Diva: Nyimbo zangu zinabaniwa sana kupigwa Redioni

Diva: Nyimbo zangu zinabaniwa sana kupigwa Redioni

Haaa haa haa pga kwanza ya sam misago na j de ndo zenu zfuatwe
 
Diva ni mwanamuziki mmoja mzuri sana kuwahi kutokea hapa tanzania...Sema ana ishu mbili tu ambazo akizisolve atakuwa juu kuliko hata v-money na Jide...Tatizo ni kuwa hajui kuimba na kutunga TU..........Akiweka sawa hayo tu......Aaaaaaah mbona mtapagawa
Hahaha jamani.
 
KUMBE MKUKI KWA NGURUWE, MMEANZA WENZENU WANAMALIZA SIONI TATIZO
 
13092350_1017963818284902_1208324435_n.jpg


Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema nyimbo zake pamoja na za mtangazaji mwenzake, Adam Mchomvu zinabaniwa na redio zingine, kitu ambacho anaona si sawa.

Anasema redio za mikoani ndizo zimekuwa zikiwapa support bila kujali kuwa wanatoka Clouds lakini redio karibu zote za Dar zimekuwa zikibania nyimbo zao.

Diva ambaye anaandaa album yake, The Life of The Diva, amesema kuwa hicho ni kitu ambacho angependa kuona kinafutika.

“Mimi naona wako so unprofessional, mbona sisi Clouds FM watu wazuri, mimi Sam Misago kaja, katoa wimbo ataitwa kwenye XXL nyimbo yake itachezwa, sisi mbona nyimbo zetu hamchezi?” amehoji Diva.

“Nilipeleka nyimbo East Africa Radio na ina haki zote za kuchezwa na haikuchezwa kwasababu natoka Clouds Media, kwanini wanatufanyia hivi? Hii ni biashara, wao wafanye kazi zao, na sisi tufanye kazi zetu lakini when it comes to music, sisi tunafanya serious kabisa,” amesisitiza.

Chanzo: Bongo 5
Mbona yeye na huyo Adam mchomvu Nyimbo Za Lady Jaydee hawapigi hapo Clouds kwanza anaimba nini heri mchomvu angalau
 
Back
Top Bottom