PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Achaneni na uongo uongo na kupamba maneno ya uchonganishi nyie.Ameukataa uteuzi na sio kutenguliwa!
Niliandika hapa juzi!Iweje Mkurugenzi TISS kupelekwa Ikulu!
Diwani ni mwenye kujitambua,ameukataa uteuzi ule.
Diwani ana uzoefu na serikali zaidi ya Nne za CCM.
Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu!
Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake!
Diwani sio Kabudi au Lukuvi!
Diwani ndie afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili .....
Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!
Pia ieleweke yeye ndie alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia.
Yote yaliyojiri katikati hapo...
Ni Diwani ndie anaeyajua!
Diwani sio wa kubezwa!
Diwani anastahili kupewa ulinzi kwa usalama wake!
Kitendo cha kuikataa safe house,ina maana amekataa ku surrender mawasiliano yake yote.
Ili kuanza kutumia mapya ya Safe House!
Na mengi bado yanakuja,maana kadri inavyonyesha,ndio matobo yanavyozidi kuonekana.
"Rais Samia atengua uteuzi wa Diwani Athumani"
By Bakari Kiango
(Mwananchinewspaper)
Alhamisi,05/01/2023.
Dar es Salaam.
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Ikulu, Kamishna Diwani Athumani uliodumu kwa siku mbili baada ya kuteuliwa akitokea Idara ya Usalama TISS.
Kamishna Diwani aliteuliwa Januari 3, 2023 kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu, akitokea katika wadhifa wa Mkurungezi Mkuu wa TISS, nafasi aliyohudumu kwa siku 1,210 tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Januari 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa nafasi ya Diwani imechukuliwa na Mululi Mahendeka aliyekuwa ofisa mwandimizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.
Alamsikhi
10101.
Eti amekataa uteuzi, mbona alipoondolewa kutoka DCI kwenda kuwa RAS hakukataa?