Habari wana jf, Poleni na harakari za hapa na pale za utafutaji, [emoji1666]
• Katika maisha, hapa duniani binadamu tunapita,
"R. I. P NiSher Davie" , sote tupo njia moja. Mwenyezi mungu akupunguzie Adhabu ya kifo huko uendako [emoji1545].
• Lakini kutokana na hili tukio la leo, nimejikuta najiuliza maswali machache :-
1.. Swali langu la kwanza : Kama kweli huyu ni Nabii (Geor Davie) je alishindwaje kutabiri kifo cha mtoto wake, ? ( au tuseme alijua kifo cha mtoto wake, lakini akaamua kukaa kimya ili kutimiza hatima ya mungu)?
2. Swali la pili : Kama kweli huyu ni nabii (Geor Davie) , je ameshindwaje kuwasiliana na mungu moja kwa moja kuhusu matatizo ya mtoto wake, ili ikiwezekana yatatuliwe mapema kabla ya umauti kumfikia NiSher ?
3. Swali la tatu : Sasa kama familia yao wanashindwa kuilinda kwa njia ya unabii wao, je mtu baki nitakaye enda kanisani kwake, nitaokolewa??
4. Swali la nne : Je tuwaite wapotoshaji !!, kama ni wapotoshaji kwa nini mamlaka zimekaa kimya?
5. Manabii wa zamani, mfano Eliya na Elisha walifanya matendo ya kimiujiza, ikiwa ni pamoja na kufufua watu, je nabii Geo davie atafufua mtoto wake?? [emoji52][emoji52].