Kilemakyaaro
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 5,051
- 5,104
LEMA ANA U BILLIONAIRE GANI HASA? BAKHESA MWENYEWE NA UTAJIRI WOTE ULE BADO HAJAFIKIA U BILLIONAIRE.
Akili maandazi sio tusi. Kuhusu kusema,yeye ni diwani anapo pa kuzungimzia yote ya moyoni hivyo kuja kusemea kwenye press ni uhuni ili ufukuzwe upate milage ya kisiasa.Hivi ukimtukana mtu usiyemjua unapata faida gani? Unajisikia kama kambabe fulani au siyo? Bila shaka wewe ni mashabiki na sio mwanachama wa Chadema.
Huyu unaemshambulia amesema hadharani kinachomkera katika chama chake kwa sababu anaona kinakoelekea si kizuri. Kwa kufanya hivyo amekipa fursa ya kuchunguza yale anayodai na kujirekebisha kama inabidi. Au mlitaka azungumzie kwenye vilabu vya pombe ambako ndiko kuna wapiga kura wengi?
Amandla....
Barua ya kufukuzwa (iliyoandikwa na Katibu Kata wake) imetoka baada ya video ya yeye kuwasema vibaya viongozi wa Chadema Arusha ( hakumsema Lema peke yake) kusambaa kwenye social media. Sasa mtu yeyote ataviunganisha hivyo vitu. Kama kuna sababu nyingine basi waliomfukuza wataweza kuitoa. Mimi sio mwanachama wa Chadema kwa hiyo siwezi kujua kwa uhakika kama aliwahi kuwasilisha tuhuma zake kwenye vikao vya kilichokuwa chama chake. Labda wewe utuambie. Kufukuzana ovyo ndiko kulikoonyesha kuwa CUF kuna matatizo. Nisingependa Chadema nao watumbukie huko huko. Lakini mwenye macho haambiwi tazama.Ajibiwe wapi? Mm nimekuuliza umeona sababu za kufukuzwa kwenye barua yake? Ni tuhuma zipi ambazo ametoa? Ni taratibu zipi za kichama ametumia kuwasilisha tuhuma, kama unavyoziita, halafu akapuuzwa? Tangu lini mhubi kwenye chama akitimuliwa inaitwa kuwa ni chama kimevurugika?
Taratibu za kukosoana ziko kikatiba na zinapaswa kufuatwa.
Hivi huko ccm kiongozi mmoja anaweza itisha press na kumtuhumu wa juu yake badala ya vikao?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ambavyo wao wanakosoa, wao pia walipaswa wawe tayari kukosolewa.
Kwa hiyo " akili maandazi" ni sifa nzuri?Akili maandazi sio tusi. Kuhusu kusema,yeye ni diwani anapo pa kuzungimzia yote ya moyoni hivyo kuja kusemea kwenye press ni uhuni ili ufukuzwe upate milage ya kisiasa.
Huku mtaani ni kwa wale wasio na vikao rasmi vya kuzungumzia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Walipomkaribisha Lowassa ambaye walituaminisha ni fisadi papa kwa zaidi ya miaka 8 na kuanza kumuimbia mapambio ya Lowassa Mabadiliko, wenye fikra kubwa tulijua CHADEMA imepoteza dira/malengo!CDM yangu sijui imepatwa na nini kwani Lema ni Mungu asituhumiwe? CDM inazidi kuondoka kwenye lengo na hii ni furaha na shangwe kwa mahasimu wetu....
Makosa ya Kangi ni yapi?Nimemsikia, alichosema ni ukweli mtupu na ukweli mchungu ambao kila uchao ninaendelea kuuzungumza hadi October 2020, haya maneno huyu diwani kayasema jana, leo katimuliwa na kikao gani?.
Kuna utaratibu wa mashitaka kwa mujibu wa katiba ya Chadema, umefutwa?. Hii isije kuwa ni kama kutimuliwa kwa Zitto na Shonza, ni kumpiga teke chura.. Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
Huyu jamaa tayari ameisha jitambua, yuko njia kuu.
Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?
Wanabodi. Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja? Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu hilo...www.jamiiforums.com
P
Kama Magu anavyoteka na kuuwa akina Azory?Wazee wa Demokrasia haoooooo. Sasa piga mahesabu wakishika nchi watafanya nini.
Kama wamekoselewa wamefukuza mtu je wakishika nchi halafu ukawakoso si utaishia kunyongwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Lowasa ni mwanachama wa CHADEMA?Hahahaha ziko kikatiba gani hahahaha kwanini Lema hakufukuzwa alipo mkosoa Lowasa mitandaoni? Hahahaha
Sent from my iPhone using Tapatalk
Viongozi wengi wa kisiasa hasa katika vyama vyetu vya upinzani hawana busara!Huu ni ujinga uliopitiliza. Chama kilichokomaa ni lazima kikubali kukosolewa. Kwa kumfukuza, kinathibitisha alichosema kuwa Arusha kweli kuna tatizo. Walitakiwa kumshukuru kwa kuwa muwazi na kufanyia kazi tuhuma zake. Uamuzi wa kumfukuza mtu uanachama hautakiwi kufanywa kirahisi rahisi hivi.
Amandla
Hawawezi kukuelewa kwa sababu ni kati ya kundi ambalo political blind follower!Mbona huyo huyo Lema Kuna kipindi alimkosoa mhe. Lowassa kwa kutumia social network wakati lowassa yupo chama Cha chadema alipoenda kukutana na Magufuli ikulu mbona hakutumia vikao vya chama na Wala hakuchukuliwa hatua zozote na chama chake.Tusipende kutanguliza mahaba kwenye mambo ya msingi.
UKWELI GANI WAKATI AMESHAFIKA BEI! MA CCM ACHENI UZUZU!
CHADEMA hakuna njia nyingine zaidi ya kutimuana, hata vikao vya majadiliano hakuna... Kwa nini msiwe mnajipa nafasi kabla ya kutimuana.!!
DuhKwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, kikao cha shina/kata kina uwezo wa kumfukuza uanachama mwanachama yoyote!
This is very detrimental.
Jamani mbona Diwani alikuwa anawaambia ukweli viongozi wake, kumbe hawapendi kuambiwa ukweli ila wao wanapenda kuwaambia wengine ukweli, hakuna demokrasia hapo bali ni changa la macho tu. Chadema kama FIFA ukipeleka kesi Mahakamani kukishitaki chama basi wewe si mwanachama tena, kuna demokrasia hapo...!!!!Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.
Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.
Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.
Kufukuzwa kwa Diwani Isaya Doita kunafanya awe Diwani wa 14 katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA aliyeondoka CHADEMA baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:
Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake
Barua ya kumvua uanachama
Video ya tuhuma kwa Godbless Lema
Kama Magu anavyoteka na kuuwa akina Azory?