View attachment 2469861
Kawaida wakurugenzi hawa wakishaondolewa katika nafasi zao, huwa wanapelekwa ubalozini huko Canada, Brazili ili kutoa nafasi kwa ajaye kufanya kazi kwa umakini. Imagine Diwani aanze kuripoti kwa huyu mpya, lazima kutakuwa na hali fulani hivi.
Halafu huwezi kujua ameichukuliaje issue ya kuondolewa halafu unamuweka jikoni kwako panapopikwa chakula
I said.
Huko ubalozini unazani ana ripoti mbinguni??
Sio kila anae ondolewa ktk teuzi amemgomea Mh.
Kumgomea ni kosa la uhaini... Uhaini sio kupindua nchi pekee...
Fahamu tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake
Fahamu tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake
Uhaini ni kosa la jinai, kwa tafsiri nyepesi ina maana kwamba ni kosa kubwa ambalo mtu analifanya dhidi ya nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti, mfano wa watu wasaliti wanaojulikana duniani ni Yuda ambaye kidini alimsaliti Yesu, mwingine ni Benedict Anold huyu jamaa aliisaliti nchi yake ya Marekani dhidi ya Mbritishi, wengine ni Vidkun Quisling, na Marshall Pe’tain.
Kisheria ukubwa wa kosa hupimwa kwa adhabu yake, kosa likiwa kubwa mtuhumiwa hutumikia adhabu kubwa vivyo hivyo kosa likiwa dogo mtuhumiwa huadhibiwa kiasi.
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.
Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais. kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini
Aidha ifahamike kuwa kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.
Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya jinai dhidi ya nchi yetu.
Iwe kwa faida yako na wengine kama wewe ambao una hisi kila mtu akitenguliwa basi amekataa nafasi hiyo...
Jitahidi kusoma kwa makini kila mstali uweze kupata uelewa...
Wenzio wakina Mbowe, Lema nk walipanda ndege kutoka dar kwenda ktk sherehe mwanza kwa Magufuli, walikuwa wana elewa haya. Wangeweza kusema wana umwa lakini ndio hivyo haikuwezekana