AKILI TATU
JF-Expert Member
- Feb 10, 2016
- 2,666
- 2,841
Ditopile ametoa kauli hiyo katika Msikiti wa Masjid Taqwa wakati akifungua Kongamano la Wanawake wa Kiislamu (JUWAKITA) Kata ya Kingale wilayani Kondoa ambapo amewataka kutumia kongamano hilo pia kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya awamu ya sita.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Ditopile amesema Wanawake wamekua ni nguzo kubwa kwenye jamii hivyo kupitia kongamano hilo anaamini jamii ya Kingale na Kondoa kwa ujumla itakwenda kunufaika na kubadilika.
" Niwapongeze sana JUWAKITA Kata ya Kingale kwa kongamano hili, tumezoea kuona JUWAKITA ngazi ya Wilaya, Mkoa au Taifa ndio wanafanya makongamano lakini nyinyi mmefanya ngazi ya Kata, niwapongeze sana na niwaahidi kuwaunga mkono katika kutatua changamoto ambazo mmeziainisha katika risala yenu.
Nyie ni mashahidi namna alivyoleta madarasa kila kona ya Nchi yetu na hapa Kingale ameleta pia, ameruhusu elimu bila malipo hadi kidato cha sita tumeona ameongeza bajeti ya Kilimo lengo lake ni kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta hii muhimu, hivyo ndugu zangu niwaombe tumuunge mkono Rais wetu," Amesema Ditopile.
Amesema kupitia kongamano hilo anaamini JUWAKITA Kata ya Kingale itakua mstari wa mbele katika kuhamasisha elimu kwa watoto wa kike katika Halmashauri ya Mji Kondoa.
" Nimeambiwa kupitia kongamano hili ambalo hufanyika kila mwaka limesaidia pia kumaliza changamoto ya kuvunjika kwa Ndoa, sasa niwaase sasa kupitia kongamano hili tukahamasishe elimu kwenye Wilaya yetu na hasa kwa watoto wetu wa kike," Amesema Mbunge Ditopile.