza kuzifanya; kwa mfano GRAPHIC DESIGN.
Repeat and repeat hadi utakapoona zile unazoweza kufanya umezi-search ku-save. Ukishamaliza hapo, maana yake ni kwamba kwenye page yako zitakuwa zinatokea zile kazi ambazo zipo related na ulizo-search kabla na ku-save. Haziwezi kutokea, mathalani kazi za Legal Practice wakati hakuna keyword ambayo uli-search na ku-save related na masuala ya sheria.
Aidha, sijui kwa New Comers siku hizi inakuwaje lakini sie wengine CONNECTS (token zinazokuwezesha kuomba kazi) tunanunua! Kwa mfano, Connects (Token) 60 unanunua kwa $9. Hizi Connects 60 unaweza kutumia ku-apply a minimum of 10 Jobs, and 30 jobs Maximum.
Hiyo maana yake ni kwamba, unatakiwa kuwa makini unapo-apply kazi yoyote cos' you don't want to waste your paid Connects for anything. Lakini hata kama umepewa Connects za bure probably kwa sababu hujawahi kuingiza pesa, still you don't want to waste them uselessly kwa sababu no matter what, lazima hizo Free Connects utapewa in limited amount, say 60 per months.
Sasa basi, kwa kuangalia screenshot ya hapo juu, Post #19, hiyo kazi ya kwanza iliyoanza na "Hello. I'm an entreprenuer who...."
Think twice kabla huja-apply hiyo kazi na kuhatarisha Connects zako kwa sababu huyo Client hayupo VERIFIED
View attachment 1357659
Clients wa aina hiyo wapo wanaokuwa serious kutafuta Freelancer lakini bado hajafahamu sawasawa, na kwahiyo ukimwelekeza anaweza kumalizia usajiri na kuwa verified, lakini pia kuna wengine ambao hawapo serious! Ni kwamba anajisajiri, ana-post kazi na baada ya hapo harudi tena bila kujua kwamba ku-apply hiyo kazi watu wanatumia pesa!
Vile vile kazi kama hizi hapa chini unatakiwa kuwa makini kabla huja-apply na kuhatarisha Connects zako!!
View attachment 1357661
Kazi ya kwanza hapo juu utaona kuna Proposals 50+; yaani walio-apply ni zaidi ya 50 wakati nafasi zenyewe ni 3 tu! Hiyo maana yake ni kwamba, wewe uki-apply unaweza kuwa labda Applicant wa 55 !!! The question is: Kwanini huyo Client/Employer apitie application ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne na kuendelea hadi anaifikia ya 55 ambayo ni ya 55?!! Hakuna atakayefanya huo ujinga! Atakachofanya atapitia application ya kwanza, akiona ana-qualify atampa Interview Offer. Atachukua inayofuata na zingine zinazofuata, or probably randomly na akipata idadi anayotaka, zingine hata ukifungua HATAFUNGUA!!!!!
The same kwa kazi ya pili ambayo kuna Proposals 20-50; which means hapo uki-apply utakuwa somewhere above mtu wa 20! Na kwa kazi kama Data Entry, unaweza kukuta wakati wewe una-apply kuna wengine 25 wana-apply at the same time. Which means, kama hauna speed, hadi una-click SUBMIT, unakuta application yako ipo kwenye 50+ wakati ilikuwa 20-50!!!!
Rule of Thumb ni kwamba, kwa kazi ambayo una-qualify basi chance ya kupata Interview inakuwa kubwa zaidi kama application yako inatokea juu juu; among the top 10, lakini inakuwa njema zaidi kama inakuwa among top 5 unless kama nafasi yenyewe inataka Freelancer zaidi ya mmoja!!!
Kwa maana nyingine, especially kwa hizi kazi zinazoonekana kila mmoja anaweza kufanya, basi make sure unakuwa faster kwenye ku-apply! Kwa kazi kama Data Entry, unaweza kuiotea ikiwa ndo kwanza imekuwa posted; maybe posted 3 minutes ago, but trust me, usipokuwa na speed, unaweza kukuta umetumia dakika 2 tu ku-apply lakini application yako inakuwa ya 30!!!
WHAT TO DO?! Unatakiwa kuandaa Template ya Application Letter Template kwa kazi mbalimbali, kwa mfano, template letter kwa Swahili-English-Swahili Translation, Graphic Design template letter, Web Design Template Letter and so on based on your skills!!
BUT,
BE CAREFUL! Clients/Employers wengi kama sio wote wanapiga VITA SANA huo mtindo ambao unaitwa Generic Letters!!! Wanapiga vita kwa sababu Freelancers katika harakati za kuhakikisha applications zao zinakuwa juu, wengi huwa wana-copy tu template letters zao na ku-paste bila kusoma Job Descriptions. Sasa some Clients huwa wanaweka mitego kuwanasa watu wa aina hiyo! Kwa mfano, angalia hii kazi hapa chini:-
Sasa ukiangalia hiyo kazi, ndani ya maelezo ya job description, ame-include "
Btw, please create a G doc that says "hey Jason" and includes a link at the start of your application." Huo moja kwa moja ni mtego wa kuwakamata watu wa copy and paste bila kusoma job description! Ina maana usiposoma, hutaona maelekezo ya kuweka Google Doc link yenye maneno "hey Jason" ambayo kimsingi hayana maana yoyote kwenye kazi husika! Mwingine kati katikati ya job description angeweza kuandika "...at the start of your application, write the first name of the US President"!
Hao wanachofanya, wakifungua tu wanaangalia neno la kwanza kwenye application na wakiona hakuna jibu la mtego wao, wanaitupa kapuni!!!
Hata hivyo, 99% ni kama Wajinga manake huwa wanatumia the same keywords "start" So, ukiona maelezo ni marefu ni marefu sana, tumia keyboard yako ku-click CTRL+ F to find a keyword START, na ukifanya hivyo within a second or two, utakutana na huo mtego kwa sababu ame-include the keyword START!!!
Lakini pamoja na hayo, ni MUHIMU SANA kupitisha macho kwa haraka haraka sana throughout the job description, na hiyo itakuwezesha kuyaona maelezo kama ya hapo kwenye BLUE na RED Chini kabisa!! Hayo maelezo ya Blue yatakuwezesha ku-edit kidogo template yako ambayo huenda haitakuwa na maelezo yanayojibu hizo blue requirements. Aidha, hayo maelezo ya chini kabisa (RED) utaona yametoa requirement ya hiyo kazi ambayo ni video (wengi huwa wanataka voice note). Huo sio mtego bali ni requirement especially kwa kazi za Phone Sales/Telemarketing & phone Customer Service. Lengo lao hapa ni kujua kama upo Fluent in English na HAUNA Strong Accent! In most cases, hata kama upo fluent lakini strong accent ina uwezekano mkubwa wa kukufanya upigwe chini!!!