Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

wewe uko upande upi kati ya serikalini au upinzani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nipo upande wa kuunga mkono baadhi ya mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu hii ya Tano.
Mfano kufaulu kwenye vita kubwa kama ya kusambaratisha ugaidi uliokua umejikita kuanzia chini mpaka juu. Fedha nyingi haramu ziliingizwa na magaidi kwenye nchi za Afrika ikiwemo Afrika mashariki.
Awamu hii imefanya vizuri kupunguza au kuzuia ugaidi na magaidi kuingiza fedha haramu.

Kujenga miundo mbinu naunga mkono serikali.
Naunga mkono suala Kupambana na rushwa iliyokua imejikita kwenye wizara mbalimbali na mawaziri kujikusanyia Mali kama alivyowahi kusema Del Filikunjombe(RIP).

Kutokomeza uhalifu mkubwa wa Kisiasa na kiuchumi.
Wanasiasa wengi waligauka kuwa wahalifu kwa nia ya kugombania madaraka. Wapinzani walikua wanatumia damu za watoto wa maskini kujipatia umaarufu kupitia maandamano ya hovyo hovyo. Chama tawala nao walitumia rushwa na ushirikina kama nyenzo ya kujikita madarakani.

Kukomesha utoto wa wabunge kuzomea zomea badala ya hoja kama Enzi za Dr. Slaa na Makame Rashidi.

Naunga mkono Kukomeshwa maandamano yasiyo na tija kwa Taifa.

Umeongea point kubwa Sana.
 
Hiyo haijathibitishwa sehemu yoyote, ni tetesi tu na speculations za watu. Siwezi kuongelea tetesi au conspiracy theories.
mm nasema kwa uhakika kabisa TUNDU LISU alimiminiwa risasi kwa order ya mkubwa baada ya kuonekana anampinga. ben sananane, mawazo, gwanda, kagoye na wengine wengi (rejea maneno ya pr. kabudi akiwa BBC house)
 
Hiyo haijathibitishwa sehemu yoyote, ni tetesi tu na speculations za watu. Siwezi kuongelea tetesi au conspiracy theories.
bilashaka wewe ni mamini wa dini hizi za mapoke (uislam/ukristo) nani amethibitisha uwepo wa mungu hadi uende KUABUDU?
 
Jamani mbona Diwani alikuwa anawaambia ukweli viongozi wake, kumbe hawapendi kuambiwa ukweli ila wao wanapenda kuwaambia wengine ukweli, hakuna demokrasia hapo bali ni changa la macho tu. Chadema kama FIFA ukipeleka kesi Mahakamani kukishitaki chama basi wewe si mwanachama tena, kuna demokrasia hapo...!!!!
Ukweli gani aliowaambia? Tuhuma za uowongana chuki ndo wewe unaziita ukweli? Kukosa hekima, utii na nidhamu? Hayo Ni maadili gani? Hakuna taasisi isiyo na maadili na miiko yake. Viongozi lazima waheshimiwe. Hkuku kwetu kunamiiko ya maadili na uongizi. Huyo anastahili adhabu hiyo aliyopata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.

Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.

Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.

Kufukuzwa kwa Diwani Isaya Doita kunafanya awe Diwani wa 14 katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA aliyeondoka CHADEMA baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:

Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Barua ya kumvua uanachama
EPUVdxeXUAA597w

Video ya tuhuma kwa Godbless Lema

IKO HIVI ANAENDA MAHKAMANI
WANASIMAMISHA HILO.ZOEZI LA.KUMFUKUZA
KESI ITAAMULIWA OCTB 31-2020
STY TUNED
CHAMA.CHA WATU SO MTU
 
mm nasema kwa uhakika kabisa TUNDU LISU alimiminiwa risasi kwa order ya mkubwa baada ya kuonekana anampinga. ben sananane, mawazo, gwanda, kagoye na wengine wengi (rejea maneno ya pr. kabudi akiwa BBC house)
Thibitisha tuhuma zako.
 
bilashaka wewe ni mamini wa dini hizi za mapoke (uislam/ukristo) nani amethibitisha uwepo wa mungu hadi uende KUABUDU?
Mimi ni Mkatoliki.

Wakatoliki tunafundishwa na tunaamini kuwa Mungu ni mkubwa kuliko akili na uwezo wa kuelewa mambo wa mwanadamu.

Hatuwezi kumthibitisha, ndio maana tunaamini. Imani ni uhakika wa mambo yatarajiwayo, bayana na yasiyoonekana.

Hata hivyo tunaweza kuelewa, kwa akili zetu ndogo, uwepo wa Mungu kupitia effects zake mbalimbali katika maisha. Hivyo, suala la Mungu ni la kiimani zaidi, na Mungu anaweza kuelezeka kupitia effects zake.

Kwahiyo mkuu na wewe unaamini tu kuwa Tundu Lissu alifanyiwa huo unyama. Kwamba hilo nalo ni swala la kiimani?
 
Back
Top Bottom