Dizasta Vina anaweza akawa ndio best rapper Tanzania

Anakwambia

"Harmonize kaja jana na leo anakaa Masaki
Anavaa mashati, siku hizi hafanani kukaa Masasi"

Hahaaaaaa.

Nimecheka saaana hapo.
 
Huwa na nyimbo zake zaiidi ya 120,

Hivyo Mood ikiwa bomba huwa namsikiliza vyema.
 
Mimi si nawasikiliza tu.

Sisi ndio foundation wao walitusikiliza sisi kabla hawajawa hapa.

I was there when it all started, with Kwanza Unit, Hard Blasters, GWM,O Juice etc.

Back in the early nineties.
Safi sana,
Enzi za Kwanza Unit(Mashimo ya mfalme Suleiman-Msafiri) Nilikuwa bado bwana mdogo sana.


Lakini baadhi ya nyimbo za Hbc na Kwanza Unit na n.k ninazo , Huwa maramoja -moja nazitegea sikio.
 
Anakwambia

"Harmonize kaja jana na leo anakaa Masaki
Anavaa mashati, siku hizi hafanani kukaa Masasi"

Hahaaaaaa.

Nimecheka saaana hapo.
Hahaha.

Unju anavituko sana,kucheza na maneno na kufanya yalete maana na furaha si kazi ndogo kabisa.

Kuna ngoma moja alikuwa akimdiss Ney wa mitego hiyo ndio inavituko balaa...
Moja ya mashairi yake.

"Kanga moko ndembe-ndembe laki sipesa/
Kila akikatiza mamende wanabaki na presha/
Ahaa Jamani ney ama kweli maanani hakosei/
Massita du mitaani hawaongei/"

Katoboa kitovu katoboa ulimi vikuku miguu yote kope utadhani jini/

Anataka atoke na mimi naogopa tope lakini/


Hizi nyimbo wakati mwingine zipo vizuri zinafikirishi na kuburudisha.
 
Huyu jamaa BASATA wangekuwa wanamuelewa angefungiwa hahaa.

Bora kawazidi misamiati na flow.
 

"Kama unatafuta kiki, vuta kiti
Waza "Mbona nna sura mbaya, halafu kufa sifi?""

Jamaa anaweza kuwaharibia watu afya zao za akili.
 
Huyu jamaa BASATA wangekuwa wanamuelewa angefungiwa hahaa.

Bora kawazidi misamiati na flow.
Labda BASATA vichwa vyao ni vizito sana.

BASATA hawasongi mbele,Mpaka wasukumwe Nyuma.

Baba Malcom ana-flow kali mpaka jigga ham'wezi.
 
"Kama unatafuta kiki, vuta kiti
Waza "Mbona nna sura mbaya, halafu kufa sifi?""

Jamaa anaweza kuwaharibia watu afya zao za akili.
Hahaha,Kwakweli Ubongo wako kama ni mzito, jamaa anakuacha mweupe ka'mkorogo.
 
ni hisia zako tu mkuu zilizokusukuma kufuta nyimbo za fid q nakuhusu kuwa rapper mahili pia bado anasafar ndefu kidogo aisee.....
ila dizasta vina kwenye wimbo wa kanisa ameongea vitu muhimu kule
"Kanisa utachomwa moto nakuapia"
 
Bora hata ungetafuta mtu mwingune.
Si kumlinganisha na Mwanamalundi.

Au unafanya tathmini uone ni jinsi gani Fid Q anakubalika kwenye ulimwengu wa HipHop.

Yaani Sangara unamlinganisha na kidagaa!
Kamanda wangu,

Yupi unataka tumfananishe na Fid q....ili iwe sangara kwa sangara.
 
Siwafichi mpaka sasa Dizasta vina anaweza kuwa best real rapper Tanzania....take time umsikilize...Huyu jamaa kanifanya nifute nyimbo zote za wasanii kama kina Fid Q kwenye playlist yangu.
Ahsante..Heshima kwake disazta vina.


Kwa mtazamo wako na maoni yako vitu gani unaviona au mambo gani au uwezo gani unaouona mpaka kutaka kuhitimisha yakwamba dizasta vina anawaacha mbali wasanii wenzeka..?

Unaweza kuorodhesha vitu vinavyomtenganisha na wasanii wenzake, sio mbaya ukifanya hivyo.
 
1.anaimba uhalisia hasa vitu ambavyo watu wengi wanaogopa kuvizungumzia
2.anaimba ngumu hayuko soft kama wengine ambao wakati mwingine unashindwa kutofautisha kama wanaimba hip hop au Bongo fleva
3.Mwandishi mzuri
4.Anajua kujenga hoja ya kile anachokiimba ukamwelewa
5.Watu rika zote wanaweza sikiliza mziki wake
6.Nyimbo zimejaa mafunzo mazuri kwa jamii
7.Mpangilio wa vina na mizani uko vizuri
8.Amelenga sana kuelimisha
 
Nilichoelewa unamkubali FID Q... kuliko kawaida sema tu Umekuja kivingine
 
Nikisilizaga pini za Baba Malcom, huwa naenjoy sana swahili rap. The guy is really talented.

-Kaveli-
Anajua kucheza na lugha, halafu mara atokee msela kupitiliza, mara katokea meneja anawaeleza wenzake jinsi ya kufanya biashara ya muziki, mara katokea kawageuka wahuni anawaponda wanavuta sana, yani mda wowote anaweza kubadilika tu halafu yupo on key.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…