TANZIA Diwani wa CCM Kiziguzigu auawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali Kigoma

TANZIA Diwani wa CCM Kiziguzigu auawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali Kigoma

Kuna dalili kuwa viongozi wanao patikana kupitia CCM kuongoza wananchi wote walichaguliwa na minority ila wanatawala majority!
 
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiziguzigu Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Mwl. Martin Runaku Mpemba, amefariki usiku wa Aprili 3 katika Kijiji cha Kibingo Kata ya Kiziguzigu, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma, Christopher Palangyo, amesema CCM imesikitishwa na tukio la kifo cha Diwani Mpemba, ambaye ameuawa baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani wakati akitokea sokoni kurudi nyumbani kwake.

Katibu Palangyo amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wauaji wanapatikana haraka na kuchukuliwa hatua za kisheria, na kwamba mauaji ya namna hiyo hayakubaliki katika jamii iliyostaarabika, hivyo uchunguzi wa haraka ufanywe ili kuondoa mashaka na wasiwasi, ambao umewakumba wananchi baada ya tukio hilo.

Palangyo ambaye amewasilisha Salamu za pole za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi kufuatia msiba huo, amesema Chama kinaungana familia, Wana-CCM na wananchi wote katika msiba huo.

Kumbe na maccm yanauawa!
 
Chadema wavunje magenge yao ya uhalifu
 
Kifo ni kifo tu.
Inakuaje mtu kuchaguliwa Kwa kura na wananchi,Bado wale wale walio kuchagua waje kukuua?
Bwana yako Yesu ilikuaje ni mtetezi wa wanadamu na akauliwa kwa kuning'inizwa msalabani?
 
Yalianzia kwa watu wa CHADEMA na sasa yamehmia CCM , kiukweli mambo yawasiojulikana siyo yakufumbia macho ndugu zanguni serikali ifanyie kazi swala hili , apumzike kwa amani Diwani wetu ,daima nitamkumbuka kuna KIPINDI NIMEWAHI KUSHIRIKI NAE SEMINA YA KILIMO KILICHOKUWA KINASIMAMIWA NA NYAKITONTO YOUTH DEVELOPMENT.
 
Siasa za kumwaga damu CCM wameziansha wenyewe, sasa ngoma imetua nyumbani tulisema humu kuwa likishachanganya hakuna atakaebaki salama, itakuwa ni Tit for tat CCM wakiua na wao wanauwawa until full blown civil war.
 
Back
Top Bottom