Diva, B12, na Mchomvu wapigwa chini Clouds

Diva, B12, na Mchomvu wapigwa chini Clouds

nawashauri waende mahakaman ili wawe watangazaji wa mahakama kama zitto alivyokuwa mbunge wa mahakama
 
Duh....so sad..............huwa nasikiliza xxl kwa ajili ya B twangala......anyway....nimeshaanza mazoezi kusikiliza na redio nyingine labda nitapata mbadala.

Kama jamaa anasema tu utovu wa nidhabu bila kuainisha...yaelekea ni serious ishu.......labda ametuachia room tujiongeze.....Let me tafakari......Mmmmmmmhhhhh...B12.....Mchomvu.....Diva.......may be wameonwa "wakirukiana" maeneo ya kazi.........na Fetty naye yuko wapi ili hisia zangu zi balance ?

Namuombea B12 arudishwe aise...mshikaji yupo cool sana.....
 
Kwa habari zilizotufikia ni kwamba watangazaji maarufu wa clouds fm diva,b12,na mchomvu wamesimamishwa kazi kwa muda husiyojulikana kwa utovu wa nidhamu,.kosa kubwa ni kushndwa kujumuhka na wenzao sikuku ya miaka 14 ya clouds fm,pamoja na makosa mbalimbali yanayowakabili hayo yamethbitishwa na mkurugenzi wa vipindi sebastian maganga

Du noma sana!!!
 
Unajiita Kaka halafu unaandika hivi!!??Spellings za aina gani hizo eti hara,twangara halafu huachi nafasi mmmh hata kuandika Kiswahili unashindwa.Hebu muwe mnaandika vizuri aibu eti..

mkuu.hawa wamezoea mmu na chit chat ndio andika yao hiyo.
 
Ha ha ha,nilimsikia huyu jamaa teja muuza bangi wa Keko. Kweli dakta isaac alikuwa anababaika kutaja jina kinega kila mara,lol!
Clouds noma sana nakumbuka J2 iliyopita hata Dr. Isaack aliogopa kutaja neno kinega mpaka kwanza akaomba ruhusa kwa ruge kulitaja hilo neno maana mtu teja aliyekuwa anamuhoji aka yake ni kinega,na akasema huyu jamaa jina lake flan aka yake ntakuja kukutajia baadae ndio akampigia simu ruge jamaa anaitwa kinega vp tulitaje hewani? Ruge akamwambia haina noma we litaje.
 
Hiyo ni sawa tu yaliyokuwa yanatokea kwa wenzao ndio nao wayajue kuwa akina Jide sio wehu! Kila la kheri Redio ya watu!
 
DIVA, B 12, MCHOMVU ‘OUT’ CLOUDS
by GLOBAL

Stori:- MUSA MATEJA

WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.

Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.

Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.

“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.

“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”

Source: GPL
DIVA, B 12, MCHOMVU ‘OUT’ CLOUDS – Global Publishers

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Kuna watu humu Jf ,kazi yao kukosoa lugha..,pu***fu zenu...badala ya kuchangia mada mnaleta Ujuaji kumbe hamjui chochote
 
naona hii habari nzuri kwa times fm haya times dili hilo mlichukua masoud kipanya,mkamchukua gadner sasa hao yatima wanakuja na yie tumieni fursa. kama clouds walivyokuwa wanasema
 
Back
Top Bottom