Dini ya kweli ni haki, kinyume chake ni ushetani

mangikule

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
6,369
Reaction score
5,866
Nimefuatilia mijadala mingi ya kisiasa hapa.

Kuna wanaopinga au kuunga mkono tu kwa kigezo cha dini ya kiongozi mkuu.

Mijdala ilianzia mbali sana
Miaka ya tisini mbuga zetu ziliuzwa Loliondo upinzani na uungaji mkono ukalalia udini.

Miaka ya 2005 hadi 2010 ufisadi mkubwa ukajitokeza na mandala wa udini wa kiongozi ukaibuka.

Miaka ya 2015 kampeni zikaibuka na udini ukashika kasi (kura za maslahi).

Miaka hii tena 2023 kashfa ya bandari imeibua udini kwa kasi ya ajabu.

Inasikitisha;
Kwamba kiongozi asipingwe kwa lolote hata kama amevunja haki zote za binadamu kwa sababu ni wa dini yetu?

Au kiongozi aungwe tu mkono kwa sababu ya dini yake?

Au kiongozi apingwe tu kwa sababu ni wa dini fulani.

Tunahubiri haki

Dini BILA HAKI NI USHETANI

Ninawasilisha!!
 
Haki ni Nini ? Natural Justice maybe...., lakini hata hio Haki katika dunia yenye mfumo wa Samaki wakubwa kuwala wadogo (Kwamba tumekubaliana na Matabaka ndio mfumo wa Maisha) sidhani kama tafsiri ya Haki yako itakuwa sawa na yule aliye level tatu chini yako (wewe wa juu utajustify kwamba kulamba asali na wengine makombo ndio haki yao)

Matsya Nyaya​

Matsya Nyaya (Sanskrit: मात्स्यन्याय; IAST: mātsyanyāya) is an ancient Indian philosophy which refers to the principle of the Law of Fish.
 
Ushenzi tu hichi ni chama kingine kinacho jaribu kujieneza duniani kwa mwamvuli wa dini..
 
Dini ya kweli isiyo na taka Mbele ya Mungu Ni hii Kwenda Kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na Kujilinda na dunia pasipo Mawaa

Yakobo 1:27
Kuliko kuwatazama na kuwapotezea muda na kuwaacha waendelee kuwa Yatima na Wajane wawezeshe ili kusiwe na tofauti kati ya Wajane na Yatima..., I am of a belief charity inasababisha utwana na Ubwana kuondoa mzizi hata ukitoa toa kwa siri wasijue na jaribu kuwavuta waweze kujipatia na sio kupewa
 
Nimefuatilia mijadala mingi ya kisiasa hapa.

Kuna wanaopinga au kuunga mkono tu kwa kigezo cha dini ya kiongozi mkuu.

Mijdala ilianzia mbali sana
Miaka ya tisini mbuga zetu ziliuzwa Loliondo upinzani na uungaji mkono ukalalia udini.

Miaka ya 2005 hadi 2010 ufisadi mkubwa ukajitokeza na mandala wa udini wa kiongozi ukaibuka.

Miaka ya 2015 kampeni zikaibuka na udini ukashika kasi (kura za maslahi).

Miaka hii tena 2023 kashfa ya bandari imeibua udini kwa kasi ya ajabu.

Inasikitisha;
Kwamba kiongozi asipingwe kwa lolote hata kama amevunja haki zote za binadamu kwa sababu ni wa dini yetu?

Au kiongozi aungwe tu mkono kwa sababu ya dini yake?

Au kiongozi apingwe tu kwa sababu ni wa dini fulani.

Tunahubiri haki

Dini BILA HAKI NI USHETANI

Ninawasilisha!!
Haki ni ipi!?
Kuna watu wanaona haki yao kufanya ushoga je tuwaache tu kwa kuwa kuwazuia ni kuwanyima haki yao?

Kuna watu wanaona ni haki yao kuvuta bangi, je tukizuia bangi ni kuwanyima haki yao?

Wapo wanaoona ni haki yao kutembea uchi mitaani, tukiwazuia ni kuwanyima haki yao?
 
Haki ni Nini ? Natural Justice maybe...., lakini hata hio Haki katika dunia yenye mfumo wa Samaki wakubwa kuwala wadogo (Kwamba tumekubaliana na Matabaka ndio mfumo wa Maisha) sidhani kama tafsiri ya Haki yako itakuwa sawa na yule aliye level tatu chini yako (wewe wa juu utajustify kwamba kulamba asali na wengine makombo ndio haki yao)

Matsya Nyaya​

Matsya Nyaya (Sanskrit: मात्स्यन्याय; IAST: mātsyanyāya) is an ancient Indian philosophy which refers to the principle of the Law of Fish.
Eneza ujumbe wako wa haki unaouhitaji! Nasisitiza DINI bila haki ni Ushetani
 
Haki ni ipi!?
Kuna watu wanaona haki yao kufanya ushoga je tuwaache tu kwa kuwa kuwazuia ni kuwanyima haki yao?

Kuna watu wanaona ni haki yao kuvuta bangi, je tukizuia bangi ni kuwanyima haki yao?

Wapo wanaoona ni haki yao kutembea uchi mitaani, tukiwazuia ni kuwanyima haki yao?
Unaweza kueneza haki unvyotaka wewe lakini msisitizo hapa DINI BILA HAKI NI USHETANI
 
Haki ni ipi!?
Kuna watu wanaona haki yao kufanya ushoga je tuwaache tu kwa kuwa kuwazuia ni kuwanyima haki yao?

Kuna watu wanaona ni haki yao kuvuta bangi, je tukizuia bangi ni kuwanyima haki yao?

Wapo wanaoona ni haki yao kutembea uchi mitaani, tukiwazuia ni kuwanyima haki yao?
Hapa tunazungumzia rasilimali zetu, wewe kama unapenda nenda huko baravarani katembee makalio wazi ukibakwa hakuna atakayekulaumu, lakini rasilimali za taifa letu, urithi wa vizazi vijavyo zisichezewe, ukichezea, lazima uitwe jina stahiki.
 
Eneza ujumbe wako wa haki unaouhitaji! Nasisitiza DINI bila haki ni Ushetani
Hata nikieneza Haki yangu huenda isiwe Haki kwa mwingine....

Kuna Imani ambazo zinakubali mwanamke kuwa Mke mwenza Je; Hio ni Haki kwa huyo Mwanamke kama hataki ?

Na wale wenye Imani ya Kaka kurithi Mke n.k.; Na imani nyingi zinaamini kuheshimu mamlaka vipi hapo kama hayo mamlaka yanakubaliana na watawala na watawaliwa (mabwana na watwana)
 
Haki kila mtu huzaliwa nazo, somo la haki tunahitaji post pekee inayojitegemea tamko la haki za binadamu like toka 1948 baada tu ya vita vya pili vya dunia. Haki haibagui na haina udini. Dini bila haki ni ushetani.
 
Back
Top Bottom