MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.
Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.
Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.
Kufukuzwa kwa Diwani Isaya Doita kunafanya awe Diwani wa 14 katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA aliyeondoka CHADEMA baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:
Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Barua ya kumvua uanachama
Video ya tuhuma kwa Godbless Lema
Video ya tuhuma kwa Godbless Lema