Dini ya Simba na Yanga inavyodhoofisha maisha ya Watanzania

Dini ya Simba na Yanga inavyodhoofisha maisha ya Watanzania

Michezo ni tasnia ambayo inatoa ajira za kutosha kupitia wachezaji, media, viongozi n.k Na ndio tasnia kubwa kwa sasa Tanzania sasa kwanini watu wasijadili?
Naona bado unakaza fuvu kaka.😁
 
Nakumbuka ile wiki tunajadili tozo za mabenki,kila mtu anashusha uzi
Ghafla likatokea sakata la masanja na katibu wake aise watu wakahamia huko wakasahau habari ya tozo
Baada ya usimba na uyanga inafuatia umbea
 
Too much is harmful..

#Ova
Vivyo hivyo na matatizo ya nchi yametofautiana kama dar kuna shida ya maji ila ukienda Arusha yapo. Sasa hapo unadhani mjadala utakuwa hot topic ikiwa kila mtu ana shida zake na vipaumbele vyake. Ila mpira ukifungwa dar lazima shabiki aliyeko kigoma aumie na ndio hapo kwanini unaona mpira unajadiliwa sana.
 
shida ukiandamana kuipinga serikali unapigwa risasi

ila ukiandamana kwa mambo ya simba na yanga hupigwi kwanza kwenye hayo maandamano na maaskari wanakuwemo
 
Inasikitisha na kushangaza sana.

Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru,nchi ambayo inasemekana tuna utajiri wa maji kuliko nchi yoyote ukanda huu wa maziwa makuu na pengine Afirka nzima,leo tunajadili swala la mgao wa maji.Tena Kuna wengine wameenda mbali zaidi kwa kuandika makala za kuwasifia Waislamu jinsi walivyo na ukarimu kiasi Cha nyumba zao za ibada kutoa maji ya bure.Yani Tanzania leo karne ya 21 tunalia kuhusu uhaba wa maji Safi ya kunywa?

Mwaka 2013 gazeti Moja maarufu liliandika makala "Sasa Tanzania uhaba wa umeme basi.Kuuza nje ya nchi jirani pia" .

Leo mwaka 2022 tukiwa tunaumaliza tukiwa tunakaribia 2023,miaka 10 baada ya kuisoma ile makala ya siasa ila bado umeme Ni kizungumkuti,majenereta yanaunguruma kila sehemu,umeme unakatika kila saa.

Katika Dunia hii ambayo matumizi ya internet yamepelekea kuajiri vijana wengi hapa nchini,maana ajira ni kitendawili,wao wanazidi kupunguza matumizi ya data(mb) kila siku na serikali hakuna kitu inafanya.Ukiuliza unajibiwa gharama za uendeshaji zimeongezeka. Siku hizi kila siku najiunga kifurushi cha wiki.Kila siku napata meseji za hongera tu kutoka Airtel na Voda. "Hongera, umefanikiwa kujiunga kifurushi cha wiki, umepata mb 350 kwa TSH 1000" baada ya masaa mawili bando limekata,unajiunga tena Kisha tena unaambiwa hongera!!!

Mambo mengi sana,ila Kuna kitu huwa najiuliza..

Hivi ile nguvu ya watanzania , mashabiki wa club ya Simba kuandamana pale uwanjani siku wanatoka droo na timu ya KMC (narudia siyo Simba walifungwa ila ilikuwa draw),ile wanaandamana kuanzia uwanjani tena usiku "hatumtaki Matola" inatoka wapi? Au yanga juzi tu hapo kutolewa club bingwa wakaangukia shirikisho,huko clabuni ilikuwa mshike mshike nusura kocha afukuzwe.Droo na Simba ikamwokoa,ila timu ngefungwa ingekuwa balaa kwake. Mashabiki na viongozi linapokuja swala la timu hizi za kariakoo hawataki mchezo!! Wanalala mbele na wewe.

Kuna ambao hawajanielewa point yangu kwa nini nimechanganya Simba na Yanga hapo.

Ni hivi; ule uchungu ambao timu za Simba na Yanga zinapopitia misukosuko kwa nini hawa watanzania hawana uchungu Kama huu linapokuja swala la kitaifa/nchi pale mambo ya hovyo yakifanyika?

Yale maandamano Tena ya bila kulazimishwa ya hawa watanzania katika hizi timu mbili kwa nini hatuoni yanajitokeza pale viongozi wakifanya mambo ya hovyo?

Ukiangalia juu juu unaweza sema Watanzania Wanapenda michezo ndiyo maana hutokea hayo mambo,ila ukweli watanzania Wanapenda Simba na Yanga na siyo michezo.

Hapa Tanzania Simba na Yanga ni dini kamili.

Watanzania Wanapenda Simba na Yanga kuliko wanavyoipenda nchi yao.

Mpaka najiuliza;Au CCM ndiyo wametuletea Simba na Yanga ili tuwe mazezeta,huku wao wanakula kiulaini na familia zao,sisi tuwe bize na dini hii ya Simba na Yanga?

Ukipita kwenye vijiwe vyote kuanzia vya kahawa,machinga,daladala hadi vya maofisini mjadala Ni Simba na Yanga tu .."Wewe mwaka huu huna timuuu".."Nakuambiaje kesho ukitetema nite mbwa nimekaa pale"..Ukiwa kwa mbali unaweza dhani wanajadili mambo ya maana labda maisha yamekuwa magumu lakini Kuna watu wanalamba asali na kula kwa urefu wa kamba kiulaini.Kumbe wapi,ni Simba na Yanga.

