TANZIA Director Khalfani afariki Dunia

TANZIA Director Khalfani afariki Dunia

Wakati anachipukia alikuwa anafanya kazi na Nisher
Poleni sana wafiwa.
 
Hii tasnia ina mauza uza sana wanalogana sana kuna director mmoja anaitwa jowzetz na yeye ali paralyse ikawa ana direct videos huku amelala ila sasa hivi ana nafuu yaani ukijisahau kufanya tambiko la mwaka wanakula kichwa faster hawachelewi.
 
Stroke ama kiharusi hutokea ghafla tu nafikiri ni kama fault tu hujitokeza mwilini na huwa mbaya zaidi kama itapiga kichwani maana hupasua mishipa midogo na kusababisha damu kuvilia kichwani.

Kuna sababu kuu mbili za kiharusi na zote huanzia ulipo ubongo...

1. Ischemic stroke: Chanzo cha aina hii ya kiharusi ni kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kupelekea ubongo kufa taratibu sababu ya ukosefu wa olsijeni na virutubisho.

2. Hemorrhagic stroke: Chanzo kikuu cha aina hii ya kiharusi ni kuvilia kwa damu kwenye ubongo kutokana na kupasuka kwa mishipa midogo ya damu, aina hii ya kiharusi inamuondoa mtu haraka mno...

I lost my aunt on early 2021 sababu ya same case ya stroke iliochapa kichwani. Haikumaliza week tulienda kuzika. Inaumiza sana!

Pole sana, huenda aunt alikuwa na shida haswa shinikizo kubwa la damu...
 
Huyu alipata stroke, ushawahi sikia stroke sasa huyu alipata. Inatokea kwa mtu yyte na ghafla sasa sababu kazisome popote. Ila stroke unaaweza kuwa na shughuli zako za kila siku, mawazo ghafla paap stroke.

Inakuja kwa ghafla lakini sababu huwa zipo mkuu...

Kuna makundi ya watu ambayo yapo kwenye risk ya kupigwa na kiharusi...

1. Watu wenye asili ya Afrika au wale walatino studies zinaomesha wanakumbwa sana na kiharudi...

2. Watu waiofanya mazoezi

3. Watu wenye matatizo ya shinikizo kubwa la damu, kisukari, rehamu nyingi mwilini

4. Watu wanaokunywa pombe, wenye maradhi kama Covid, HIV

5. Matumizi ya dawa kali kwa muda mrefu
 
Nikiwaza tu kifo najiuliza duniani ma

naangaikia nini? Ukisema ujikalie usiangaike na mikazi bado utachelewa kufa yaani dah

Yaani kufunikwa yale maudongo, bati zege hata ukigufukia huko huwezi pumua, unalala uko mwenyewe, huna wa kuongea nae, huli hunywi kifo nyie.

Kuna rafiki yangu binti alifariki mdogo kabisa alikuwa akiishi hapa mjini ana saloon yake, basi alivyoumwa akaenda kijijini kwao ndo akafia huko.

nikaja pata taarifa washazika muda mrefu, mama yake akaja huku mjini kufata vitu vya mwanae.

Hichi ndo kiliniuma zaidi, mama wa marehemu baada ya kujua mm ndo nilikuwa rafiki wa mwanae, akabeba simu ya marehemu akaniletea nitowe password, marehemu alikwisha niambia pesa yake anatunza kwenye simu.

Na alipokuwa anaumwa alikuwa akitoa hela kwa wakala anamtuma mtoto anamletea hela.

Nyie simu ya mtu iache tu, bibi wa watu hajui kutumia smartphone ndo ananiuliza kama ninajua password ya mwanae, tuliweka mwaka wake waaap, tukaweka password zote waapi.

Kifo ni fumbo angejua anakufa si angemwachia hata password mam yake? Dah kifo hakina huruma

Rip
 
Inakuja kwa ghafla lakini sababu huwa zipo mkuu...

Kuna makundi ya watu ambayo yapo kwenye risk ya kupigwa na kiharusi...

1. Watu wenye asili ya Afrika au wale walatino studies zinaomesha wanakumbwa sana na kiharudi...

2. Watu waiofanya mazoezi

3. Watu wenye matatizo ya shinikizo kubwa la damu, kisukari, rehamu nyingi mwilini

4. Watu wanaokunywa pombe, wenye maradhi kama Covid, HIV

5. Matumizi ya dawa kali kwa muda mrefu
Sijasema sababu hazipo nafahamu, na mimi si mgeni wa stroke kwa vijana, i do alot of charities nikiwa bongo i understand the problem.
Mfundshe mwamba niliyemquote
 
Sijasema sababu hazipo nafahamu, na mimi si mgeni wa stroke kwa vijana, i do alot of charities nikiwa bongo i understand the problem.
Mfundshe mwamba niliyemquote

Nimejazia ulipoishia mkuu, kama muendelezo wa comment yako kuleta muunganiko...
 
Back
Top Bottom