Nmekumbuka jambo, Kuna wagonjwa huwa haijulikani anaumwa ugonjwa gani nini...Mtu anapelekwa hospitali kubwa huko India lakini haijulikani ugonjwa wake ni nini haswa, Ndugu wanaamua kumrudisha nyumbani wakisubiri kifo chake....EMU naomba unielezee hili jambo huwa kuna shida gani mpaka science inashindwa kung'amua ugonjwa kwa watu kama hawa ?
Twende na mantiki.
Unakubali kwamba, tunaweza kujua jibu hili si sahihi, kabla hata hatujajua jibu sahihi ni lipi?
Yani unaelewa kwamba ukiniletea mwanamme wa miaka 30 leo, Juma, ukaniletea na binti mchanga wa miezi 6 leo, Suzy, ukaniambia huyu binti wa miezi 6 leo ndiye mama mzazi wa huyo mwanamme mwenye miaka 30 leo, naweza kujua habari hii si sahihi, binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, bila hata kumjua mama mazazi wa huyo mwanamme mwenye miaka 30 leo ni nani?
Shida haijajulikana. Hilo halinizuii mimi kujua kwamba majibu fulani si majibu sahihi.
Kwani body of work ya sayansi inasema inajua kila kitu leo ?
Kwani sayansi kutojua kitu maana yake tatizo ni uchawi au supernatural reason?
Mbona kabla ya sayansi kujua bacteria na viruses, magonjwa ya bacteria na viruses yalijuwapo, sasa wakati huo haya magonjwa yalisababishwa na supernatural causes?
Kwa nini inakuwa vigumu sana kusema "huu ugonjwa hatuujui, inatubidi tuuchunguze tuuelewe kwanza, halafu tutaudhibiti baada ya kuuelewa" ?
Kwa nini tukikutana na kitu hatukielewi, tunakimbikia kwenye uchawi na supernatural reasons?
Mbona magonjwa mengi tu hapo awali hatukuyajua, lakini tulifanya utafiti mpaka tukayaelewa?
Sasa, na leo tukikutana na ugonjwa hatuuelewi, kwa nini tunakimbilia habari za uchawi na supernatural reasons badala ya kufanya uchunguzi tuelewe mambo within a natural framework?
Unaelewa kwamba tunaweza kujua kuwa jibu fulani si sahihi, kabla hata ya kujua jibu sahihi ni lipi?
Unaielewa hiyo dhana kwamba tunaweza kujua jibu fulani si sahihi, kabla hata ya kujua jibu sahihi ni lipi?