Dini ipo ndani ya moyo wako. Dini ni upendo. Dini ni uwazi. Dini sio haya mashirika mnayoenda kuyafaidisha na kutimiza itikadi zao.

Dini ipo ndani ya moyo wako. Dini ni upendo. Dini ni uwazi. Dini sio haya mashirika mnayoenda kuyafaidisha na kutimiza itikadi zao.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Mmekuwa manipulated kwa enzi na enzi kumuunganisha Mungu na dini.

Mmekuwa brainwashed kuona njia ya kumifikia Mungu ni dini.

Mungu sio dini, Dini sio Mungu.

Dini hizi ambazo viongozi wenu wanalindwa na mabaunsa huku wakiwahamasisha msiwe na hofu Mungu yuko na nyie.

Dini hizi ambazo viongozi wenu wanahamasisha mfanye maandamano kupinga ujenzi wa unaofanya na dini tofauti na yenu wa jumba la kuabudu Mungu huyo huyo mnaemtegemea.

Dini hizi ambazo viongozi wenu hawapatii majibu ya uhakika kwanini walibadirisha baadhi ya vifungu kwenye kitabu kitakatifu ili kiendani na miiko yao.

Mara ya mwisho lini umetengeneza madhabahu moyoni mwako kwa ajili ya ibada ya alie juu.

Mara ya mwisho ni lini umepaandaa sehemu ya nyumba yako kuwa mahala pa faragha ya kumfikia Muumba wako.

Hauwezi hayo yote, kwa maana umeshakuwa engineered kwa kukimbilia kwenye mashirika na kuyafaidisha huku roho yako ikibaki chalii na kuendelea kujilaumu labda haufanyi jitihada kubwa kwenye mashirika hayo ndio maana labda mikosi haiishi.

Kilichofatia, wamekuwa mabilionea huku mkibaki kuwa wanajeshi wa itikadi zao. Imebaki sasa kuwaambia mjiandae na vita ya tatu ya dunia kwamba mtakuwa mnapiga kwa ajili ya Mungu, kumbe ni kwa ajili yao.

Nampenda Mungu ila sio Dini.
 
Una hoja ya msingi kabisa..tizama kiboko ya wachawi alivyobaka imani za wengi ..aliwafanya weeeee huku akiwaibia kwa tittle ya unabii
 
Una hoja ya msingi kabisa..tizama kiboko ya wachawi alivyobaka imani za wengi ..aliwafanya weeeee huku akiwaibia kwa tittle ya unabii
Hahahah wamebaki na njaa yeye anatanua
 
Back
Top Bottom