Dini ya Simba na Yanga inavyodhoofisha maisha ya Watanzania

Dini ya Simba na Yanga inavyodhoofisha maisha ya Watanzania

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
6,432
Reaction score
25,646
Inasikitisha na kushangaza sana.

Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru,nchi ambayo inasemekana tuna utajiri wa maji kuliko nchi yoyote ukanda huu wa maziwa makuu na pengine Afirka nzima,leo tunajadili swala la mgao wa maji.Tena Kuna wengine wameenda mbali zaidi kwa kuandika makala za kuwasifia Waislamu jinsi walivyo na ukarimu kiasi Cha nyumba zao za ibada kutoa maji ya bure.Yani Tanzania leo karne ya 21 tunalia kuhusu uhaba wa maji Safi ya kunywa?

Mwaka 2013 gazeti Moja maarufu liliandika makala "Sasa Tanzania uhaba wa umeme basi.Kuuza nje ya nchi jirani pia" .

Leo mwaka 2022 tukiwa tunaumaliza tukiwa tunakaribia 2023,miaka 10 baada ya kuisoma ile makala ya siasa ila bado umeme Ni kizungumkuti,majenereta yanaunguruma kila sehemu,umeme unakatika kila saa.

Katika Dunia hii ambayo matumizi ya internet yamepelekea kuajiri vijana wengi hapa nchini,maana ajira ni kitendawili,wao wanazidi kupunguza matumizi ya data(mb) kila siku na serikali hakuna kitu inafanya.Ukiuliza unajibiwa gharama za uendeshaji zimeongezeka. Siku hizi kila siku najiunga kifurushi cha wiki.Kila siku napata meseji za hongera tu kutoka Airtel na Voda. "Hongera, umefanikiwa kujiunga kifurushi cha wiki, umepata mb 350 kwa TSH 1000" baada ya masaa mawili bando limekata,unajiunga tena Kisha tena unaambiwa hongera!!!

Mambo mengi sana,ila Kuna kitu huwa najiuliza..

Hivi ile nguvu ya watanzania , mashabiki wa club ya Simba kuandamana pale uwanjani siku wanatoka droo na timu ya KMC (narudia siyo Simba walifungwa ila ilikuwa draw),ile wanaandamana kuanzia uwanjani tena usiku "hatumtaki Matola" inatoka wapi? Au yanga juzi tu hapo kutolewa club bingwa wakaangukia shirikisho,huko clabuni ilikuwa mshike mshike nusura kocha afukuzwe.Droo na Simba ikamwokoa,ila timu ngefungwa ingekuwa balaa kwake. Mashabiki na viongozi linapokuja swala la timu hizi za kariakoo hawataki mchezo!! Wanalala mbele na wewe.

Kuna ambao hawajanielewa point yangu kwa nini nimechanganya Simba na Yanga hapo.

Ni hivi; ule uchungu ambao timu za Simba na Yanga zinapopitia misukosuko kwa nini hawa watanzania hawana uchungu Kama huu linapokuja swala la kitaifa/nchi pale mambo ya hovyo yakifanyika?

Yale maandamano Tena ya bila kulazimishwa ya hawa watanzania katika hizi timu mbili kwa nini hatuoni yanajitokeza pale viongozi wakifanya mambo ya hovyo?

Ukiangalia juu juu unaweza sema Watanzania Wanapenda michezo ndiyo maana hutokea hayo mambo,ila ukweli watanzania Wanapenda Simba na Yanga na siyo michezo.

Hapa Tanzania Simba na Yanga ni dini kamili.

Watanzania Wanapenda Simba na Yanga kuliko wanavyoipenda nchi yao.

Mpaka najiuliza;Au CCM ndiyo wametuletea Simba na Yanga ili tuwe mazezeta,huku wao wanakula kiulaini na familia zao,sisi tuwe bize na dini hii ya Simba na Yanga?

Ukipita kwenye vijiwe vyote kuanzia vya kahawa,machinga,daladala hadi vya maofisini mjadala Ni Simba na Yanga tu .."Wewe mwaka huu huna timuuu".."Nakuambiaje kesho ukitetema nite mbwa nimekaa pale"..Ukiwa kwa mbali unaweza dhani wanajadili mambo ya maana labda maisha yamekuwa magumu lakini Kuna watu wanalamba asali na kula kwa urefu wa kamba kiulaini.Kumbe wapi,ni Simba na Yanga.

Alafu ni CCM Kama wameshatujulia, media houses zote kuanzia asubuhi hadi jioni vipindi vikubwa vinavyopewa airtime Ni michezo na zaidi Sana kuzijadili Simba na Yanga.Watu hawana mijadala na gharama za bando,mchele umefika buku 3,chapati jero, na maji ya mgao.Kwake Simba ikshinde Kisha akimbilie redioni kusikiliza uchambuzi wa Edo kumwembe pale wasafi FM.

