Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Lile jasusi sio la kubeza manake lilisema litashinda dakika ya tisini. Naona kama ni lishindi lile kwa yaliyotokea au ww mkuu unaonaje!??
 
Suala la peter wa royal tour, halihusiki kweli?
Kutenguliwa balozi wa USA, na yeye kuondolewa kwake madarakani, huenda walishindwa kumpa mama siri na malengo halisi ya peter!
Nchi ngumu sana hii.
Maswali ni mengi kuliko majibu
Siyo peter ni peral we vipi ama hukumsikia mama kwenye movie unasound kibongo bongo
 
Tafuta hela kijana haya makasiriko sio wewe kabisa
 
Lile jasusi sio la kubeza manake lilisema litashinda dakika ya tisini. Naona kama ni lishindi lile kwa yaliyotokea au ww mkuu unaonaje!??
Hamna alichoshinda labda kushindia kuwalisha sungura wake mchicha nyumbani kwake 🤣🤣🤣!

Ushindi ilitakiwa apindue meza kama M7 wa Uganda.
 
Akili za kuambiwa, Changanya na zako-Mzee mmoja aliwahi Sema.
 
Nchi hii, watu huwa wanapenda kukuza sana mambo. Utasikia, ooh mkurugenzi wa Taifa ana siri zote nzito za nchi hii! Upuuzi mtupu.

Yaani mtu mwenye akili timamu kabisa uamini kuwa mkurugenzi wa usalama wa Taifa anajua siri nyingi nzito za Taifa kumzidi Rais.

Mkurugenzi wa usalama wa Taifa amepewa kakitengo tu ndani ya usalama wa nchi. Na anaripoti kwa Rais. Kuna IGP, naye ana kitengo cha ujasusi, naye anaripoti kwa Rais. Kuna CDF, naye ana kitengo cha ujasusi, naye anaripoti kwa Rais.

Lakini wapo pia watu maalum wanaofanya ujasusi wasioripoti kwa IGP, kwa CDF au Mkurugenzi wa TISS, ambao wanaripoti moja kwa moja kwa Rais. Hata mkurugenzi wa TISS, IGP na CDF wanafanyiwa ujasusi pia ili kuwa na uhakika kuwa wakati wote wapo kwenye mstari.

Halafu mtu anatoka huko anaropoka eti mkurugenzi wa TISS ana siri nyingi, kama vile ana uelewa wa mambo mengi kumzidi Rais ambaye anapokea taarifa mbalimbali toka kwa vyombo vingi vya ulinzi na usalama.

Achaneni na hekaya za Abunuasi kusema kwamba Diwani amekataa uteuzi wa Rais. Hayo ni maneno ya watu wa vijiweni wasio hata na ABC ya hiyo idara aliyokuwa akiiongoza Diwani. Kwa kadiri ya kiapo cha hawa watu na kwa nature ya kazi yao, hawaruhusiwi kukataa order yoyote toka kwa Rais. Akifanya hivyo ni sawa na uhaini.

Huyu bila shaka kuna makosa amefanya, akashushwa na kupelekwa karibu ili achunguzwe zaidi mienendo yake. Huenda ndani ya muda mfupi wa uteuzi kuna taarifa mbaya zaidi zimemfikia mkuu wa nchi kiasi cha kuonekana kuwa hafai hata kwa nafasi hiyo au pengine anafikiriwa kwa nafasi tofauti na hiyo.
 
Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu!

Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake!

Diwani sio Kabudi au Lukuvi!

Diwani ndie afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili .....

Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!

Pia ieleweke yeye ndie alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia.[emoji2827]
 
Kukataa uteuzi wa Rais anajiweka ktk hatari kubwa sana, nakwakatiba hii ilivyompa Rais mamlaka wanaweza mchomekea kesi nzito akafie gereza la ukonga
Alikuwa DG wa TISS kwa siku 1000 na ushee anajua pa kuingilia na pa kutokea... ANAJIAMINI!

Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu!

Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake!

Diwani sio Kabudi au Lukuvi!

Diwani ndie afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili .....

Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!

Pia ieleweke yeye ndie alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia.
 
Katiba ndivyo inavyosema?

Diwani sio wa kwanza kuukataa uteuzi!

Hata Chegeni pia aliukataa uteuzi wa kuwa RC.
Chegeni alikuwa Askari? Tofautisheni kati ya kuteuliwa na Rais, na kuteuliwa na Amiri Jeshi Mkuu. Tofautisheni mambo ya hiari na mambo ya amri.

Teuzi zote ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama ni amri.
 
Ahaaahhahahahahah huyo jamaa nilikuwaga sjamuelewa kwenye kale kamsemo ka niguse ninuke..na dakika ya 89..

Alipofariki ndipo nikaelewa mnuko..

Wabililah wautaufiq waminqum
 
Uko sahihi kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…