Dini ya Simba na Yanga inavyodhoofisha maisha ya Watanzania

niliona andiko linalofanana na hili juzi,nikatafakari sana kwakuwa na mm ni shabiki wa timu mojawapo kwakweli simba na yanga imepumbaza raia wengi sana wa taifa hili kiasi kwamba hali inazidi kuwa mbaya na hatuna habari sisi ni mayele,aziz ki.chama na phiri.Saa mbili asubuhi vijana wanadamkia kwenye vilinge vya magazeti wakizozana kuhusu simba na yanga,hao hao saa sita mchana utawakuta kwenye mabanda ya kubeti wakiendeleza mabishano yao mpk jioni.HII NI HATARI SANA KWAKWELI,
 
Hali ni mbaya sana.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kwani Tanzania ndo nchi pekee inayo jadili mpira tu au acheni watu wale raha yao kama wewe hupendi mpira tulia kwako
 
Kwani Tanzania ndo nchi pekee inayo jadili mpira tu au acheni watu wale raha yao kama wewe hupendi mpira tulia kwako
Kuna kujadili mpira na kujadili Simba na Yanga.Sisi tunajadili Simba na yanga.

Ni kama zimekuwa dini.
 
Kuna uwezekano mkubwa hukuwahi kulizingatia somo la ufahamu na ufupisho, wakati unasoma. Siyo kwa maelezo yote haya.
 
1-Kwahyo tukiacha kujadili simba na yanga ndio maendeleo yatakuja?
2-Kwani kuanzia tuanze kuzijadili simba na yanga miaka nenda rudi ni club gani imeleta ubingwa wa afrika?
3-simba na yanga zimejibrand miaka nenda rudi ndio maana leo hii zinazungumziwa sana. Kwanini na wengineo wasijibrand?
4-uwanja wa mkapa ukijaa full house sio mapato kwa serikali?
5-hivi vilabu viwili hujiulizi vimetoa ajira ngapi mpaka sasa je sio maendeleo?
 
Mkuu adriz kosa langu Mimi liko wapi hasa,?

Mvona mtu anatoka povu hivi?
 
Na siku hizi kukikucha tu asubuhi, huku kuna George Ambangile kule kuna Bin Kazumari yaani ni mwendo wa vipindi vya michezo asubuhi kabla hata ya watu kunywa chai
 
Picha nimepiga mtaa dukani hivi maeneo ya Yombo Vituka hiko kijiwe mijadala yao siku zote Simba na Yanga tu ,unaweza pita ukasikia watu wanavyobishana kwa nguvu kubwa utaweza kudhania kuna jambo muhimu sana linajadiliwa.
 
Picha nimepiga mtaa dukani hivi maeneo ya Yombo Vituka hiko kijiwe mijadala yao siku zote Simba na Yanga tu ,unaweza pita ukasikia watu wanavyobishana kwa nguvu kubwa utaweza kudhania kuna jambo muhimu sana linajadiliwa.View attachment 2405971
Ila mkuu huu ukuda sasa.πŸ˜‚πŸ˜‚

Poker njoo ushuhudie hii.Watu utadhani wanazindua mtaro happy chini Kumbe ukumbusho wa mechi ya shirikisho.
 
Serikali inabweteka kwa kuona wananchi mazombi kwa sababu ya kuyapa mgongo mambo ya msingi na kuwekeza muda mwingi katika kujadili Simba na Yanga , hata ukichunguza kwa bongo ni raia wachache sana wanaojua mambo muhimu kuhusu nchi yao na ulimwengu kwa ujumla hata kwa uchache .

Ndio maana vijiweni wakianza kuongolea habari muhimu utakuta chai nyingi kwa sababu watu wengi uelewa mdogo sana kuliko wanavyozijua na kufuatilia Simba na Yanga . Muhimu kubalance kama wenzetu Misri wale machizi mpira lakini kwenye masuala ya msingi hawayapa mgongo na huwakuti wakiuabudu mpira kama huku tunavyoabudu Simba na Yanga.
 
Michezo ni tasnia ambayo inatoa ajira za kutosha kupitia wachezaji, media, viongozi n.k Na ndio tasnia kubwa kwa sasa Tanzania sasa kwanini watu wasijadili?
 
Michezo inawaweka na kuwaleta watu karibu..

Siasa ya maendeleo inabagua kati ya masikini na tajiri..

Simba sc & Yanga sc wanawaunganisha masikini na matajiri, CHADEMA & Ccm, vipofu wanaona na viziwi wanasikia.

Ukiona mtu haongelei budle kupanda, mgawo wa maji / umeme ujue ameshakubaliana na matokeo.
 
Michezo ni tasnia ambayo inatoa ajira za kutosha kupitia wachezaji, media, viongozi n.k Na ndio tasnia kubwa kwa sasa Tanzania sasa kwanini watu wasijadili?
Naona bado unakaza fuvu kaka.😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…