Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiziguzigu Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Mwl. Martin Runaku Mpemba, amefariki usiku wa Aprili 3 katika Kijiji cha Kibingo Kata ya Kiziguzigu, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma, Christopher Palangyo, amesema CCM imesikitishwa na tukio la kifo cha Diwani Mpemba, ambaye ameuawa baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani wakati akitokea sokoni kurudi nyumbani kwake.
Katibu Palangyo amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wauaji wanapatikana haraka na kuchukuliwa hatua za kisheria, na kwamba mauaji ya namna hiyo hayakubaliki katika jamii iliyostaarabika, hivyo uchunguzi wa haraka ufanywe ili kuondoa mashaka na wasiwasi, ambao umewakumba wananchi baada ya tukio hilo.
Palangyo ambaye amewasilisha Salamu za pole za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi kufuatia msiba huo, amesema Chama kinaungana familia, Wana-CCM na wananchi wote katika msiba huo.