Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Naona baada ya Diwani kutenguliwa kila mtu anakuja na dhana yake na kuipa uhalali . WABONGO NI WAZUSHI JAMANI!!! Halafu ukiwa lofa unaweza kuamini kila UJUAJI unaoletwa humu.

Halafu akili za wengi zinatafsiri negatively kwa kila jambo. Yaani mtu hawezi kuiruhusu akili yake ikawaza kuwa ni mabadiliko ya kawaida baada ya Mhe Rais kubaini au kushauriwa kuwa hastahili pale kutokana na nafasi aliyokuwepo awali ya DGIS.
Kesho atakapopewa nafasi nyingine utasikia FIX za wana JF humu. Wengine watasema NILIJUA TU
 

Breaking: Rais Samia Atengua Uteuzi wa Kamishna Diwani​





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya, aliyemteua tarehe 03 Januari, 2023 kuwa Katibu Mkuu Ikulu

Amemteua Bw. Mululi Majula Mahendeka kujaza nafasi hiyo. Hapo awali Bw. Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.
 
Yaani nikutoe kwenye taasisi nyeti nije kukuweka kutongoza kasehemu ambako ndiko kanakoratibu mambo yangu. Yaani Washauri wa Rais sijui niwaambie nini. Yaani mtu demoted to such a junior position mnamuweka hapo kweli? Huyo kiutaratibu anapangiwa Ubalozi au kuwa nyumbani maana popote atakapopelekwa nchini ni Sawa na junior position kwake. Yaani kifupi Wakurugenzi wakitoka huko Idarani iwe kustaafu au kustaafishwa wanabaki nyumbani kwao au kupelekwa nje. No more.
 
Kwa jinsi Magufuli alivyokuwa nafikiri angetumia hicho kifungu kuwateua wapinzani waliokuwa wanamsumbua
Na kama wangegoma wangetiwa ndani kirahisi tu
 
Kiukweli alimkosea heshima Diwani Athuman! Hivi unajua majukumu ya katibu mkuu wa ikulu (Mnikulu)? Yani atoke kuwa DG akasimamie usafi kweli?
 
Diwani Athman atenguliwa ikulu.

View attachment 2469855

=========

Rais Samia ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa katibu Mkuu Ikulu

Aidha, Rais Samia amemteua Bw. Mululi Majula Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Nawaza tu Hata ningekuwa mm Diwani ningeshusha kofia chini maana naujuwa ukweli ambao wengi hawajuwi pale ikulu nitapotea kama alivyopotea Kijazi na siri naijuwa why nisiwe kama akina Mangula? Taifa lina majitu yana akili jamani.
 
Hawa wakuu wa hiki chombo miaka ya karibuni wamelambishwa sana sakafu sababu ya kutosimama kwenye msingi wa kile taasisi imepangiwa kufanya.

Wanafanya kazi kwa upepo wa wanasiasa, Mwisho wa siku zigo la misumari linawadondokea wao.
What he could have done better?
 
That was likely to happen.

Wala haishangazi, Athuman angepaswa kustaafu. Siyo kushushwa cheo kiasi kile ambapo sehemu ya maelekezo atapokea kutoka kwa aliyekuwa Junior kwake.
You haven't noticed trend ya utendaji wa mwenye nchi, he frustrates you kabla hajakumwaga ili ku justify
 
Nawaza tu Hata ningekuwa mm Diwani ningeshusha kofia chini maana naujuwa ukweli ambao wengi hawajuwi pale ikulu nitapotea kama alivyopotea Kijazi na siri naijuwa why nisiwe kama akina Mangula? Taifa lina majitu yana akili jamani.

Huyo kaondolewa baada ya kukataa kuonesha alipo Been Saanane maana kwenye majadiliano Hilo jambo limeongelewa Sana. Wamfukue alipo ili familia imzike kwa heshima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…