Diploma ya clinical medicine: md miaka 5 au amo miaka 2—utachagua ipi?

Diploma ya clinical medicine: md miaka 5 au amo miaka 2—utachagua ipi?

Khaibar

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2025
Posts
1,803
Reaction score
4,693
Umemaliza kusoma diploma ya clinical medicine miaka walau mitatu iliyopita. Ukapiga kazi ukiwa na ndoto ya kuongeza elimu. Ila serikali wakarudisha advanced diploma of clinical medicine (AMO). Je, utachagua kwenda kusoma MD 5 years au AMO 2 years!?

Na ukijaribu kufuatilia maslahi unaambiwa AMO na MD wanapishana asilimia ndogo sana ya mshahara isiyozidi 25%.

Je, kimaslahi utaongeza kiwango gani cha elimu kutoka hapo!?
 
Jisikilize wewe. Unataka nini?
 
Bwana mdogo utakuwa hujui vizuri field ya MEDICINE.Ukiingia kazini hakuna cha zaidi huko ni kutumika mpaka ufe,Hiyo misifa na maujiko yote huwa yanabaki getini.

Acha kupoteza muda kasome physiotherapy ngazi ya degree.

Hakuna night shift muda huo wewe utakuwa unailoweka na kuichapa kwa mamsup.

Wagonjwa wako watakuwa ni wachache hakuna lawama huko.Ngangania MD uje kikurambe utaita maji mma.Ukienda md wewe na theator, theator na wewe calls haziishi na kulipwa majaaliwa.Saa nyingine upo juu ya kiuno unashangaa unapigiwa simu ukaassit huko kimeumana😄😄😄

Mshahara wa Physiotherapist ni karibu sawa na wa MD.

Muda wa ziada unafanya mambo yako na ukijikaza ukamiliki vifaa vyako unaweza ukawa unawafata wagonjwa wako majumbani unawafanyisha mazoezi kwa makubaliano ya pesa.Au ukafungua clinic yako private kwa huduma za mazoezi ya viungo.

Ukilamba shavu ukapata timu hizi za michezo ukawa daktari wao.Umeula wewe unapiga kotekote kama RONADO😄😄😄

Pia oportunities za kufundisha vyuo vya diploma bado zipo nyingi kwakua wataalamu wa physio ni wachache.

📌Bongo hakuna passion. Jiposition uenjoy maisha kaza fuvu uwehuke, achana na story za secondary za udaktari wa MD huko hakuna hela, hakuna kupumzika. Na ukiringa kwakuwa mpo wengi wenzako wanakula.
 
Maslahi unamaanisha mshahara wa serikali means lengo lako ni kuingia serikalini kama nimekuelewa.
Maana MD huyohuyo akiwa kwenye taasisi au miradi ya tafiti hashikiki hela zipo za kutosha na pia ana future potential ya kupata scholarship +sponsorship kusoma zaidi ndani/nje ya nchi hivyo kuwa na advantage kwenye soko la ajira la binafsi kama taasisi zinazotoa mikataba na kadhalika kama akispecialise kulingana na malengo yake na upepo wa soko la ajira.
Kama ishu ni mshahara wa serikali hata asiende kusoma,atafute kazi za miradi apate japo hata contract ya mwaka mmoja ndio itakuwa njia yake ya kuanzia baada ya hapo anaweza akadhani ndoto za kurudi shule kwa kuwa atapata fursa mbalimbali za kufanya kazi na national na international organizations ambazo pesa sio shida zao. Ila cha muhimu ajiposition kwa kuwa tayari kujifunza,kusoma vitu vipya na kuwa flexible kuandika proposals na mambo kama hayo.
Otherwise pia kama ni ishu ya kukimbizana na muda + kukwepa gharama kubwa ya kusoma +marejesho kausha damu ya helsb anaweza akasoma AMO 2 years akafanya kazi kwa kujifunza vitu mbalimbali akawa experienced zaidi(+5 years) then akahama kutoka clinical practices akaingia upande wa research akajiokotea hela kama mpumbavu 😂.
Ni hayo tu mkuu kwa maelezo mengine karibu kwa maswali zaidi.
 
Kibongo bongo kuongeza kiwango cha pesa kwa kusoma bora hata ufuge tu kuku, binafsi hapo nitasoma MD tu , kama ndoto yangu tu na sio kuongeza kipato
Yes uko sahihi mkuu. Ukipiga difference ya kwenda kusoma MD then uje ukatwe kausha damu yao kama ulichukua mkopo it's almost unarudi mule mule tu maana pia na makato ya PAYE yanaongezeka.
Kama lengo ni kuongeza maokoto Incase alishafungua biashara imesimama na inamlipa vizuri anataka kuexpand biashara achukue mkopo tu. Ila kupoteza 6 good years all in the name of kuongeza maslahi haisound gudi kabisa.
Angesema yeye
1. Anapenda tu kusoma sawa.
2. Anataka aweke historia ya kuwa daktari wa familia sawa.
3. Anaona future ya opportunities zenye hela kupitia MD/AMO pia nayo sawa kwa kuwa sio kila lengo ni la matokeo ya hapo hapo bali long term plan.
Ila kama ni chenchi hizo zinazobaki baada ya mapanga ya helsb ndugu hapo hakuna maisha.
Anyway ninawafahamu watu wenye diploma za afya wanapata mshahara gross wa daktari MD wao wanauchukua kama take home.
Hivyo fursa za maokoto mengi sio shule tu japo ni ya muhimu.
Ila kama ni future opportunies ambazo umeshaziona na unaweza kutengeneza network ya watu pia ukiwa unasoma mpaka unamaliza unaingia tu kwenye mfumo chap kwa haraka.
 
Umemaliza kusoma diploma ya clinical medicine miaka walau mitatu iliyopita. Ukapiga kazi ukiwa na ndoto ya kuongeza elimu. Ila serikali wakarudisha advanced diploma of clinical medicine (AMO). Je, utachagua kwenda kusoma MD 5 years au AMO 2 years!?

Na ukijaribu kufuatilia maslahi unaambiwa AMO na MD wanapishana asilimia ndogo sana ya mshahara isiyozidi 25%.

Je, kimaslahi utaongeza kiwango gani cha elimu kutoka hapo!?
AMO haipo niwdays ni Kusoma MD pekee au ukomee CO sema kada ya Afya imekaa kitapeli sana hii
 
Kilosa Health institute wanatoa. Na kuna vyuo viwili vya ziada pale pale Morogoro vinatoa. Lugalo nao wana mpango wa kuiweka mwaka huu kama sijakosea.
Mkuu AMO haiwezi kurudi hata wakifanya vipi sheria ya mwaka 2023 ya medical practitioner hairuhusu labda kama ukienda kusoma nje..
na usiwadanganye watu hata kidogo hakuna chuo kimerejesha AMO
 
Mkuu AMO haiwezi kurudi hata wakifanya vipi sheria ya mwaka 2023 ya medical practitioner hairuhusu labda kama ukienda kusoma nje..
na usiwadanganye watu hata kidogo hakuna chuo kimerejesha AMO
Bro nikuletee ushahidi!?? Usipinge vitu kama haujafanya uchunguzi. Nikuletee vyuo na requirements zake!?
AMO IMEREJESHWA MWAKA JANA SEPTEMBER BRO.
 
Back
Top Bottom