1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Nipo upande wa kuunga mkono baadhi ya mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu hii ya Tano.
Mfano kufaulu kwenye vita kubwa kama ya kusambaratisha ugaidi uliokua umejikita kuanzia chini mpaka juu. Fedha nyingi haramu ziliingizwa na magaidi kwenye nchi za Afrika ikiwemo Afrika mashariki.
Awamu hii imefanya vizuri kupunguza au kuzuia ugaidi na magaidi kuingiza fedha haramu.
Kujenga miundo mbinu naunga mkono serikali.
Naunga mkono suala Kupambana na rushwa iliyokua imejikita kwenye wizara mbalimbali na mawaziri kujikusanyia Mali kama alivyowahi kusema Del Filikunjombe(RIP).
Kutokomeza uhalifu mkubwa wa Kisiasa na kiuchumi.
Wanasiasa wengi waligauka kuwa wahalifu kwa nia ya kugombania madaraka. Wapinzani walikua wanatumia damu za watoto wa maskini kujipatia umaarufu kupitia maandamano ya hovyo hovyo. Chama tawala nao walitumia rushwa na ushirikina kama nyenzo ya kujikita madarakani.
Kukomesha utoto wa wabunge kuzomea zomea badala ya hoja kama Enzi za Dr. Slaa na Makame Rashidi.
Naunga mkono Kukomeshwa maandamano yasiyo na tija kwa Taifa.
Sent using Jamii Forums mobile app