Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

@Jumong S Hii mada bado inaendelea? By the way Adam na Hawa walizaa watoto wengi wa kiume na wa kike. Basi ni wazi kuwa Kaini alipooa alimchukua dada yake maana ndio waliokuwa duniani.
Imeandikwa wapi Kaini alioa dada yake? Kwanza walikua wawili then akamuua mdogo ake Abel, kisha akafukuzwa akaenda nchi ya Nod, akaoa na kuzaa huko. Swali, watu wa Nod walitoka wapi? Adam na Eva waliwazaa lini watu wa Nod??? Kaini alimzaa Henoko na akajenga mji akauita Henoko kwa jina la mwanae. Je, huo mji waliishi akina nani wkt alikuwepo Kaini, mkewe na mtoto wao Henoko??

Kuna lot of gaps hapa!
 
Ulimwengu wa dini umejaa matapeli wengi, wanajipigia wajinga tuu...kila siku wanawatajirisha welevu
 
Ila ni mtu mjinga tu asiyeamini uwepo Wa Mungu.Nawahakikishia Mungu yupo.kwanza uwepo wa Mungu unathibitishwa na uwepo wa Sayari ya dunia.angalia uzuri wa Dunia.Angalia mifumo ya dunia yaani kila kitu kimeundwa kwa akili kubwa.kaweka mifumo ya upatikanaji wa maji,kaweka mimea na miti,kaweka wanyama na samaki,kaweka bahari na nchi kavu.yaani kila kitu kimedesigniwa kwa ustadi mkubwa na maarifa makubwa.mfano akasema ngoja tuweke dunia kwa umbali fulani kutoka kwenye jua sio akili ndogo hii ndo sababu mojawapo ya maisha kuwepo duniani.kwa hiyo huhitaji kwenda kwenye vitabu ukitumia akili tu unaweza kusema kuna natural force Sehemu bigger than everything.yaani kuna Mungu.
 
Pia Ubovu wa hizi dini zetu hauhalalishi kutokuwepo kwa Mungu kwa sababu hizi dini zetu zinaongozwa na binadamu wenye tamaa.Na pia sio kila dini ni ya ukweli.ninauhakika na asilimia nyingi ukristo ndo dini ya ukweli.lakini binadamu ndo wanaharibu hii dini kwa kuingiza maovu yao.
 
Sawa wa hayo yote umetoa wapi si ufikiri wako ni vitabu vya hadithi na sayansi uka summarize ukaja na hoja sasa basi vitabu vya wanasayansi na vya manabii vipi bora sisi tunaoamini tunaona bora vya manabii wewe ambae huamini fata vitabu vya wanasayansi
 
Kwasababu hakuna anayejua for sure ulimwengu huu umefanyikaje, ina wezekana hiyo high power above all iliofanya ulimwengu ipo....... LAKINI SIO MUNGU WA KWENYE HEKAYA ZA BIBILIA, QURAN NK. Big No
 
Kuamini ni matokeo ya ujinga
 
Uko sahihi kabisa
 
So, Natural force ndo Mungu? Umezungumzia uzuri, na ubaya je?


 
Kuna dini zilianza Miaka zaidi ya 300,000 kabla ya Ukristo, why uamini Ukristo ndi ukweli? Kwa nn Mungu asiweke dini moja na miungu isiabudiwe kabisa?:Si anao uwezo huo? Hii mikanganyiko ya nani yupi sahihi na nani hayupo sahihi ndo inaleta maswali...
 
Vitabu vya manabii vimejaa ndoto na fikra zisizo na uhakika...mengi ni dhahania. Vitabu vya Sayansi vinakupa matokeo kabisa. Mf Mgonjwa wa UTI tunajua kabisa amekua affected na Eschricia coli na dawa ya kuwaua hawa bacteria ni Cipro, Nitrofurantoin, Amoxcillin au Azithromycin...proved and effective.

Sasa ww nabii anakuambia kaombewe sijui unywe maji ya upako utapona...wengi wanaishia kutapeliwa.

Sayansi gives more answers than Dini!
 
Sir Isaac Newton, mwingereza huyu, ni moja kati ya Wanasayansi wakubwa tu walioeahi kuishi kwenye uso wa dunia na ni moja kati ya watu wenye IQ kubwa tu kuwahi kuwepo duniani na alikuwa Mwanathiolojia (Elimu ya dini na mambo ya kale) mzuri tu na alikuwa anaamini katika dini na alikuwa anaamini katika MUNGU na aliwahi ku
Sir Isaac Newton, mwingereza huyu, ni moja kati ya Wanasayansi wakubwa tu kuwahi kuishi kwenye uso wa dunia na ni moja kati ya watu wenye IQ kubwa tu kuwahi kutokea duniani na alikuwa Mwanatheolojia mzuri tu wa mambo ya dini na alikuwa anaamini katika uwepo wa MUNGU, ko akili na imani havina uhusiano kabisa, imani inaanzia pale akili inapokomea!
 
Ukikubali Mungu wa miujiza ambaye hapingiki wala kuthibitishika kisayansi umeshapingana na sayansi.

Ukikubali Mungu anayepimika na kuthibitishika kisayansi, umeshamuondoa huyo Mungu kwenye uungu na kumuweka kwenye kanuni ya sayansi tu.
Mungu ameshawahi kuwepo duniani na kutembea kama binadamu wa kawaida na kula na kunywa kama binadamu! Mtihani ulikuwa ni kuamini kwamba ndiye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…