A
Anonymous
Guest
Wito kwa Uongozi wa DIT kuhusu usalama wa wanafunzi
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Kwanza (Bachelor) katika Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT). Ningependa kuwasilisha changamoto inayohusu usalama wa wanafunzi wanaotumia njia kati ya DIT Main Campus na jengo la nje la chuo, ambalo limetenganishwa na barabara kubwa ya Bibi Titi Mohamed Road.
Kwa muda sasa kumekuwa na ahadi ya ujenzi wa barabara ya juu (flyover/pedestrian bridge) ili kurahisisha wanafunzi kuvuka kwa usalama. Hata hivyo, hadi sasa utekelezaji wake haujaonekana, huku wanafunzi wakiendelea kuhatarisha maisha yao kila siku kwa kuvuka barabara yenye mzunguko mkubwa wa magari na pikipiki.
Swali la kujiuliza ni: Je, tunasubiri mpaka mwanafunzi apate ajali ndipo hatua zichukuliwe? Kinga ni bora kuliko tiba. Usalama wa maisha ya wanafunzi unapaswa kuwa kipaumbele kabla ya kutokea kwa tukio la kusikitisha.
Tunaona inawezekana kutekeleza suluhisho hili kama ilivyofanyika katika maeneo mengine kama Hospitali ya Aga Khan, ambako kuna njia ya juu inayowaunganisha watumiaji kati ya majengo bila kuhatarisha maisha yao.
Tunaiomba na kuishauri menejimenti ya DIT pamoja na wadau husika kulifanyia kazi suala hili kwa haraka. Ujenzi wa njia hiyo hautakuwa tu kuboresha miundombinu ya chuo, bali utakuwa uwekezaji katika usalama na ustawi wa wanafunzi.
Tunaomba hatua zichukuliwe sasa, si baada ya kutokea kwa ajali.