Dini ya Kiislamu na usawa kwa Mwanaume na Mwanamke: Haki ya Mwanamke katika Elimu | Haki ya kutafuta Elimu

Dini ya Kiislamu na usawa kwa Mwanaume na Mwanamke: Haki ya Mwanamke katika Elimu | Haki ya kutafuta Elimu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Chama cha Wanasheria wa Kike Visiwani Zanzibar [Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA)] kimeandaa chapisho linalozungumzia Haki za Mwanamke linaloitwa "Haki za Mwanamke kwa Mujibu wa Qur'an na Sunnah za Mtume (S.AW)"

Katika chapisho hilo, inaelezwa kuwa Uislamu umetoa umuhimu kwa binadamu kutafuta elimu akiwa Mwanamme au Mwanamke na nyezo muhimu za kupata elimu ni kusoma na kuandika.

Mwanamke wa Kiislamu ana haki na Uhuru kamili wa kutafuta elimu na maarifa na kutumia elimu hiyo kwa njia halali. Zipo aya na hadithi nyingi zinazobainisha hayo miongoni mwa hizo ni:

Mtume (S.A.W), amesema: “Kutafuta elimu ni faradhi (lazima) kwa Muislamu mwanamme na mwanamke”. Imepokelewa na Bayhaky na Tabaraniy. Pia Mtume (S.A.W) amesema: “Anayeulizwa kuhusu taaluma akaificha, atafungwa kamba za moto siku ya kiama”. Imepokelewa na Ahmad, Abu Daud, Nasai, Tirmidhy na Ibnu Majah.

Kutokana na hadhithi za Mtume (S.A.W) hapo huu, jambo la msingi ni kutafuta elimu kwa nia ya ibada; nako ni kukusudia kujisaidia mwenyewe, jamii na taifa kimaendeleo katika nyanja zote.

Sharia ya Kiislamu inapomlazimisha mwanamke kusoma inalenga elimu za aina zote na inampasa kuifanyia kazi elimu aliyoipata. Aidha elimu iliyo bora zaidi kwa mwanamke ni ile itakayomkomboa kimaarifa na kimaisha.
 
Back
Top Bottom