Hayo ni miongoni mwa maneno yaliyotamkwa na mkazi wa Kata ya Kibosho Mashariki, John Massawe, wakati akimweleza Diwani wa kata hiyo, Steven Massawe, hali ya taka zilizotupwa katika eneo la barabara ya Mweka, barabara inayotumiwa na wageni wanaposhuka kutoka Mlima Kilimanjaro.
John alizungumza hayo mara baada ya Diwani kufika eneo hilo kujionea mwenyewe hali halisi ya mazingira, ambapo taka zimerundikana kando ya barabara na katika maeneo yanayohusishwa na vyanzo vya maji vinavyotumiwa na wananchi.
Kwa John, tatizo hilo si suala la uchafu pekee.
Ni tishio kwa maji ambayo jamii inayatumia kila siku.
Akizungumza mbele ya Diwani, alisema eneo hilo linapita watoto wadogo wanaokwenda na kurudi shule, huku akieleza hofu kwamba hali hiyo inaweza kuwa chanzo cha magonjwa kwa wananchi endapo taka zitaendelea kutupwa karibu na vyanzo vya maji.
“Hawawatendei haki wananchi wako. Kuna watoto wadogo wanaenda shule. Kuna ambao hawaendi shule. Kipindupindu kitatokea kwetu kupitia watu tusiowajua. Tunafanyaje kuondoa hiki kitu?” alihoji John.