Black Legend
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 174
- 301
Kupitia waziri wa utumishi na utawala bora, mh Mohamed Mchengerwa, serikali iliahidi kupandisha watumishi wake vyeo kwa kada mbalimbali, ikiwepo na kutenga bilioni 300 kwa ajili ya kulipa madai ya malimbikizo ya mishahara.
Lakini siku ya leo baada ya mishahara kutoka kumekuwa na vilio kila kona ya watumishi kutoona mabadiliko kama ahadi ya waziri ilivyokuwa. Suala hili limezua taharuki, ni vizuri serikali ikatolea ufafanuzi mapema kuhusu suala hili.