Ma mimi nakujibu kama ifuatavyo
1. Kwanza MUNGU hana Dini, Dini zimeletwa na Binadamu, Musa hakuhubiri kuhusu Dini ya kiyahudi, Yesu hakuhubiri kuwa tuwe wakristo, Mohamad kidogo historia yake ndio inachanganya yeye kwenda na kurudi na kusema MUNGU kasema Dini ni uislamu, japo mbali na yeye hakuna shahidi wa kama ni kweli Mungu alihimiza Dini ni uislamu... Ukitizama vizuri Dini ni mapokeo ya utofauti wa kiimani kwa wanadamu wenyewe, ila kwa Mwenyezi MUNGU wote ni wake, na hana DINI. Na DINI haiwezi kukupeleka Peponi kamwe, bali ni matendo mema ya hapa Duniani.
2. Hajawaacha katika sintofahamu, kawaachia neno litakaloishi milele, katika Biblia kuna mstari unasema kama umpendi Jirani yako unayemuona, utampenda vipi MUNGU husiyemuona. Imani ni kuamini katika MUNGU uwepo wake na neno lake, ukiweza kufata neno kwa ufasaha utampendeza MUNGU, imani kali sio mapenzi ya Mungu. Unaweza kudhani Imani kali ndio wanaompendeza Mungu, lakini ukashangaa wanaoingia mbinguni wakawa wale watu uliowaona hawafai kwenye jamii. Hajatuacha tusumbuane kiimani bali anataka tujue ukweli juu yake, anataka tumtafute, tutafute neno lake la kweli basi hapo nasi tutakuwa pamoja nae.
3. Wapo mitume walioandika kwa mikono yao neno la MUNGU, na wapo ambao wanafuasi wao ndio waliandika neno la mungu. Mfano Suleimani (Solomon) inasemekana aliandika baadhi ya maandiko kwenye biblia wakati Yesu yeye maandiko yake yaliandikwa na wanafunzi wake waliokuwa wanatembea nae kila mahali.
4. Maisha ya hawa manabij hayakuweza kuandikwa yote tokea utotoni kwasababu manabii wengine walichaguliwa na MUNGU wakiwa tayari watu wazima mfano Ibrahim, hivyo maandiko ambayo yatakayo kuwa na mashiko ni kuanzia hapo alipochaguliwa na MUNGU. Na maandiko yote katika vitabu vya Dini yameanza kuandika mara moja pale MUNGU alivyoanza kugusa maisha ya hawa manabii. Mfano kina Jeremia, Samwel, Yusufu, Musa, Daudi, Samson, Isaka, Yosia, Yesu hawa maandiko yao yalianza kuandikwa tangu wakuwa wadogo au watoto na kuendelea kwa sababu MUNGU alianza kusema nao tangu wakiwa wadogo. Maandiko yako hayawezi kuandikwa wakati hukusemezana na MUNGU, ukianza kusemezana nae ndipo maandiko yanaanza kuandikwa.