Ungekuwa smart kama ungetoa mifano ya hiyo michanganyo kuliko kuandika vitu kama vile wote tumefundishwa na mwalimu mmoja au tumevisoma wote kwa pamoja hivyo vitabu
Ni dini gani inakufundisha kuikataa sayansi? Kwa nini unafikiri dini na sayansi vimepingana? Sayansi inaanza na ku observe nature, study it, experiment it na baadae kuja na uvumbuzi. Dini inajaribu kujibu maswali kama tumetoka wapi, kwa nini tuko duniani na hatima yetu kama binadamu ni nini? Hamna sayansi iliyo na majibu ya maswali haya mpaka leo
Hayo ya wafuasi wa dini kushabikia pande zinazogombana ni matatizo yao binafsi labda na viongozi wao vipofu, at least kwenye mafundisho ya Biblia nina uhakika hakuna mahali inatuambia kushabikia upande wa Israeli inapofanya mauaji ya wasio na hatia.
Lakini pia sijaona sayansi ikija na suluhisho la huo mgogoro. Halafu 86% ya wamarekani hawana dini umetoa wapi hizi takwimu. Yani hata kwa ku google tu from different sources utaona stats zao zinasema US has above 50% only Christians.
Hao wavumbuzi wa technologies mbalimbali wote hawana dini? Technologies nyingi za leo zimewezekana kwa sababu ya sayansi iliyofanyiwa kazi na wanasayansi walioamini katika uwepo wa Mungu kuanzia kina Isaac Newton mpaka kina Albert Einstein. Nimesema hivi kwa sababu umegusia Atheism, labda kama ungetofautisha dini na theism.
Leo hii kuna shule na vyuo vikuu vingi vilivyoanzishwa na taasisi za dini ambavyo vime produce wanasayansi wakubwa duniani.
Ungeweka hapa details kidogo tujifunze vizuri hoja yako lakini kukataa uwepo wa Mungu au dini jumla jumla bila hoja yoyote hakukufanyi wewe au watu wa aina yako kuwa na akili.