Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Mkuu miongoni mwa watu wenye upeo mkubwa wa kujibu maswali yanayotatiza miongoni mwa watu na kuonekana kana kwamba hayawezi kujibika ww umeweza kuyajibu kwa usahihi zaidi..

Kuhusu sayansi haiwezi kujibu mambo yote kuhusiana na maisha.

Ikiwa leo kila kitu kinajiendesha kwa utaratibu uliopangwa kwa maana yupo mpangaji(muanzilishi) itawezekanaje kila kitu kwa dunia?

Maana ukisema hakuna dini ni sawasawa na kusema hakuna muumba.

Swali la msingi ni kujua tu ni ipi dini sahihi na ipi sio sahihi, hapa ndipo panapohitajika tafiti za kielimu pasina kuendeshwa na utashi wa nafsi.
Ndio hakuna muumba
 
Yes, dini ni kwa ajili ya watu wasio na ufikiri sahihi. Dini ina vitu ambavyo ni vya watu wa akili za chini sana.

Vitabu vyote vya dini vina michanganyo isiyohitaji hata kutumia nguvu kujua kuwa "hapa tumepigwa na tunaendelea kupigwa"

Sayansi imejibu maswali mengi sana ambayo dini ilishindwa kuyajibu na kuishia kuwaambia wafuasi waamini tu bila kuona!

Sayansi imetibu magonjwa complex ambayo dini haijawahi hata kuyagusa, inaishia kujipenyeza kitapeli tu.

Mf katika mgogoro wa leo wa Gaza, dunia imegawanyika. Watu wasio na uelewa wanaishia kuchagua upande wa dini A na dini B. Wale wanaoiunga mkono Israel kwa kisa cha dini ya ukristo wajue kuwa % kubwa ya waisrael hawaakini ktk dini na Marekani 86% hawana dini. Pale kinachogombewa ni Maslahi tu!

Dini zetu tungeachana nazo tungekuwa na maendeleo makubwa. Mf China na Nchi za Ulimwengu wa kwanza, nyingi zimeachana na mambo ya dini na zinaendelea sana.

Watu wanavumbua issues za drones, AI na mirobotic machines kibao we unakesha kanisani eti uwe millionea, sijui upate mtoto real?

Unalala na vichupa vya maji sijui chumvi na mafuta ya upako upate gari, are u serious?

Nilikua namsikiliza Shehe/Maalim mmoja anasema wale kunguni wa Ufaransa ni jeshi la Allah limekuja kuwaangamiza kisa wana madhambi...are we real serious?

Dini zina mfumo ambao Unatufanya "tuwe limited" kwenye ufikiri na uvumbuzi.

Live your live, Death is the Ending game! Dini ni ulaji wao!

Atheists make sense than who are not
Nina uhakika fika bado science haijakupa majibu unayoyataka mpk kufikia kuandika unavyojisikia upate kjitetea na kuzidi kujidanganya ww mwenyewe.
 
Mf China na Nchi za Ulimwengu wa kwanza, nyingi zimeachana na mambo ya dini na zinaendelea sana.
Ukiwa mwongo ujue namna ya kuwa na kumbukumbu. China hawana dini..? Nachojua china wana dini yao.

Halafu pia kuna wana sayansi km albert eistein walikua na imani kubwa saana kwa Mungu.

Soo hata sayansi inategemea imani ili kuwa na nia ya kutafuta chanzo mpaka hitimisho.

Dini ni ya watu wenye akili sema vichaa ndio hawana dini
 
Sayansi haiendani na miujiza, kimsingi kabisa. Sayansi inaendana na mambo yanayoweza kuelezeka, kupimika, kuthibitishika, kufanyiwa majaribio na kurudiwa, kwa kanuni za kisayansi ambazo hazina miujiza.

Ukishaingiza kitu chochote chenye muujiza, hicho kinapingana na sayansi.

Hivyo, Mungu wa miujiza anapingana na sayansi.

Huwezi kusema unaikubali sayansi, halafu hapo hapo unamkubali Mungu wa miujiza.

Hiyo ni contradiction.
Mkuu, hakuna mtaala wa kisayansi unaokulazimisha kutoamini uwepo wa Mungu anayefanya miujiza. Sayansi haitumii Imani katika kufanya kazi kwake na Imani haithibitishwi na sayansi katika kufanya kazi kwake.

