SoC04 Dira ya maendeleo ya taifa ndani ya miaka 20 ijayo

SoC04 Dira ya maendeleo ya taifa ndani ya miaka 20 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

sba

New Member
Joined
Jun 16, 2024
Posts
4
Reaction score
2
Kama taifa ili kukua kiuchumi yafuatayo yanaweza saidia kulifikisha taifa sehemu nzuri ya kimaendeleo
1.kuweka Dira ya pamoja kama taifa ambayo itaonesha mipango mikakati ya mda mrefu na mda mfupi kama taifa ni wapi tunapaswa kufika na vitu gani tunataka kuwa navyo

2.kuwekeza nguvu kwa vijana na makundi maalumu lengo likiwa ni kupunguza utegemezi kwa taifa kwani iwapo kutafanyika uwekezaji kwa vijana na watu wenye makundi maalumu kila mtanzania atakua na uwezo wa kujitegemea na hivo kuipunguzia mziho serikali

3.kupitia mpya Sera yetu ya ukusanyaji mapato kwani kodi nyingi zilizopo ni gandamizi zimelenga Kundi la watu wenye kipato cha juu na kuua mitaji ya watu wenye kipato cha chini na hivo kuongeza mzigo kwa serikali kutoa mahitaji na huduma za mhimu.

4.kuwekeza kwenye swala Zima la elimu ya ujasiriamali kwa watanzania wenye kupato cha chini lengo likiwa ni kutoa mwanya wa kuwaandaa watanzania kusoma nyakati na kubuni biashara inayo endana na wakati hivo kuwainua kiuchumi

5.kutengeneza mazingira ya miundo mbinu bora kama barabara ,huduma ya maji, huduma ya umeme, huduma ya afya ,huduma ya elimu kwa kufanya hivo kutachochea watu wengi kushiriki kwenye maendeleo ya uzalishaji mali na si kuwaza kwenye miundo mbinu bora

6.kuwawezesha watanzania wenye uhitaji wa mitaji ili kuweza kuendesha biashara zao. Kuna makundi ya watanzania wana malengo mazuri ya kibiashara kitu kinacho wafanya wasifanye biashara hiyo ni mitaji hivo serikali iliangalie na kuweza kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili kila mhitaji aweze kunufaika na uandaliwe mfumo mzuri wa utoaji wa mikopo hiyo

7. Wapewe nafasi wasomi kusimama kwenye taaluma zao kwani ukienda maeneo mengi wasomi wapo mitaani hawana kazi wanazo zifanya na badala yake kazi walizo pasta kufanywa nao zinafanywa na watu wasio kua na taaluma husika hivo kuchangia kudolola kwa mambo ya msingi

8. Kila mhimili wa serikali usimamie kazi na shughuli iliyo pangwa kusimamia kusiwepo na muingiliano wa majukumu kwani jambo hili hupelekea kazi za msingi na huduma ya msingi ambayo serikali inapaswa kufanya na kutoa kuto kutolewa kwa wakati

9. Wapewe Nafasi wazawa kwenye miradi ya serikali .kwa kufanya hivi kutahamasisha vijana na watu wenye taaluma fulani kuwa na uwezo wa kujiamini na hivo kupelekea kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye maendeleo ya taifa

10. Kuwepo na masomo ya uzalendo mashuleni na semina elekezi kwa vijana wa mitaani lengo likiwa ni kuwafanya vijana watambue ni majukumu gani na vitu gani taifa linawataka wao wachangie na hivo kutawapelekea kufanya kazi kwa waledi na kwa masilahi mapana ya taifa

Mwisho Naamini yakifanyiwa kazi mambo niliyo yasema hapo juu kama taifa tutakua sehemu fulani ya kimaendeleo
 
Upvote 3
Back
Top Bottom