Why you guys, you never talk about SINGLE FATHERS… why
Kwanin? Tunawaonea sana hawa singo mazas na ukuti hata siku moja tukidiscus kuhusu singo fazas why
Jibu ni simple sana single father hawa exist in real life kwasababu kitendo cha mwanaume kutengana au kumpoteza mwanamke wake then akabakia na mtoto au watoto then huwa hana option ya kuishi pekee yake na watoto huwa anatafuta mwanamke wanaanzisha familia upya.
Wanawake on the other hand wanazaa na wanaume ambao hawajengi nao familia. Hebu nikuulize unamwitaje single father mwanaume ambaye anafamilia yake ila kazaa na binti fulani? Single kivipi na yupo ndani ya ndoa na ana mkewe?
Nakupa mfano mwingine,atokee binti amezaa na mwanaume wakashindwana,then huyu binti akaamua kukabidhi mtoto kwa baba yake halafu yeye akaenda anza mahusiano upya na mwanaume mwingine then wakafunga ndoa na wakapata watoto wengine,huyu mwanamke utamwitaje single mother?🤔 Wanaitwa masingle mother kwasababu wengi wanachukia ndoa,wakipata vihela vya kununua kitimoto kila weekend wanakuwa na dharau sana na wanaume na wanasema hawahitaji wanaume,sasa unawalinganishaje na wanaume?
Mifumo dume.. makosa mengi sana anapigwa nayo singo maza
Mfumo dume haujawahi wala hautawahi kuwa tatizo kwa mwanamke, mwanaume na jamii kwa ujumla.
Kinachoendelea kwasasa ni matokeo ya kukosekana mfumo dume ndani ya jamii.
Ni kukosa akili au elimu kama utadhania pale mwanamke anapoharibikiwa basi ni mwanaume kasabisha hiyo ni fikra potofu na ndio imetufikisha hapa.
wanawake wa sasa mnaishi mnavyojiskia ninyi sio mfumo dume unavyo taka.
Mfumo dume unataka mwanamke asijihusishe na mwanaume nje ya ridhaa ya wazazi ,je sio ninyi wanawake ndio kila siku mnapinga hilo na kutaka wanaume mjichagulie wenyewe,hapo mfumo dume ulikukandamiza wapi kama mwanamke na ulichagua mwenyewe,wakati mabibi za mabibi zako walichaguliwa wanaume wa kuishi nao ninyi mnakataa kuchaguliwa mbona mnaowachagua hamdumu nao?🤔
Mfumo dume unataka mwanamke akae ndani ya himaya ya mume wake na mwanaume asimamie majukumu 100% kwa mkewe,ninyi wanawake mkasema hapana na sisi tunataka tutoke tutafute. Kumbuka ukitoka nje unakuwa umeacha majukumu yako kama mke so utalazimika kuwajibika kwa 100% katika familia, na huu mtihani wengi unawashinda ndio maana mahusiano kwenu ni kama adhabu hamuelewi cha kufanya,mnabakia kuteseka na maisha ambayo wanaume hawakuwahi kuwaambia muyachague mitaka ninyi wenyewe,hapo mfumo dume umehusikaje kumuumiza mwanamke?
Ukifutilia watoto wa kiume wenye changamoto nyingi za kitabia ambao wanashindwa kuishi na wanawake ni zao la mama dhaifu au baba aliyetoka familia au ukoo wenye bibi dhaifu au babu dhaifu kwenye malezi. Ukifuatilia familia nyingi zenye wanaume imara katazame ukoo wake uone kama hautakutaka na mfumo dume.
Mfumo dume ni uongozi na direction,mfumo jike ni usimamizi na kufuata utaratibu. Sasa ukimuweka mwanamke kuwa ndie mkuu wa kaya utegemee nini kwa offsprings wake?