Ukisema huwezi kuwa mwanasayansi na huku unaamini katika Mungu(au kuwa na Imani ya kiroho) maana yake wewe ni kama roboti ambaye hufanya kazi kwa kutumia pre-defined set of rules na huwezi kuishi/kufikiri in some other dimension inayokupa uwezo wa kujua kinachoendelea au kufanya maamuzi, nje ya established scientific principles.

Wakati huo huo unakuwa umemaanisha Mungu umefanikiwa kum define using your scientific approach na umethibitisha pasi na shaka kuwa Mungu na Sayansi cannot co-exist. Otherwise hiyo concept inabaki kuwa Imani kama Imani nyingine.

Halafu mbona wako wanasayansi wengi wakubwa tu wanaoamini katika Mungu. Sijui hili unalielezeaje.
 
Mkuu, hakuna mtaala wa kisayansi unaokulazimisha kutoamini uwepo wa Mungu anayefanya miujiza. Sayansi haitumii Imani katika kufanya kazi kwake na Imani haithibitishwi na sayansi katika kufanya kazi kwake.

Ukisema huwezi kuwa mwanasayansi na huku unaamini katika Mungu(au kuwa na Imani ya kiroho) maana yake wewe ni kama roboti ambaye hufanya kazi kwa kutumia pre-defined set of rules na huwezi kuishi/kufikiri in some other dimension inayokupa uwezo wa kujua kinachoendelea au kufanya maamuzi, nje ya established scientific principles.

Wakati huo huo unakuwa umemaanisha Mungu umefanikiwa kum define using your scientific approach na umethibitisha pasi na shaka kuwa Mungu na Sayansi cannot co-exist. Otherwise hiyo concept inabaki kuwa Imani kama Imani nyingine.

Halafu mbona wako wanasayansi wengi wakubwa tu wanaoamini katika Mungu. Sijui hili unalielezeaje.
Hakuna muujiza katika sayansi.

Unaelewa hilo?
 
Ungekuwa smart kama ungetoa mifano ya hiyo michanganyo kuliko kuandika vitu kama vile wote tumefundishwa na mwalimu mmoja au tumevisoma wote kwa pamoja hivyo vitabu

Ni dini gani inakufundisha kuikataa sayansi? Kwa nini unafikiri dini na sayansi vimepingana? Sayansi inaanza na ku observe nature, study it, experiment it na baadae kuja na uvumbuzi. Dini inajaribu kujibu maswali kama tumetoka wapi, kwa nini tuko duniani na hatima yetu kama binadamu ni nini? Hamna sayansi iliyo na majibu ya maswali haya mpaka leo


Hayo ya wafuasi wa dini kushabikia pande zinazogombana ni matatizo yao binafsi labda na viongozi wao vipofu, at least kwenye mafundisho ya Biblia nina uhakika hakuna mahali inatuambia kushabikia upande wa Israeli inapofanya mauaji ya wasio na hatia. Lakini pia sijaona sayansi ikija na suluhisho la huo mgogoro. Halafu 86% ya wamarekani hawana dini umetoa wapi hizi takwimu. Yani hata kwa ku google tu from different sources utaona stats zao zinasema US has above 50% only Christians.

Hao wavumbuzi wa technologies mbalimbali wote hawana dini? Technologies nyingi za leo zimewezekana kwa sababu ya sayansi iliyofanyiwa kazi na wanasayansi walioamini katika uwepo wa Mungu kuanzia kina Isaac Newton mpaka kina Albert Einstein. Nimesema hivi kwa sababu umegusia Atheism, labda kama ungetofautisha dini na theism.

Leo hii kuna shule na vyuo vikuu vingi vilivyoanzishwa na taasisi za dini ambavyo vime produce wanasayansi wakubwa duniani.

Ungeweka hapa details kidogo tujifunze vizuri hoja yako lakini kukataa uwepo wa Mungu au dini jumla jumla bila hoja yoyote hakukufanyi wewe au watu wa aina yako kuwa na akili.
Wow!
 
Kwenye sayansi hakuna kuamini wala hakuna muujiza.

Na sayansi haiendi kwa kufuata mtu gani anaamini nini, hii ni logical fallacy ya "argument from authority".

Unajionesha hujui sayansi wala logic.
Kwa akili zako anayepinga uwepo wa chanzo(nguvu) ndie anayeijua sayansi?
 
