Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Kabla ya kukuthibitishia, je, unaamini kwamba Mungu yupo?
Kwa nini kuamini kuwe ni jambo muhimu?

Ikiwa mimi kuamini au kutoamini hakuwezi kubadili ukweli.

Kama Mungu yupo, halafu mimi naamini hayupo, hilo halibadilishi ukweli kwamba yupo. Imani yangu ina umuhimu gani hapo?

Kama Mungu hayupo, halafu mimi naamini yupo, hilo halibadilishi ukweli kwamba hayupo. Imani yangu ina umuhimu gani hapo?

Kwa nini unaona imani ni kitu muhimu wakati imani si lazima iwe katika kweli?

Kea nini unapngelea imani, badala ya fact?
 
Kwasababu kumjua Mungu hakuhitaji akili za kibinadamu, ko nitakapokuwa nathibitisha kwamba Mungu aliwahi tembea dunia kama binadamu utakataa kwakuwa hakutakuwa na ushahidi wa kuonekana kwa macho.

Lakini pia nitatumia biblia kama kitabu cha rejea nitakapokuwa nakuthibitishia hilo jambo.

Je, unakubaliana na maandiko yaliyomo katika biblia kwamba sio visa vya kubuni?
 
Kama kumjua Mungu hakuhitaji akili za binadamu wewe umemjua kwa akiki gani, za popobawa?

Biblia ina contradiction kibao, nikikuwekea hapa huwezi kuzitatua.

Bisha.
 
Umeongea kulingana na uelewa wako,! Dini sio kigezo cha wewe kutokua na akili ya ubunifu. Unaweza fanya vitu vikubwa na bado ukawa na dini yako.
 
Binaadamu kiumbe jeuri sana.
Umeumbwa kutoka kwenye tumbo la mamaako kama tone la manii kisha ukawa pande la damu kisha pande la nyama mpaka kua kiumbe kamili, umezaliwa ukiwa huna unalolijua.

Eti baada ya kua na ufahamu unakanusha uwepo wa Mungu aliekuumba [emoji3]

Hii dunia miaka 1500 tu iliopita hakukua na hao wanasayansi wenu watu waliishi wakaja wengine mpk leo tupo sisi na miaka zaidi ya 100,000 imepita.

Ardhi na mbingu havikuumbwa ili tu uje uishi ustarehe kisha ufe ukidhani ndo umemaliza.

Hawawi sawa wenye akili na wasio na akili, na kila mmoja atalipwa kwa haki kwa alioyatenda.

Nachosema tu ni kwamba baada ya kifo ndo utajua Mungu yupo au hayupo.
 
Mungu ni roho na sayansi ni vitu vyenye kushikika. Kinachofikirisha ni ukweli kwamba hao wanasayansi Ijumaa au Jumapili wanaamkia misikitini na makanisani.

Ukiugua hata ukiwa mwanasayansi muda mfupi kabla hujaaga dunia ukiwa mkatoliki unaitiwa Padre kwa ajili ya upako wa mwisho.

Ukuu wa Mungu ni mkubwa kuliko uwezo wa wanasayansi wa kuja na majibu kwa shida za ulimwengu huu, Mfano hai ni namna Covid 19 ilivyotesa na kuua mamilioni mwishoni mwa muongo uliopita na mwanzoni mwa huu wa sasa.

Punguza kufuru, naamini umri wako ni mdogo kuna mengi utakuja kuyajua miaka ijayo.
 
Jeuri kaipata ukubwani baada ya kupata akili timamu. Mungu ni roho haonekani lakini adhabu zake zipo hai hajazisitisha.
 
Kwa huo mfano wa Covid 19, unamaanisha ndio ukuu wa Mungu katuonyesha au umemaanisha nini sijakupata.
 
Kwa huo mfano wa Covid 19, unamaanisha ndio ukuu wa Mungu katuonyesha au umemaanisha nini sijakupata.
Tuiheshimu nguvu kubwa ya muumba ipo siku zote. Tatizo la binadamu la kusahau mapema.

Kule Italia muda mfupi kabla ya ugonjwa kuibuka walifanya ushenzi mwingi sana wa ushoga, ikafika wakati wa adhabu iliyo kuu wakafa maelfu kila kukicha.

Mwanasayansi ikifika Jumapili au Ijumaa anakuwa wa kwanza kanisani au msikitini, ndio ujue nguvu ya Mungu ilivyo.

Kiburi na ukosefu mzima wa unyenyekevu ndio sababu ya kwanza ya mipango yetu mingi kufia njiani.
 
Reactions: 511
Wacha mie ningojee mabikira 72 weupe peeee,warefu macho kqma mbuni we acha tu
 
Mkuu , umeachanga ma file vibaya Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…