Maumivu ya kuibisa bando ashayasahau. Anasahau Kama dakika 10 zilizopita alikuwa anajibizana na mheshimiwa Nape Twitter kuhusu kupungzwa kwa kifurushi alafu hakuna taarifa.Mtwnie tu basi tuandamane kupinga huu uonevu. Thubutuuu. Subiri Sasa Yanga wafungwe leo na club africaans ya Tunisia ndiyo utawajua wabongo akili zao. Dakika 0 wamejaa saramander tower wanamtaka engineer Hersi ajiuzulu. Ukiuliza nani aliwaambia waandamane hadi pale,jibu hakuna ila uchaguzi CCM wanaiba kweupe wote tumeweka masikio yetu majumbani kwetu tukifatilia maandamano Jf.Tukimsubiri Lisu aandamane kwa niaba yetu kudai katiba mpya.

Aliyetuletea dini ya Simba na Yanga ametuweza Sana watanzania.Nadhani hata maisha yawe magumu Kama ya Afganistan au tuwe na ukame kuliko Somalia na Ethiopia, CCM wanaweza kuongea na TFF wapange mechi ya dharura Kati ya Simba na Yanga, Kisha wakaongea na media houses zote wiki nzima mjadala uwe mpira ili wapoze malalamiko ya maumivu ya maisha magumu na ukame. Na hakuna kitu tutafanya.

Hii dini ya Simba na Yanga inadhoofisha Sana maisha ya watanzania kwa kweli.

NB: Huu siyo uzi wa michezo mods wasije kuhamisha
 
Mkuuu naungana na ww kwa zaidi ya 100000% hizi simba na yanga serkal ya ccm inafaidika nayo sana na hata baadhi ya matokeo huwa wao ndo wanayapanga ili kutaka mijadala mingi ya watz ihamie huko kwenye simba na yanga ...WATANZANIA TUSHITUKE TUNAFANYWA WAJINGA MA MAZEZETA TUSIOJITAMBUA.
 
Hamna kitu kinaniuma kama hili jambo
La watanzania kufanywa mazuzu
Kitu ambacho nafikiria kuja kufanya ni kujiondoa katika kundi la mazuzu na kujiunga na kundi la wajanja wachache kama ikishindikana nijaribu kuwabadili mtazamo hawa mazuzu
 
Mkuu mbona wenzetu walioendelea wanapenda mpira kuliko sisi hatufiki hata robo.

Huko ulaya wanaweza kucheza Norwich na derby countly mashabiki wanajaa koo, mechi za el classico zinazungumzwa wiki mbili kabla yaani wenzetu Wana uraibu vibaya mno.
 
Mkuu mbona wenzetu walioendelea wanapenda mpira kuliko sisi hatufiki hata robo
Huko ulaya wanaweza kucheza Norwich na derby countly mashabiki wanajaa koo, mechi za el classico zinazungumzwa wiki mbili kabla yaani wenzetu Wana uraibu vibaya mno
Umesema wao Wanapenda mpira.Yes uko sahihi.

Sisi tunapenda Simba na yanga,kwetu Simba na Yanga Ni dini kamili na ukileta ujuaji dhidi ya hizo timu wanakushambulia Kama nyuki.
 
Mkuu umeandika kwa uchungu sana na kwa hisia sana.
Utaeleweka na wachache sana.
Wapo bize vibanda umiza kuangalia gemu ya yanga na club africaan ya Tunisia.Mechi ikiisha wanahamia Twitter, Insta na Facebook kujibizana na wachambuzi uchwara. Kesho asubuhi na mapema watakuwa bize kufuatilia vipindi mbalimbali vya redio uchambuzi wa mechi ya Jana (leo) Kati ya yanga na club africaan).

Wataanza na Wasafi FM, kisha watahamia E fm, Clouds FM na kuanzia saa nane mchana Hadi saa 1 usiku watahamia u fm. Siku imeisha.

Huo muda wa kuchangia mada hii ili kujadili hatma yetu utatoka wapi mkuu?
 
Vipi na wewe dini yako ya TANZANIA imekusaidia nini?
Out of context.
Tafuta pesa hapa bongo hakuna mgao wa umeme wala maji!!!
Haya majenereta yanayosikia maduka ya nguo kariakoo kila siku nayasikia peke yangu?

Na mgao wa maji unaotangazwa kila siku hapa Dar ni uwongo? Huko mbezi Beach tu kwa waliozitafuta hizo pesa wakazipata wakina GENTAMYCINE juzi walilala bila kuoga,maji hayakutoka.
 
Back
Top Bottom