Diva hajitambui

Diva hajitambui

Mnao mshangaa Diva ni wajinga, wako watu wengi klko mnavyodhani hawujui wimbo wa taifa.
 
Acheni ujinga mbona philep mulugo alipokwenda south Africa alichemka na alikuwa waziri wa elimu ije kuwa huyu sio mbunge sio waziri sio diwani tatizo nn??
 
Hivi kwanini baadhi ya watu wanapenda kufikia hitimisho haraka haraka? Kwanini tumejenga mazoea ya kwamba tunayoyajua sisi, basi lazima na wengine wayajue kama sisi!!?? Kama wewe unajua kuimba wimbo wa Taifa, so what?!! Ni wewe! Tangu lini kwa mtu asiyejua wimbo wa Taifa (Tanzania) kwamba amekuwa hajitambui? Tena amekuwa mkweli kabisa kwamba haujui na haupendi! amesema wazi, nilidhani kwamba kwa kusema hayo ndio anajitambua, maana anajua asichojua na asichopenda. Labda kama kuna mengine, lakini kwa hili la Wimbo wa Taifa, hapana si haki kuhukumu. Mleta mada una mangapi huyajui maishani mwako ambayo wengine wanayajua, je na wewe kutuite hujitambui!! Hapana
Kitu usichokijua huwezi kusema hukipendi lakini pia kumbuka mtu huyu ni nini kwenye jamii ukijua Pata jibu ndio unihukumu pia, tunajifunza jambo moja tunapaswa kujipanga kama taifa uzarendo umepotea
 
hivi kwanini baadhi ya watu wanapenda kufikia hitimisho haraka haraka? Kwanini tumejenga mazoea ya kwamba tunayoyajua sisi, basi lazima na wengine wayajue kama sisi!!?? Kama wewe unajua kuimba wimbo wa taifa, so what?!! Ni wewe! Tangu lini kwa mtu asiyejua wimbo wa taifa (tanzania) kwamba amekuwa hajitambui? Tena amekuwa mkweli kabisa kwamba haujui na haupendi! Amesema wazi, nilidhani kwamba kwa kusema hayo ndio anajitambua, maana anajua asichojua na asichopenda. Labda kama kuna mengine, lakini kwa hili la wimbo wa taifa, hapana si haki kuhukumu. Mleta mada una mangapi huyajui maishani mwako ambayo wengine wanayajua, je na wewe kutuite hujitambui!! Hapana

tusitete uwongo hapa .. Huyo sijuwi nani radio presenter anaachaje kujuwa wimbo wa taifa hata kwa kuusikiliza tu ni muongo na kama amesoma bongo yetu hii mashuleni huwa tunauimba na bendera tulizichora....
 
Huyo nae yupo ktk kundi la frustrated group. Aged with no meaning to life.

Ni wa kusamehe tu.
 
Huyu mdada mashauzi mengi mpaka anaboa sana
 
DIVA HAJITAMBUI
Katika kipindi cha mkasi kilichoruka jana 21/12/2015 usiku Nilipigwa na mshangao wa kufa mtu pale muongoza kipindi Salama alipomuuliza Diva kama anaufahamu wimbo wa taifa akajibu kwa kifupi "siujui" salama hakuamini jibu hilo akamuanzishia wimbo huo ili kumsaidia hata kama alikuwa ameusahau akasema kwa msisitizo "kwanza huwa siupendi kabisa wimbo huo" kwanza nilijisikia ovyo na kuhisi kumchukia ghafla mtangazaji huyo wa clouds fm.

cc jamal malinzi
 
Hata mimi wimbo wa taifa unanikera Sana, eti mungu ibariki Afrika na viongozi wake. Hawa viongozi wezi wakubwa na mafisadi hawa ndio wabarikiwe? Big up Diva, we unaakili Sana. Umekataa kukaririshwa kama kasuku.
 
Acheni ujinga mbona philep mulugo alipokwenda south Africa alichemka na alikuwa waziri wa elimu ije kuwa huyu sio mbunge sio waziri sio diwani tatizo nn??

You guy can't differentiate! yule alikosea na inawezekana alikuwa haelewi, lakini huyu kasema haujui wimbo wa taifa na vilevile haupendi. sasa sijui wewe ulipokuwa shule unaimba wimbo wa taifa ulitaka uje uwe diwani au waziri! mi naona wewe ni mpumbavu kuliko hata huyo diva a.k.a chausiku
 
Huyu ni aina ya watu ambao hawataki hata watu wajue asili yake wapi, ndiyo maana hata lafidhi yake anataka awe kama nzungu. Aina yake ni watu wanaowakataa hata wazazi wao wakija kumtembelea mbele ya wenzie maana inawezekana alishawaambia walifariki. Hata jina lake nina wasiwasi nalo yawezekana diva sio jina lake la asili. huyu atakuwa anaitwa mkegani
 
Kipindi chake clouds ni kielelezo cha aina ya Redio hiyo. Ni upuuzi usio kifani. Mara ingine hucheka kwa kumuonea huruma. Angekuwa ana uwezo wa kujisikiliza angeweza kulia kwa aibu. Maskini majike ya aina hii hufanya chochote ili apate umaarufu. Alimualika Prezo akaishia kujitongozesha na kupigwa miti. Tch tch tch
 
