Sawa, Nakuuliza swali
Maisha ni nini ? Lipi lengo la uwepo wetu duniani kwa mujibu/mtizamo wako ?
Maisha ni mfumo wa kuendelea kwa viumbehai kufanya mambo kama kula, kufanya metaboli, kutoa uchafu, kupumua, kusogea, kukua, kuzaana na kuzijibu stimuli za kutoka nje.
Unapotumia neno "lengo" unatoa picha kwamba kuna kitu maalum kimelengwa kwa sisi kuwapo, huu ni mtizamo wa kidini, kwamba, kuna muumbaji, muumbaji ana lengo, na katuweka hapa duniani kutimiza lengo.
Ama pia unaweza kuwa ni mtizamo wa kwamba kuna special design, mambo yamepangwa, sasa unatafuta kujua mpango umepanga kwenda wapi?
Ukiondoka kwenye habari za dini/ special design, ambako mimi sipo, hakuna lengo maalum la sisi kuwapo hapa.
Evolution is driven by random mutations. There is no special direction it is taking, other than natural selection.
Baiolojia inaweza kufanya mambo fulani yawe kama malengo. Kwa mfano, kuzaana ni kitu ambacho kibaiolojia kimekuwa kama lengo. Ubongo na mwili wako umefanywa kibaiolojia kupenda kufanya mambo ambayo yatahakikisha tutaendelea kuzaana. Unapenda kula, unapenda kufanya mapenzi, unasikia maumivu ukiunguzwa na moto, na inevitably ukiishi sana kwa kula na kufanya mapenzi, na kuepuka kuunguzwa na moto, chances are, utapata mtoto na kizazi kitaendelea.
So, hapo utaona mazingira yetu yametuwekea malengo ya kiasili kama hayo ya kuzaana, lakini huwezi kusema kwamba lengo la sisi kuwapo ni kuzaana, kwa sababu kuna watu wengi wanaishi vizuri tu bila kuzaana na wame adopt watoto, au wanaishi bila watoto.
Maisha hayana lengo, hii habari ya lengo ni habari ya kidini.
Ila, hilo halikuzuii wewe binafsi kuyapa lengo maisha yako. Kwa mfano, mtu anayezaliwa katika nchi inayotawaliwa kidhalimu au kikoloni, akayapa maisha yake lengo la kuikomboa nchi yake ijitawale, akapigania hilo mpaka kulifanikisha, anakuwa kaishi maisha yenye maana sana kwa watu wengi sana.
Mtu aliyeona jamii yake haina madaktari wa kutosha, inasumbuliwa na mambo ya afya, akasoma ili kuongeza madaktari, akafanya lengo la maisha yake ni kupunguza matatizo ya afya, akafanikiwa sana kwenye hilo, anakuwa kayapa maisha yake maana kubwa sana.Tunao hawa wengi sana.
Hivyo, maisha hayana lengo, wewe mtu unayeishi ndiye unayapa maisha yako lengo.
Maisha ni kama gari. Wewe ni dereva. Gari halina pahali linapokwenda. Wewe dereva ndiye una safari, una sehemu unataka kwenda, wewe ndiye unaamua gari liende wapi, au hata kusema hutaki safari, unataka kupumzika tu.
Ndiyo maana hata hiyo evolution iliyokuwa inaenda kwa random mutation na natural selection, siku hizi watu wanaiingilia kwa gene editing/ CRISPR, tunaenda kwenye cybernetic organism na artificial intelligence.
Tunaamua baiolojia yetu iweje, maisha yetu yaweje.
Tunayapa maana na malengo tunayotaka maisha yetu, hatuulizi lengo la maisha ni nini.