Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Ndio hakuna muumba
 
Nina uhakika fika bado science haijakupa majibu unayoyataka mpk kufikia kuandika unavyojisikia upate kjitetea na kuzidi kujidanganya ww mwenyewe.
 
Mf China na Nchi za Ulimwengu wa kwanza, nyingi zimeachana na mambo ya dini na zinaendelea sana.
Ukiwa mwongo ujue namna ya kuwa na kumbukumbu. China hawana dini..? Nachojua china wana dini yao.

Halafu pia kuna wana sayansi km albert eistein walikua na imani kubwa saana kwa Mungu.

Soo hata sayansi inategemea imani ili kuwa na nia ya kutafuta chanzo mpaka hitimisho.

Dini ni ya watu wenye akili sema vichaa ndio hawana dini
 
Mkuu, hakuna mtaala wa kisayansi unaokulazimisha kutoamini uwepo wa Mungu anayefanya miujiza. Sayansi haitumii Imani katika kufanya kazi kwake na Imani haithibitishwi na sayansi katika kufanya kazi kwake.

Ukisema huwezi kuwa mwanasayansi na huku unaamini katika Mungu(au kuwa na Imani ya kiroho) maana yake wewe ni kama roboti ambaye hufanya kazi kwa kutumia pre-defined set of rules na huwezi kuishi/kufikiri in some other dimension inayokupa uwezo wa kujua kinachoendelea au kufanya maamuzi, nje ya established scientific principles.

Wakati huo huo unakuwa umemaanisha Mungu umefanikiwa kum define using your scientific approach na umethibitisha pasi na shaka kuwa Mungu na Sayansi cannot co-exist. Otherwise hiyo concept inabaki kuwa Imani kama Imani nyingine.

Halafu mbona wako wanasayansi wengi wakubwa tu wanaoamini katika Mungu. Sijui hili unalielezeaje.
 
Hakuna muujiza katika sayansi.

Unaelewa hilo?
 
Wow!
 
Kwenye sayansi hakuna kuamini wala hakuna muujiza.

Na sayansi haiendi kwa kufuata mtu gani anaamini nini, hii ni logical fallacy ya "argument from authority".

Unajionesha hujui sayansi wala logic.
Kwa akili zako anayepinga uwepo wa chanzo(nguvu) ndie anayeijua sayansi?
 
Kwa akili zako anayepinga uwepo wa chanzo(nguvu) ndie anayeijua sayansi?
Hapo umefanya logical fallacies mbili za logical non sequitur.

Kwanza, kwa muktadha wa uzi huu, umelazimisha chanzo kiwe Mungu. Hili si lazima.

Inawezekana mtu asipinge uwepo wa chanzo, lakini chanzo kikawa si Mungu.

Pili, umelazimisha chanzo kiwepo. Hili si lazima.

Katika sayansi, suala la chanzo si la lazima.

Vitu vinaweza kuwepo kwa quantum causal loop. Maana yake chanzo A kinaweza kusababisha matokeo B ambayo hayo matokeo B pia yakawa ndiyo chanzo cha matokeo A.

This is science, katika quantum physics causality breaks down na suala lako la chanzo ukilifanya la msingi, utakuwa unajionesha tu kuwa hujui quantum physics.

Kama unataka tuchambue zaidi maandiko ya kitaalamu ya sayansi kuhusu hili, naweza kukuwekea hapa.

So yes, watu walioisoma sana quantum physics wanapinga dhana nzima ya kwamba chanzo ni kitu cha msingi.

Kwa sababu dhana nzima ya cause and effect, inayokwambia kitu A ndicho chanzo kilichopelekea kitu B kuwapo, ukiitqzama hiyo dhana kwa undani at the quantum level, inavunjika katika quantum causal loop.

Google that.
 
Kwenye sayansi hakuna kuamini wala hakuna muujiza.
Naomba nijaribu kuweka sawa kidogo...
Muujiza ni nini?
Muujiza ni Sayansi ambayo ujuzi juu ya utendaji kazi wake bado haujajulikana au unafahamika Kwa mtu mmoja au watu wachache tu.
Mfano,..mtu akiunda bunduki kwa namna tusioifahamu tutasema ni muujiza Kwa kuwa hatujui formula na ujuzi aliotumia kuunda bunduki hiyo.

Kwa mantiki hiyo basi, ujinga(kukosa ujuzi juu ya jambo Fulani) ndiyo unafanya baadhi ya vitu tuvione ni muujiza lakini kiuhalisia muujiza ni sayansi tu kama zilivyo sayansi nyingine. Au naweza kusema MUUJIZA NI TAWI KATIKA MATAWI YA ELIMU kama tu ilivyo sayansi 👊

Ujinga unaweza kusababisha kitu kionekane kama muujiza.

Kwa mfano, katika siku za zamani, watu wangeweza kuamini kuwa umeme ni muujiza. Hata hivyo, baada ya tafiti na kuelewa jinsi umeme unavyofanya kazi, hakuna mtu tena anayeamini kuwa ni muujiza.
 
Katika kufanya vitu kisayansi na kuthibitisha fanya ujaribu kitu kimoja. 'Uexperiment'

Amua kutumia data zinazofikika na wewe binafsi, kutetea au kupinga dhana fulani fulani. Ntafafanua.

Mfano kwenye vya kuonekana achana na vya darubini; mambo ya anga za mbali, nebula na sayari. Chukua unavyoona kwa macho, kwa miwani na hata ukifika kwa hadubini ya mwanga kama seli na tishu. Lakini achana na vilivyo tata zaidi kama vya electron microscope. Tafuta ushahidi humo.

Maana unajuaje kama hakuna uwezekano elimu fulani ikawa imebuniwabuniwa tu (kama moon landing labda ingekuwa ni uongo kweli) yakaundwa ma modeli halafu yakawa hata ni sio au hayajakamilika kwa hiyo yakakupa tafsiri mbovu ya uhalisia?

Unaweza kukuta hawaioni cause ya effect kwa sababu kuna cause ambayo bado haipimiki au haijagundulika inayoviweka katika mwendo. Sayansi inakua kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…