Hata mimi wimbo wa taifa unanikera Sana, eti mungu ibariki Afrika na viongozi wake. Hawa viongozi wezi wakubwa na mafisadi hawa ndio wabarikiwe? Big up Diva, we unaakili Sana. Umekataa kukaririshwa kama kasuku.
Huupendi wimbo wa taifa kisa viongozi wetu ni wezi mafisadi!ipo tofauti kubwa kati ya vitambulisho vya taifa yaani BENDERA,WIMBO WA TAIFA,NGAO YA TAIFA,RAMANI YA NCHI YA TANZANIA.Vitu hivi ndio vinavyo itofautisha Tanzania na nchi zingine ni hivyo ndio vinajenga kitu kinachoitwa utaifa wetu,mtu yeyote anapodai kuchukia,kutopenda,kutothamini mtu huyo kwa jina la staha tunasema hajitambui kwa sababu huwezi kutukana tumbo lililokuzaa.
 
Invisible HUU UZI hautakiwi hapa hili si jukwaa la ujinga kuna majukwaa kibao huyu kakosea hebu uhamishe huu uzi au ufutwe
Two option
Ujinga hapa ni nini? ABCD ndio mwanzo wa alfabet na huwezi kudai unajua kusoma kisha ukadai huzijui hizo alfabet,mwanzo wa kila kitu kwa taifa lolote ni utambulisho wake yaani Bendera wimbo wa tafa na vitu vingine vinavyolitambulisha taifa husika kwa hiyo unapodai jukwaa hili linajadili mambo muhimu ya kisiasa siasa ipi isiyoanza na taifa tambua kuwa mada hii ni mtambuka inaweza kujadiliwa jukwaa lolote.
 
Last edited by a moderator:
10570236_459615814185584_1025461288_n.jpg

images
diva.JPG.jpeg

Huyu hapo kiongozi!! Ashukuru sana make up imemsaidia alikuwaga mkale sana!!
 
Mshenzi tu na hana maadili. Eti "Ohhh nimetolewa linyamatumboni nikaambiwa nikae miezi 6 bila kufanya sex, naimiss kweli sex." Watoto, vijana wanaangalia uchafu huu, eti uzungu. Anaongea upuuzi kisha "sorry daddy". Looser... Your parents must be very proud of you... poor parents.
 
Mleta mada nakukumbusha hapa tunajadili vitu muhimu kwa maslahi mapana ya taifa huwa hatupendi kujadili watu hasa ambao hawana madhara kwenye uchumi tafadhali usirudie tena kuleta hoja coco kama hii

Kila jambo ni muhimu kutokana na umeamua kuliona vipi!!

Ni lini tumewai kujadili mambo ya msingi ya kitaifa bila kuwataja watu?! Unaposema taifa unamaanisha watu, huyu naye ni mtu, na jambo alilolifanya ni jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linatoa picha mbaya ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Sote tunajua kuwa huyu bi dada ni public icon! Vipindi vyake vinasikilizwa na maelfu ya vijana wetu, kwa namna moja upuuzi ambao anaweza akaufanya huyu unaweza ukasambaa kama saratani hatari katika vichwa vya vijana wetu! Kwanini haujui wimbo wa taifa? Hakusoma shule za msingi na sekondari ambao wimbo huu uimbwa frequently?! Kama alipitia level hizo kwann asiujue?! Ni jeuri? Kiburi au ni nini? Na kama mtu anashindwa kuukariri wimbo huu, je masomo ilikuwaje😕 alifauru masomo yake vizuri kweli?! Na kwanini auchukie wimbo ambao ni national identity?! Kama haupendi wimbo je ana heshima na bendera ya taifa na nembo ya taifa?! Maana kushindwa kuyaeshimu hayo ni kosa, kisheria.....

Tanzania tunalea kizazi cha watu wapuuzi (wenye kupuuzia mambo ya msingi) na hii ni hatari kwa nchi yetu.
 
Huupendi wimbo wa taifa kisa viongozi wetu ni wezi mafisadi!ipo tofauti kubwa kati ya vitambulisho vya taifa yaani BENDERA,WIMBO WA TAIFA,NGAO YA TAIFA,RAMANI YA NCHI YA TANZANIA.Vitu hivi ndio vinavyo itofautisha Tanzania na nchi zingine ni hivyo ndio vinajenga kitu kinachoitwa utaifa wetu,mtu yeyote anapodai kuchukia,kutopenda,kutothamini mtu huyo kwa jina la staha tunasema hajitambui kwa sababu huwezi kutukana tumbo lililokuzaa.

Tumbo lililonizaa ndio bendera ya taifa? Kweli humu kuna watu wamepagawa. Kila mtu na msimamo wake kama mtu hana habari na wimbo au bendera ya taifa hakuna haja ya kumsakama. Kila mtu na maisha yake kwanza sio lazima kujua wimbo wa taifa unamaana gani.
 
Back
Top Bottom