Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Ngoja ngoja ngoja subiri kwaanza, ni mchafuko wa dhambi dunia sasa inanuka, uchawi gani wa kunirushia paka.....sema weka tenaaaa
 
Kuna ile ya shemeji!
Nimemkumbuka Marehemu Omary Omary na Juma Mpogo,

Omary aliimba nyimbo ya kumkumbuka rafiki yake aliyepata ajili pale Mataa ya Buguruni aligongwa na semi lilikuwa likitoka bandarini...Moja nyimbo za mchiriku niliwahi kuipenda kupita maelezo...RIP Omary Omary
 
Hongera sana kwake Majay. Hatimaye na mimi uwa nasikiliza hizi nyimbo haswa za Msaga Sumu... Jamani unanitega shemeji unanitega shemeji ni wimbo mzuri
 
Ngoja ngoja ngoja subiri kwaanza, ni mchafuko wa dhambi dunia sasa inanuka, uchawi gani wa kunirushia paka.....sema weka tenaaaa
Hahaha hii ya nani na inaitwaje?
 
Jambazi
Hawa nao ni wachawi tuu sijui wanataka tumsifie nani na kwa lipi? Mi nilifikiri wanapinga nilicho andika kumbe wanachukia mwenzao akisifiwa kwa jambo alilo lifanya...Teh Teh
 
Nimemkumbuka Marehemu Omary Omary na Juma Mpogo,

Omary aliimba nyimbo ya kumkumbuka rafiki yake aliyepata ajili pale Mataa ya Buguruni aligongwa na semi lilikuwa likitoka bandarini...Moja nyimbo za mchiriku niliwahi kuipenda kupita maelezo...RIP Omary Omary
Hizi ndio unifanya ni msikilize kila siku kicheko...! Huwa zunauzunisha sana na zinapeleka mbali sana...!
 
MKUU HUU MTINDO MPYA WA UIMBAJI UMEKUWA BURUDANI TOSHA SANA
Hakika kabisa mimi ndio maana nimemshukuru Majizzo maana bila radio zake mimi nyimbo hizi ningesikia wapi!

Nimekuwa mshabiki wa nyimbo hizi!
 
View attachment 353220View attachment 353221View attachment 353222


Wasalaam wana jamvi!

Ni ukweli usio pingika kuna muziki fulani uliokuwa umezoeleka ndio unatakiwa kupigwa radioni na hii ilikuwa ni uniform za Radio zote kana kwamba ilikuwa ni sheria ambayo imewekwa!

ilikuwa ni vigumu na hakuna uthubutu wa miziki ya mnanda ,visingeli na mchiriku kusikia ukipigwa radioni na sio kwamba hauna mashabiki bali una mashabiki wengi sana sema radio muda mwingine hulazimisha walaji kula hata wasicho kitaka!

Dj Majizzo baada ya kuanzisha kutuo cha E-FM imekuwa kama mkombozi wa miziki yetu ya asili na wamekuwa wakiupa muda wa kutosha kuupromote kiasi kwamba hata walio kuwa hawajui uzuri wake sasa wanaelewa!

Mimi sikuwa mshabiki wa miziki wa namna hii lakini sasa nimekuwa kama teja maana kwakweli nyimbo hizi kuna zenye jumbe nzuri sana kiasi kwamba ukisikiliza una hamasika hakika!

Kupitia DJ majizzo (E-FM) leo hii sasa nyimbo za mnanda,mchiriku na singeli zimeanza kusikika kwenye radio nyingine na wasanii hao wanapata showa kitu ambacho hakikutegemewa!

Leo hii ukisikiliza East africa radio utasikia wakipiga nyimbo hizi na hata Clouds na kwenye matamasha tunaona wasanii wa minanda,mchiriku na visingeli wanapewa show tofauti za zamani wale wa bongo fleva ndio walikuwa wanakula hela peke yao!

Ni wazi kabisa Wasanii wa minanda ,mchiriku na visingeli wanapaswa kumshukuru Majizzo kwani amechangia sana kwenye mafanikio yao na mapinduzi yao!

Mimi nimshukuru tuu Majizzo kwa kuwasaidia vijana hawa na kuupa thamani mziki wao!

Karibuni Wana jamvi!
Enzi za kampeni, sholo mwamba alinrusha na hiki kitu:
 
Hainaga ushemeji hiyo tunakulaga.
Hatari sanaaaa
 
Back
Top Bottom