Nikiwaza tu kifo najiuliza duniani ma
naangaikia nini? Ukisema ujikalie usiangaike na mikazi bado utachelewa kufa yaani dah
Yaani kufunikwa yale maudongo, bati zege hata ukigufukia huko huwezi pumua, unalala uko mwenyewe, huna wa kuongea nae, huli hunywi kifo nyie.
Kuna rafiki yangu binti alifariki mdogo kabisa alikuwa akiishi hapa mjini ana saloon yake, basi alivyoumwa akaenda kijijini kwao ndo akafia huko.
nikaja pata taarifa washazika muda mrefu, mama yake akaja huku mjini kufata vitu vya mwanae.
Hichi ndo kiliniuma zaidi, mama wa marehemu baada ya kujua mm ndo nilikuwa rafiki wa mwanae, akabeba simu ya marehemu akaniletea nitowe password, marehemu alikwisha niambia pesa yake anatunza kwenye simu.
Na alipokuwa anaumwa alikuwa akitoa hela kwa wakala anamtuma mtoto anamletea hela.
Nyie simu ya mtu iache tu, bibi wa watu hajui kutumia smartphone ndo ananiuliza kama ninajua password ya mwanae, tuliweka mwaka wake waaap, tukaweka password zote waapi.
Kifo ni fumbo angejua anakufa si angemwachia hata password mam yake? Dah kifo hakina huruma
Rip