Alafu ni CCM Kama wameshatujulia, media houses zote kuanzia asubuhi hadi jioni vipindi vikubwa vinavyopewa airtime Ni michezo na zaidi Sana kuzijadili Simba na Yanga.Watu hawana mijadala na gharama za bando,mchele umefika buku 3,chapati jero, na maji ya mgao.Kwake Simba ikshinde Kisha akimbilie redioni kusikiliza uchambuzi wa Edo kumwembe pale wasafi FM.

Maumivu ya kuibisa bando ashayasahau. Anasahau Kama dakika 10 zilizopita alikuwa anajibizana na mheshimiwa Nape Twitter kuhusu kupungzwa kwa kifurushi alafu hakuna taarifa.Mtwnie tu basi tuandamane kupinga huu uonevu. Thubutuuu. Subiri Sasa Yanga wafungwe leo na club africaans ya Tunisia ndiyo utawajua wabongo akili zao. Dakika 0 wamejaa saramander tower wanamtaka engineer Hersi ajiuzulu. Ukiuliza nani aliwaambia waandamane hadi pale,jibu hakuna ila uchaguzi CCM wanaiba kweupe wote tumeweka masikio yetu majumbani kwetu tukifatilia maandamano Jf.Tukimsubiri Lisu aandamane kwa niaba yetu kudai katiba mpya.

Aliyetuletea dini ya Simba na Yanga ametuweza Sana watanzania.Nadhani hata maisha yawe magumu Kama ya Afganistan au tuwe na ukame kuliko Somalia na Ethiopia, CCM wanaweza kuongea na TFF wapange mechi ya dharura Kati ya Simba na Yanga, Kisha wakaongea na media houses zote wiki nzima mjadala uwe mpira ili wapoze malalamiko ya maumivu ya maisha magumu na ukame. Na hakuna kitu tutafanya.

Hii dini ya Simba na Yanga inadhoofisha Sana maisha ya watanzania kwa kweli.

NB: Huu siyo uzi wa michezo mods wasije kuhamisha
Mlete Mzungu , mlete Mayele
 
Ccm mjaishtukia chukueni mfano wa kenya kwa vijana wa genz ni kwamba mkiona hawa ndio wanufaika na nchi mfano nape mnadili naye kisaikolojia mfano biashara zake, kumtenga, kumpuuza n. K ili kuwapa fundisho ccm wote.
Yoyote atakaye jihusisha na ccm ni kufanya kama nilivyosema hii nguvu inaweza uwoga sababu ile kauli ya kuwa serikali ya ccm ina mkono mrefu ni uongo wakati wakifanya ujinga ni wachaxhe kuliko nguvu ya mwananchi
 
Umeongea point ya maana sana.

Kuna mdau mmoja alisema TISS watumie Simba na Yanga ku-divert mijadala mikubwa mabayo inaweza kutikisa nchi.

Sasa naanza kuamini
And this is now what is happening in Tanzania.

Inshu ya Nape na yule jamaa wa chadema aliyetekwa na kuteswa na polisi vimezimwa na inshu ya wazee wa yanga na mahakama.
 
Tafuteni pesa mpunguze kulalamika!!

Ukiwa na pesa hutasikia habari za mgao wa maji wala umeme
Kuwa na pesa sio kigezo cha serikali kutotimiza wajibu wake wa kutatua changamoto za wananchi wake.

Hata kina Bakhressa na Mo Dewji wana pesa lakini wanahitaji umeme na maji ya kutosha kuendesha viwanda vyao.

Na si jukumu lao kuzalisha umeme.

Ni jukumu la serikali.

Una elewa hilo?
 
Kuwa na pesa sio kigezo cha serikali kutotimiza wajibu wake wa kutatua changamoto za wananchi wake.

Hata kina Bakhressa na Mo Dewji wana pesa lakini wanahitaji umeme na maji ya kutosha kuendesha viwanda vyao.

Na si jukumu lao kuzalisha umeme.

Ni jukumu la serikali.

Una elewa hilo?
Kuna comments nimezisoma kwenye huu Uzi zinasikitisha na kumtia hasira kwakweli ikiwemo na ya huyo jamaa uliyomquote hapo

Yaani uzembe wa serikali kutoa huduma muhimu kama maji na umeme wa uhakika, yeye anakwambia eti sululisho lake ni wewe binafsi kutafuta hela serious? Sasa kama ni hivyo Kuna haja gani ya Mimi mwanainchi kulipa Kodi?......

Halafu kwanza majitu yenye mawazo ya kipuuzi kama hayo ndio huwa ni mafisadi na majizi.
 
Kuna comments nimezisoma kwenye huu Uzi zinasikitisha na kumtia hasira kwakweli ikiwemo na ya huyo jamaa uliyomquote hapo

Yaani uzembe wa serikali kutoa huduma muhimu kama maji na umeme wa uhakika, yeye anakwambia eti sululisho lake ni wewe binafsi kutafuta hela serious? Sasa kama ni hivyo Kuna haja gani ya Mimi mwanainchi kulipa Kodi?......

Halafu kwanza majitu yenye mawazo ya kipuuzi kama hayo ndio huwa ni mafisadi na majizi.
Kweli mkuu, Hao ndio majizi yenyewe na wahujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom