Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Mkuu

Hivi aliemshauri Hii move ni Nani!?

Aliemwambia toa diwani weka pale ana MALENGO gani haswa KWA awamu HII!!?

Yaani Lengo lake ni kujenga au kubomoa!?

Na kama ni kujenga ni kujenga mtu au Taifa!?

Kuna mtu anamdanganya mwenye mamlaka Ili kuleta mogogoro Fulani KWA MASLAHI Binafsi!!

Au ndio system inamchezesha michezo fulani MWENYE mamlaka na yeye anashindwa kuielewa!!?

Kwanza walimuingiza chaka kwenye kutangaza nia ya kugombea 2025,sasa wanamchanganyia mafaili kwenye uteuzi yaani teua tengua!!


Kuna mtu anafunga magoli dakika ya 90 halafu haonekani!!

Hivi niguse ninuke Yuko WAPI!!?

Simuoni siku hizi mitandaoni!
 
Kiuhalisia kuna kundi liko TISS linalomuingiza chaka mteuzi.

Kwanza kiutaratibu,alipaswa kumstaafisha kisha ndio ampatie uteuzi.

Halafu kiuhalisia hawa maafisa wa ngazi hiyo,huwa wanaishia kupelekwa ubalozini.

Hii maana yake ni kuwa Disconnect na mfumo.

Na kwa wale ambao huwa wamestaafu kisheria,huwa bado wanakuwa karibu na kitengovkama washauri.

Hata wateuzi mara nyingi hiwatumia pale wanapotaka kufanya verification ya jambo fulani nyeti.

Sasa mama yeye anatengua kwa nia fulani,halafu anakupeleka Ikulu ili utazamwe 24×7.

Huyu amelitambua hilo,na hii itamsumbua sana kichwa mteuzi.
 
Kwa sababu wengi wenu huwa mnawaza ndani ya Box...siwezi kukulaumu.

Ila sidhani kama unaelewa idadi ya vikao haramu,vinavyoitishwa mahoteli makubwa makubwa kila siku,wakati wengine tumelala!

Wewe unadhani unailelewa mitandao yote nchi hii?
 
Suala la peter wa royal tour, halihusiki kweli?
Kutenguliwa balozi wa USA, na yeye kuondolewa kwake madarakani, huenda walishindwa kumpa mama siri na malengo halisi ya peter!
Nchi ngumu sana hii.
Maswali ni mengi kuliko majibu
Hilo nalo neno!
Ila pia ujiulize balozi wetu nchini Austria kufariki kwa ajali akiwa anajiendesha mwenyewe!
 
Unajua maana ya safe house unaokotaokota vimaneno mtandaoni na kutungia stori
 
Hizo hisia zako tu na uzushi hakuna mwenye ubavu wa kukata uteuzi wa rais. Mkurugenzi wa usalama wa taifa ni mtu mdogo sana hawezi kuwa hata tone ndani ya maji ya bahari. Hii nchi ni zaidi ya mtu awaye yote. Vilevile kumbuka rais ni mtu mkubwa sana nchi hii kwa mujibu wa katiba na hawezi kutishwa wala kukwamisha na limkuu wa idara moja ndani ya nchi yenye idara nyingi. Rais ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, we mkuu wa idara moja tu ya usalama utatoa wapi kiburi? Hizo ni hisia zako tu rais anasimamia nchi yenye makomandoo na vyombo vingine vya siri. Sijui kama unaweza kukumbuka issue ya Imrani Kombe aliyekuwa naye mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Alitaka kutumia uchaga wake kumsaidi mchaga mwenzake Mrema apate urais alichinjwa mchana kweupe.

Hakuna anayeweza kukataa uteuzi wa Rais, ni majuzi tu aliyekuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Silvatory Mabeyo aliteuliwa baada tu ya kustaafu na hakukataa. Kwanza utaanzaje kukataa jambo la rais? Basi itakuwa hiyo nafasi aliipata isivyostahili, wale wanatakiwa wawe na utii wa hali ya juu usiotiwa shaka ya aina yoyote ndugu. Acha kumnenea uwongo.
 
Kukataa uteuzi wa Rais anajiweka ktk hatari kubwa sana, nakwakatiba hii ilivyompa Rais mamlaka wanaweza mchomekea kesi nzito akafie gereza la ukonga
Siyo rahisi kiivyo..

Unahisi Diwani anachukiwa na kila mtu, huko huko idarani na nje ya idarani CHAWA wake hawakosekani..

Pia kumpa kesi mtu kama diwani, yule siyo kama Freeman Mbowe au Lissu.
 
Kama aliweza kushughulikiwa Lt Gen Imran... atakuwa Kamishna wa Polisi
Kama ilikuwa collective responsibility ni rahisi Sana ukiwazacho!

Lakini kama system into blocks and divided into emotions hard to happen na kama it happen it will bring chaos in the system !!

Kiasi Kwamba hata chupi za chumbani za baba na Mama zitaletwa sebuleni for the kids to see!!

Personal view after digestion of the stuff!
 
Kukataa uteuzi siyo kumtunishia misuli Rais!

Kuukataa uteuzi ni haki ya kikatiba!

Kuteuliwa huwa sio amri bali utashi.

Hata Raphael Chegeni aliukataa uteuzi.

Hata aliewahi kuwa mkuu wa mkoa wa mwanza aliwahi kuukataa uteuzi wa JPM.

Halafu uelewe kwamba sio kila mtu yuko individual.

Watu huitana vikao kabla ya maamuzi kama hayo!

Usijenge dhana isiyokuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…