Kwa akili zako anayepinga uwepo wa chanzo(nguvu) ndie anayeijua sayansi?
Hapo umefanya logical fallacies mbili za logical non sequitur.

Kwanza, kwa muktadha wa uzi huu, umelazimisha chanzo kiwe Mungu. Hili si lazima.

Inawezekana mtu asipinge uwepo wa chanzo, lakini chanzo kikawa si Mungu.

Pili, umelazimisha chanzo kiwepo. Hili si lazima.

Katika sayansi, suala la chanzo si la lazima.

Vitu vinaweza kuwepo kwa quantum causal loop. Maana yake chanzo A kinaweza kusababisha matokeo B ambayo hayo matokeo B pia yakawa ndiyo chanzo cha matokeo A.

This is science, katika quantum physics causality breaks down na suala lako la chanzo ukilifanya la msingi, utakuwa unajionesha tu kuwa hujui quantum physics.

Kama unataka tuchambue zaidi maandiko ya kitaalamu ya sayansi kuhusu hili, naweza kukuwekea hapa.

So yes, watu walioisoma sana quantum physics wanapinga dhana nzima ya kwamba chanzo ni kitu cha msingi.

Kwa sababu dhana nzima ya cause and effect, inayokwambia kitu A ndicho chanzo kilichopelekea kitu B kuwapo, ukiitqzama hiyo dhana kwa undani at the quantum level, inavunjika katika quantum causal loop.

Google that.
 
Kwenye sayansi hakuna kuamini wala hakuna muujiza.
Naomba nijaribu kuweka sawa kidogo...
Muujiza ni nini?
Muujiza ni Sayansi ambayo ujuzi juu ya utendaji kazi wake bado haujajulikana au unafahamika Kwa mtu mmoja au watu wachache tu.
Mfano,..mtu akiunda bunduki kwa namna tusioifahamu tutasema ni muujiza Kwa kuwa hatujui formula na ujuzi aliotumia kuunda bunduki hiyo.

Kwa mantiki hiyo basi, ujinga(kukosa ujuzi juu ya jambo Fulani) ndiyo unafanya baadhi ya vitu tuvione ni muujiza lakini kiuhalisia muujiza ni sayansi tu kama zilivyo sayansi nyingine. Au naweza kusema MUUJIZA NI TAWI KATIKA MATAWI YA ELIMU kama tu ilivyo sayansi 👊

Ujinga unaweza kusababisha kitu kionekane kama muujiza.

Kwa mfano, katika siku za zamani, watu wangeweza kuamini kuwa umeme ni muujiza. Hata hivyo, baada ya tafiti na kuelewa jinsi umeme unavyofanya kazi, hakuna mtu tena anayeamini kuwa ni muujiza.
 
So yes, watu walioisoma sana quantum physics wanapinga dhana nzima ya kwamba chanzo ni kitu cha msingi.

Kwa sababu dhana nzima ya cause and effect, inayokwambia kitu A ndicho chanzo kilichopelekea kitu B kuwapo, ukiitqzama hiyo dhana kwa undani at the quantum level, inavunjika katika quantum causal loop
Katika kufanya vitu kisayansi na kuthibitisha fanya ujaribu kitu kimoja. 'Uexperiment'

Amua kutumia data zinazofikika na wewe binafsi, kutetea au kupinga dhana fulani fulani. Ntafafanua.

Mfano kwenye vya kuonekana achana na vya darubini; mambo ya anga za mbali, nebula na sayari. Chukua unavyoona kwa macho, kwa miwani na hata ukifika kwa hadubini ya mwanga kama seli na tishu. Lakini achana na vilivyo tata zaidi kama vya electron microscope. Tafuta ushahidi humo.

Maana unajuaje kama hakuna uwezekano elimu fulani ikawa imebuniwabuniwa tu (kama moon landing labda ingekuwa ni uongo kweli) yakaundwa ma modeli halafu yakawa hata ni sio au hayajakamilika kwa hiyo yakakupa tafsiri mbovu ya uhalisia?

Unaweza kukuta hawaioni cause ya effect kwa sababu kuna cause ambayo bado haipimiki au haijagundulika inayoviweka katika mwendo. Sayansi inakua kila siku.
 
Back
Top Bottom