Kwenye swali langu sijataja neno "super natural power" Wala sijautaja uchawi
Ila nmetaka ufafanuzi, Hayo maelezo yako yote yanatoka wapi ?
Mimi nmeuliza swali moja kuwa huwa science wanafail wapi hadi wanakubali ndugu kuondoka na mgonjwa wao bila kuondoa tatizo ?
Sawa kuna majibu umenipa mwishoni kwamba science sio kwamba inafahamu kila kitu,
Nna maswali mawili moja ni ndani ya hii hoja na lingine ni nje ya hii hoja
1; Ni kwanini wasimuache huyo mgonjwa kwajili ya tafiti ili waufahamu ugonjwa huo mpya ambao hauonekani kwenye vipimo na badala yake wanaruhusu tu mgonjwa aondolewe bila wao kuambulia chochote kile ?
2; Umesema science haifahamu kila kitu, Swali, Ni kwanini mmeshahitimisha kuwa Mungu hayupo na mnajua science haifahamu kila kitu na haijavumbua vitu vingi bado ?
1. Kuna mambo mengi ya ethics, consent, economy etc yanayoweza kuzuia utafiti. Utafiti wa kiutabibu haufanyiki ovyo ovyo tu. Pia, kuna sehemu nyingi wanafanya tafiti. Hospitali moja au mbili za India hazi represent "science". Unahitaji kuelewa science ni nini kwanza. Science ni nini?
Science si hospitali fulani iliyopo India!
2. Nimekwambis kwamba, unaweza kuwa hujui jibu sahihi, lakini ukajua jibu fulani si sahihi.
Vivyo hivyo, huhitaji kujua kila kitu ili kujua jibu fulani si sahihi. Wewe hujui kila kitu, lakini, hilo halikuzuii kujua majibu fulani si sahihi.
Ni muhimu sana uelewe dhana hii, kwamba, ukiambiwa "tafuta square root ya 2". Halafu ukajua kuwa, square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, huhitaji kuhesabu namba zote ili kujua kuwa 10 si square root ya 2. In fact, katika step ya kwanza ya "elimination method", unaziondoa namba zote zilizo kubwa kuliko 2 na kusema "jibu langu haliwezi kupatikana huko, jibu ni lazima liwe dogo kuliko 2".
Huhitaji kujua namba zote ili kujua kuwa 10 si square root ya 2.
Swali lako ni kama unaniuliza mimi hivi "Wewe umesema hujui namba zote, unajuaje kuwa 10 si square root ya 2?".
Naweza kujua kuwa 10 si square root ya 2 bila kujua namba zote, tena bila kujua square root ya 2 ni nini. Kwa kujua tu kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2. Namba yoyote kubwa zaidi ya 2 haiwezi kuwa square root ya 2. Kwa sababu ita contradict kanuni muhimu kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Niilitoa mfano, mwanamme wa miaka 30 leo, Juma, ambaye hamjui mama yake mzazi, hajui kila kitu, hamjui hata mama yake mzazi, lakini, akiletewa binti mchanga wa miezi 6 leo, Suzy, na kuambiwa kuwa huyo Suzy ni mama yake mzazi Juma mwenye miaka 30, anaweza kujua kuwa huyo Suzy si mama yake mzazi, bila kujua kila kitu, bila hata ya kumjua mama yake mzazi.
Juma mwanamme mwenye miaka 30 leo hahitaji kujua kila kitu ili kujua kuwa Suzy, binti mchanga mwenye miezi 6 leo, si mama yake mzazi, hawezi kuwa mama yake mzazi, kwa sababu Juma kamzidi Suzy kwa miaka 29.5.
Sasa, swali unaloniuliza hapo, la kwamba sayansi inajuaje Mungu hayupo kama haijui kila kitu, ni sawa na kuniuliza, Juma anajuaje Suzy si mama yake mzazi wakati hajui kila kitu?
Huhitaji kujua kila kitu, wala huhitaji kujua jibu sahihi, ili kujua jibu fulani si sahihi.
Juma kajuaje Suzy si mama yake mzazi bila Juma kumjua mama yake mzazi wala kujua kila kitu?
Simple, kwa sababu jibu la Suzy kama mama mzazi wa Juma lina violate kanuni ya logical consistency. Ili Suzy awe mama mzazi wa Juma, inabidi kwanza Suzy atimize sharti la kuwa mkubwa kumpita Juma kwa miaka ya kuweza kumzaa. Suzy si tu hajampita Juma kwa umri huo, bali ni mdogo kuliko Juma kwa miaka 29.5. Hivyo tunajua Suzy hawezi kuwa mama mzazi wa Juma.
Suzy kumzaa Juma ni contradiction ya timeline ya maisha yao. Contradictiin hii inaonesha Suzy hawezi kuwa mama mzazi wa Juma.
Vivyo hivyo, kujua Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ulimwengu huu ambao unaweza kuwa na mabaya hayupo, tunatumia mantiki hiyo hiyo ya proof by contradiction.
1. Mungu ni mjuzi wa yote
2. Mungu ni mwenye uwezo wote
3. Mungu ni mwenye upendo wote
4.Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kuwepo.
1,2,3 na 4 zote haziwezi kuwa kweli bila ya contradiction, Mungu mwenye sifa za 1, 2 na 3 kuumba ulimwengu wa 4 ni contradiction.
Contradiction hii inatuonesha Mungu huyo hayupo na hawezi kuwepo, huyo Mungu ni hadithi za watu tu katika siasa zao.
Tunaweza kujua Mungu huyo hayupo bila kujua kila kitu, kwa proof by contradiction, kama tunavyoweza kujua kuwa Suzy, binti mchanga mwenye umri wa miezi 6 leo, hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme Juma mwenye miaka 30 leo.
Kwa kuangalia mantiki na contradiction.
Tatizo, wangapi wana uwezo wa kuielewa hiyo contradiction, kuikubali, kuondoka saikolojia ya "cognitive dissonance", kuondoa majadiliano yanayoongozwa na hisia badala ya kuongozwa na logic na fact?